Wanafunzi 59 wa Chuo cha VETA Kagera na wakufunzi wao 3 mbaroni kwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera inawashikilia wanafunzi 59 wa Vyuo viwili vya ufundi VETA kwa madai ya kukutwa na simu za mkononi katika chumba cha mtihani.

Mbali na kuwashikilia wanafunzi hao wa Chuo cha Veta wilayani Muleba na kile cha Veta Tuinuane kilichopo Bukoba vijijini, taasisi hiyo pia inawashikilia walimu watatu na kukamata Sh151,000 zinazodaiwa kuchangwa na wanafunzi kwa ajili ya kuwapatia wasimamizi wa mtihani.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Desemba 15, 2020 na Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kagera, John Joseph katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Ametumia mkutano huo kuonyesha simu hizo na kubainisha kuwa wanafunzi wa chuo cha Tuinuane ni 21 na Muleba wapo 38.
 
Daaa!!! Hivi jamani elimu yetu inaelekea wapi? Very soon,we will have no alternative, except to allow expatriates from outside! Unapeleka gari gereji kumwaga oil, baada ya wiki imenoki.
 
Wanafunzi 59 wamejichanga wakakusanya 150,000 tu. Kwanza wizi ni wa kijinga na kutumia simu ndio kabisa wasimamizi wao wamezembea vibaya.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kagera inawashikilia wanafunzi 59 wa vyuo viwili vya ufundi VETA kwa madai ya kukutwa na simu za mkononi katika chumba cha mtihani.

Mbali na kuwashikilia wanafunzi hao wa chuo cha Veta wilayani Muleba na kile cha Veta Tuinuane kilichopo Bukoba vijijini, taasisi hiyo pia inawashikilia walimu watatu na kukamata Sh151,000 zinazodaiwa kuchangwa na wanafunzi kwa ajili ya kuwapatia wasimamizi wa mtihani.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Desemba 15, 2020 na mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Joseph katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Ametumia mkutano huo kuonyesha simu hizo na kubainisha kuwa wanafunzi wa chuo cha Tuinuane ni 21 na Muleba wapo 38.
Laiti tungejua kati ya hao wanafunzi wa kike ni wangapi na wakiume ni wangapi, tungechimba zaidi.., anyway mpaka hapo kuna harufu ya rushwa ya ngono. Ngoja tusubiri ripoti. Ninavyoviona vibinti vya VETA na Vijana waalimu wa VETA ni kitendawili kidogo..
 
Back
Top Bottom