Wanafunzi 11 shule iliyoungua moto Geita wafukuzwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
geitapic

Kufuatia matukio matatu ya moto katika Shule ya Sekondari Geita ndani ya siku saba na kusababisha wanafunzi watatu kujeruhiwa, maabara na darasa kuteketea kwa moto, mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule ameiagiza bodi ya shule hiyo kuwafukuza wanafunzi 11 waliobainika kuwa na makosa ya jinai.

Akizungumza leo Jumatano Julai 14, 2021 katika shule hiyo, Senyakule amesema uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa kuchunguza matukio ya moto imebaini mambo mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa wanafunzi na matukio ya kijinai.

Amesema mbali na hao 11 wapo wengine 24 ambao bodi ya shule imetakiwa kuwapa adhabu ya kurudi nyumbani siku 30.

“Hawa wanafunzi 11 wamekutwa na makosa ya jinai walikuwa na visu, wana makosa ya kubaka na makosa mengine mengi ya kijinai wapo ambao walishajadiliwa na bodi na shule hawa washtakiwe kwa makosa ya jinai sio tu kufukuzwa shule, “ amesema Senyamule

Amemtaka katibu tawala wa mkoa kumchukulia hatua za kinidhamu mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu 13 walioshindwa kuwajibika kwa mambo muhimu na kutaka kuwabadilisha kituo cha kazi ndani ya siku saba.

Pia amezitaka kamati za usalama kwa kushirikiana na shule kuweka alama kwenye mabweni yote ya shule ili moto unapotokea usilete madhara na kutaka ulinzi shirikishi uimarishwe ili kuzuia matukio yasiyo ya lazima.

Katika hatua nyingine walinzi wa shule hiyo wamefukuzwa kazi kutokana na uchunguzi kubaini hawana mafunzo ya usalama na hawakupitia Jeshi la Akiba la Mgambo.

Mwananchi

Pia soma >
 
Haya maamuzi aliyofanya huyu mama yanaweza kuwa ya kukurupuka........siku mbili tu hizo amejiridhisha na kufanya hayo maamuzi yooote
 
“Hawa wanafunzi 11 wamekutwa na makosa ya jinai walikuwa na visu, wana makosa ya kubaka na makosa mengine mengi ya kijinai wapo ambao walishajadiliwa na bodi na shule hawa washtakiwe kwa makosa ya jinai sio tu kufukuzwa shule, “

Visu shuleni ni ajabu?

Mengine yanafikirisha, Uchunguzi umefanyikaje huu au ni mashauzi tu?
 
Makosa yao ya muda mrefu yamehusishwa tu Na tukio la moto.

Nakumbuka enzi zetu kulitokea tukio la Mwl Mmoja wa kike kutukanwa sana kwa kuandikwa kwenye choo vya wanafunzi.

Katika kuwatafuta wahalifu Sasa wa tukio la matusi ,walimu Wakaanza kukamata wanafunzi wachoraji wote, viburi,wachelewaji ,wachafuaji wa Kura za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi n.k

Ni mfumo wa kuhusisha tu Na ni wa kizamani sana.
 
Kama ni watuhumiwa, unakuwaje wafukuzwe shule.

Kwanza hata hawajakamatwa na kutumiwa na Polisi wala ofisi ya mashtaka.

Mama ametafuta KIKI.
Walinzi wote wa Shule Tanzania wamepitia Mgambo ?
 
Sasa hapo ndio wamewafunza nini,
Ingawa kuna wanafunzi wengine ni manunda lakini kazi ya shule nini
Kazi ya shule ni kuwapatia elimu tabia utawafundisha wewe nyumbani. So wameletwa uendelee kuwafundisha tabia nzuri wakinyooka watafutie shule nyingine unasikia wewe mzazi eeh.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom