Wanachuo 300 wajiunga CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachuo 300 wajiunga CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Mar 21, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na Grace Macha, Lushoto
  HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
  Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
  Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
  CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
  Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
  Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.


  NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
  KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kuna shule moja ya msingi vitoto vinalazimishwa kuvaa fulana za njano na scurf za kijani. CCM wanasahau kuwa hao ni watoto na wadogo zetu sisi tulioko vyuoni.
   
 3. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  my MP lema,,, im proud ov u... Piga kazii,,, tafuta wanachama wa kutosha,,mabadiliko nchini tanzania yamabakia kuletwa na CHADEMA tu,, God Bless CHADEMA
   
 4. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  naona CHADEMA inajaa wasomi, vizuri sana, hawa watumike kuelimisha jamii kwenye masuala tofauti, itasaidia kutukomboa kwenye umaskini, watu watafanya maamuzi kwa vitu wanavyo vijua na kuvielewa kwa undani, sio kuburuzwa tu!
   
 5. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM ndo washarikoroga yakhe! Zege ukishalichanganya haliwezi kurudi kuwa cement tena. Hicho ni kifo cha CCM na kaburi lao nawaandalia mimi mwenyewe ili siku ikifika tukawalaze mahali pabaya peponi.
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  tutafika tu...
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Safi sanaaaaaaaaaaaaa safi sana na na na na na na
   
 8. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Amina! I mean na iwe hivyo, CDM kaza uzi mpaka tuhakikishe ccm ikigusa uzi huo inajikata!! Kifo cha ccm kishakaribia, Heko kwa kijana wetu Lema na Nassari endeleeni na huo moto nasi tupo nyuma yenu kuchochea zaidi, tunataka chama kwanza kitishe kwa kuwa na wasomi zaidi. Naiona Tumaini Universities inakuja kwa kasi ya ajabu kutaka mapinduzi ya nchi hii, Sie Makamanda wa Makumira tushafungua tawi na karibu lina wanachama 500. Big up CDM!
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  CHADEMA endelezeni mashambulizi ili mafisadi wazidi kuchanganyikiwa zaidi...
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  namba nzuri sana ukizingatia limefunguliwa juzi juzi tu endeleeni kuhamasisha sijui kwanini wasomi kama nyie muendele kubaki CCM...
   
 11. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  na bado. safari hii tutafika hadi secondary school. vijana wanatuhitaji sana huku. buriani ccm.
   
 12. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ujumbe huu ni mahususi kwa wabunge wote wa CHADEMA bila kujali jinsia au njia walioingilia bungeni iwe ya kuchaguliwa au kuteuliwa.
  Kila mbunge ahakikishe anapata wanachama wapya kwa ushawishi wa aina yeyote.
  HII NDO KAZI YA MBUNGE
   
 13. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ndiyo CDM!! kuna tetesi ambazo sio rasmi nimezisikia mahali nataka wana JF mwe makini kuzichunguza na kuzitafutia tiba iwapo na endapo kweli zitakuja kutimia. tetesi zenyewe ni juu ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Februari 2011, inasemekana kuwa serikari ya CCM ina mpango wenye nia mbaya wa kupunguza ufaulu wa wanafunzi eitha kwa kuficha matokeo ama kuwafelisha wanafunzi kwa kiwango cha kutisha! Adhima na sababu iliyopo nyuma ya kusudi hili ni kwamba Vijana wengi wakijiunga na vyuo vikuu na vyuo vingine moja kwa moja wanaenda kuongeza idadi ya wafuasi wa CDM ambapo upinzani wao dhidi ya CCM unakuwa ni upinzani uliopevuka kiakili na kifikra. Hivyo wana JF natoa tahadhari mapema ili endapo hii hali ikitokea tujue jinsi ya kuwatetea wadogo zetu na wenzetu wa CDM, sio taarifa rasmi lakini inaleta hisia ya kujiweka tayari kwa sababu CCM sa ivi imeamua kuingiza siasa katika maslahi yanayomhusu mwananchi moja kwa moja kama njia mojawapo ya kutaka kujitetea dhidi ya shubiri inayotolewa na CDM. Tusifikiri kwamba ccm wamenyamaza tu kuona vijana wengi vyuoni wakijiunga na CDM na bado matawi yakifunguliwa vyuoni kwa kasi hivi!! CDM tuwe makini!
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mwandishi alisahau kuwakumbusha kuwa Nasari Yoshua alishinda zikachakachuliwa! Hawa vijana wanafanya kazi nzuri sana! Waingie na mitaani na kwenye kila kata kufungua matawi ili kuimarisha chama. Baada ya 5yrs chama kiwe kimefika kila kijiji. Hiyo ndio kazi ya vijana siku zote. Kuimarisha chama! GOD BLESS CHADEMA
   
 15. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  i APPRICIATE THIS
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wazazi nao wanawaangalia tu!!!hiyo shule inajikomba kwa chama tawala!
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mbowe alisema hakuna kijiji ambacho hakitakuwa kimefikiwa na kiongozi wa juu yoyote wa Chadema kufika 2015 na jua CCM kuna sehemu hawajafika kwa zaidi ya miaka 20..
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180

  Duh another smell of sad story from CCM...yaani kama hii inshu ni kweli basi nawashauri CHADEMA msifunguie matawi kwenye mashule ya sekondari, bora hukohuko vyuoni coz ikitokea CCM wakajua kwamba kuna sekondari ina tawi la CDM nadhani madent watafanya kusikia tu abt University, sidhani kama kuna pua itagusa chuo.
   
 19. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Maendeleo ya Chama = Watu + Itikadi, vizuri sana CDM..
   
 20. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Lema wewe piga kazi wenzako wanafikiria posho za vikao dar na dodoma big up sana
   
Loading...