Wanafunzi vyuo vikuu waishukia UVCCM. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi vyuo vikuu waishukia UVCCM.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jan 31, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mawaziri wa mikopo katika serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu jana waliitisha kikao na kuutaka umoja wa vijana wa ccm kuacha kuingilia utendaji wa bodi ya mikopo na kutoa ushauri usio na tija wa kutaka bodi hiyo ivunjwe bila kushauri hatua mbadala. Tamko hilo lilikua na jibu kwa UVCCM ambao kupitia mjumbe wake zamaradi kawawa uliitaka serikali ya chama cha mapinduzi kuivunja bodi ya mikopo kwa kua imeshindwa kutimiza majukumu yake. Wakiongea na waandishi wa habari mawaziri hao wa mikopo waliionya uvccm iache kujitafutia umaarufu kwa kua bodi ya mikopo sio mali ya uvccm. Walisema ushauri uliotakiwa kutolewa ni wa kuboresha bodi hiyo. Aidha mawazili hao wa mikopo wameiomba serikali kuongeza pesa za kujikimu na malazi kutoka sh. 5,000 hadi sh 10,000 kutokana na kuongezeka kwa garama za maisha. Source: itv news sa mbili usiku jana. .
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Kisomi zaidi.

  Safi sana. Wanajitafutia umaarufu tu hao. hawana lolote.

  Wakiitisha maandamano tuyapotezee. waandamane wao watoto wa mafisadi
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Si wawafuate huko kwenye vikao vyao na wawatie adabu?

  Hawa dawa yao ni KUWALIA maharage na MAYAI na kwenda pale kuachia GAS hadi wakimbie wenyewe.

  Sidhani kwa sababu hiyo kama wataitwa FFU.

  Ingelikuwa UK, basi jamaa wangelienda na kuwavulia kabisa nguo na kuelekeza makalio yao kwao kabla ya kuachia BOMBA la nguvu ili kuwatoa ndani NGUCHIRO hao.

  Inabidi kuanza kutumia mbinu za kupigana za Wa-Asia yaani unamshinda mtu bila kutumia neno wala kumpiga.

  Wakiitisha Maandamano, tupokee hela na twenda ila tuweke vidole viwili mbele.....

  [​IMG]

  Ridhiwan anashindwa nini kwenda kumwambia baba yake AACHIE NGAZI?

  Hii danganya toto waipeleke huko CCM pekee.

  Huyu Bashe asijifanye ana kimbelembele sana. Kama CCM walimla nusu, Pipo Pawaa itamla mzima.

  Kidumu chama cha ............enhhh!!! MASHANGINGI????
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi sana kama mawaziri hawa wamejuaa ujanja wa kitoto kushupaliaa bodi wkt hawala suluhu....hoja zao zote zimepanguliwa kama.....karanga za saida....wangekuja na suluhisho zaidi ningesema hawa hawako kijiweni kupoteza muda....wangekuja na research na comparison za nchi zinazokopesha kama sisi warelebishe na wagundue makosa ya wapi.....wakumbuke baba yao alisema kosa liko busket fund...wana mix pesa za bodi na za wizara....unafikiria yeye hajui kuwa wanapewa pesa kidogo????waache siasa za kitoto haoo....kwanza uwezo nmdogo sana kama wazazi wao wangetuliaa kama fadhila rz1 ameshalipa kwa beno anataka nini???hiyo pass ni ya kubebwa sembuse angeachwa mwenyewe??watuliee huyo zaonab angetafuta shule akasome atulie!!!!
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  UVCCM wanatuzuga ili watanzania waone mmbaya ni bodi ya mikopo na sio serikali ya CCM. wamwambie JK aiwezeshe bodi na sio kuitupia lawama bodi. THEY ARE TECHNICALLY PLAY POLITICAL GAME ILA WAMEKOSEA TUMESHAWASTUKIA
   
 6. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Asanteni mawaziri wa vyuo vikuu kwa kugundua unafiki na uzandiki wa hao akina ridhiwani na kundi lao wanahitaji kupata sapoti yenu watoseni kwani baba zao ndio wanasababisha nyie msome kwa shida
   
 7. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  wanatekeleza maagizo ya slaa kwani aliahidi kuivunja bodi na kuanzisha uhuru fund
   
 8. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  mwaka wa tabu huu kweli,wamewatuma mashehe watuvuruge maasikofu kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! wametuma uvccm kichapo kibayaaaaaaaaaaaaaaaa! wamemtuma nimrod mkono nae chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! hapapo mpakushika mwaka wa tabu huuu kweli! Nyerere alikukataaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Yeah hii ni nzuri bora wameamua kuwashushua uvccm, wana ajenda yao ya kutafuta umaarufu but wanaamua kupitia matatizo ya wanavyuo!
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanaona manavyuo sasa hawaganganyiki! Sasa wanaona kutupa karata ya lawama ya BODI MIKOPO ili kuwachoka kiulaghai wanafunzi vyuo vikuu.Ni mkakati maalumu ulioundwa na ccm baba kutumia uvcc baada ya kuona umaalufu wao umeisha. Tunawashukuru mawaziri hawa kwa kuwa wameonesha kuelevuka na kuwa wapembuzi wa kauli za kinafiki. Huwezi vunja BODI ya MIKOPO wakati huna suluhu na namna ya kuiunda. Ukweli ni kuwa BODI haiwezeshwi na serikali ipasavyo na inaendeshwa na wanasiasa zaidi-ccm.
   
 11. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaonekana hawajui watendalo. Bodi ihiyo imeundwa na serikali ya chama chao wenyewe, sasa unaandamana ili iweje? Pia hawakufanya utafiti wa kutosha ili kuona kama wanachuo ambao ni waathirika wa suala hilo kama wako tayari kuandamana au la. Au kuna watu maalum wanaowataka wao wawekwe katika bodi hiyo kwa malengo yao mengine wanayoyajua wao? Au kuna lengo jingine la ku 'divate attention' ya wananchi katika masuala muhimu zaidi yanayojadiliwa hivi sasa? Lakini lipo tatizo jingine la msingi katika jumuiya hiyo ambalo huenda wenyewe hawalifahamu, ni kwamba hakuna kiongozi yeyote mwenye mvuto wa kiuongozi 'charismatic' na mwenye 'convincing power'. Hivyo hata kama itatokea wakazungumzia jambo zito na la msingi watu hawatashtuka. Tatizo la Uongozi wa kupeana.
   
 12. K

  Kakulwa Senior Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama mambo yenyewe ndiyo haya,wacha wengine tuendelee kusotea makaratasi mpaka kieleweke
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Safi sana Samir Nasri. Ukweli ndio huo
   
 14. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyo Ridhiwani Kikwete si aliombwa na babake ampigie kampeni? Ameshindwaje kushirikiana na mama amshauri mzee avunje hiyo bodi?
   
Loading...