tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,932
- 18,391
Du hiki chuo kilifaa kiwe Saudia, sio TZ.Wanafunzi saba wa chuo kikuu cha waislamu Morogoro wamekatisha masomo yao kwa kufukuzwa chuo hapo kwasababu mbalimbali, sita kati yao wamefukuzwa moja kwa moja wasirudi chuoni na mmoja amefukuzwa kwa muda wa muhula mmoja.
Akizungumza jana mara baada ya swala ya ijumaa iliyofanyika chuoni hapo, mwenyekiti wa kamati ya nidhamu chuoni hapo Sheikhe Abdul Kassim Jiba alisema wanafunzi hao wamefukuzwa kwa makosa tofauti ikiwemo ugomvi lakini wengi wao wamefukuzwa kwasababu ya mahusiano (Mapenzi).
Pia Shekhe Jiba alitumia muda huo kuwaasa wanafunzi chuoni hapo kufuata sheria za chuo ikiwa pamoja na kutojihusisha na masuala ya mapenzi ,pia hairuhusiwi kutembea au kukaa wawili mwanamke na mwanaume isipokuwa awepo mtu wa tatu.
Kwa mujibu wa sheria za chuo hicho ni kosa kwa mwanafunzi kuwa na mahusiano ya kimapenzi ukiwa chuoni au likizo nyumbani isipokuwa kwa mke au mume. Kama umeoa au kuolewa unatakiwa kuwasilisha cheti cha ndoa kwa uongozi wa chuo ili kutambua uhusiano wako.
My Take:
Vyuo vingine viige huu utaratibu ili kurejesha maadili kwa vijana wetu na kupambana na janga la vijana kujiingiza katika ngono.