Wanafunzi hawa waliopata zero wanaenda wap?

Ingetakiwa abayepata Div 4 asiruhusiwe kwenda chuoni, arudie (ku reseat) ili apate sifa za kwenda form 5 au chuo/Veta. Kumpeleka Div 4 chuoni ni kuzidi kuongeza tatizo.
 
Kwani diamond sio mtu, we ndo umeleta ujinga wa ajabu wabongo sisi tunaakili fupi kinoma
Siwezi kujibizana na wewe kwa fact kwa sababu unaonekana tu haupo timamu. Na dalili kuu ya kutokuwa timamu ni huyo Role-model wako uliyemuweka hapo kwenye Avatar yako ni mvuta bangi... (MUNGU wa WAVUTA BANGI DUNIANI)

Wavuta bangi hawanaga akili! Lazima kidogo ziwe zimecheza... 😊
 
Alafu akisha enda form 5 au aka re seat ndo inakuaje akimaliza Hata huyo wa zero kashatoa ujinga kichwani kila my anaenda shule kupata kitu flani sio WOTE Wana lengo mmoja,, Mimi vyeti vyote viko ndani Wala sijawahi tembea na Cheri kuomba kazi anywhere shule nilifata vitu vingne sio nitoke nianze kuzurura naomba kazi ,, si ajabu nilisoma sababu wazazi hawakutaka kunipa pesa ya chuo mkononi nikazisake mapema hawakuweza kunipa 1mil cash nisisome Tena nikapambana kitaa ila walikuwa tayari kulipa 2.5M kwa mwaka kwa miaka mitatu huo ndo utofauti

Na huwezi sema miaka yote minne kapa ..huo mtihani haujaanzwa fanywa form 1 ,, means kapita huko pote vizuri ,, ila mwshoni mtihani wa kumaliza kazingua kila la kheri kwao ..na hao unaowaona wamepata zero ndo watakuwa maarufu badae na hao wa 4 div watatoa ajira kwa wenye dv 1 na 2 na 3 badae
 
Usiingize Ujinga kwenye Discussion zenye mantiki. Huyo Diamond wako ana secret zake zilizomfanya afike pale... usipende kudanganyika na kuhadaika na mafanikio ya watu usiowajua kiundani. Fikiri kama mwanaume mwenye akili timamu. Shauri yako!
Mkuu umeongea kwa uchungu sana,binafsi km mtu Mzima nimekuelewa sana.
 
Ni makosa sana kupeleka failure VETA... atakuwa na ubunifu gani huyu?
Ukienda kule TEMEKE Ilipo Mgulani VTC na VETA na ukawaona wale vijana wanaosoma kule utaumia sana na kuona sijui TANZANIA yetu inakwenda wapi 😔
Kijana uelewa wake ni finyu mno! Sasa sijui tunaanda kitu gani jamani 😔😔😔
 
Twende huko nchi za Scandinavians tuwape consultancy waje wauchambue mfumo wetu wa elimu, matatizo na changamoto zake and then watuandalie mfumo mpya unaoweza kuendana na mazingira yetu. Hawa jamaa wako vizuri mnoo kwenye elimu, tusione aibu jamani sisi wenyewe tumeshashibdwa.
 
Wataenda kujiajiri na kufanya biashara binafsi , suala la kutoboa kwenye maisha haliangalii ulipata div 1 or 2 japo elimu ni muhimu sana ila ya kibongobongo ukijichanganya unaajiriwa na mwenye 0
 
Unaonekana ulifeli shule wewe.. maana huna lolote unaloongea bali ni kutetea wanaofanya mchezo na shule. Nani alikwambia kuna michujo shule za namna hiyo ambazo zinazalisha Zero nyingi?! Ukianza utamaliza tu! Na ndo matokeo yake hayo...

Usitetee ujinga tunazalisha Taifa la vijana wajinga KWELIKWELI! na kaa usome tena sikuongea kuwaponda na kuwavunja moyo ambao hawakufanya vizuri shuleni.
 
Kurasini mhhh basi ndio maana
 
Tatizo lako unashindwa kuelewa umuhimu wa kuelimika au kuwa na jamii iliyosoma. Hakuna kitu kigumu na cha hatari kama kuwa na jamii isiyo na elimu. Hata kuishi mitaani vizuri ni rahisi ukiwa umeelimika kuliko kuwa mbumbumbu..
 
Mnataka mfauli bila kusoma acha ujinga na uvivu
 
Kupata zero Ni ujinga ,, Kuna uhusiano gani Kati ya kushindwa au hujaamua kariri ulichofundishwa uko busy na Mambo mengne dhidi ya akili yako binafsi,, kwa hio wewe uanamini kuwa mwenye div 1 ana akili kubwa kuliko div 0
 
Hizo shule zipo hapahapa post ya kariakoo au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…