WANAFUNZI zaidi ya 1000 wapo hatarini kufukuzwa katika Chuo cha Usimamaizi wa Fedha [IFM] baada ya kubainika kukosa sifa za kujiunga katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa chuo hicho na kubandikwa kwenye mbao za matangazo wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza ambao majina yao yaliorodheshwa walitakiwa kuwasiliana na uongozi huo.
Taarifa hiyo ilikwenda sambamba na kutajwa kwa wanafunzi hao ambao hawakuwa na sifa kwenda kwa msajili wa chuo kuhakiki majina yao na kuwasilisha vyeti vyao vya kumaliza elimu ya sekondari.