Wanachuo 300 wajiunga CHADEMA

Huu ni mwaka wa kwanza tuu na bado haujaisha, mpaka 2015 tutakuwa tumebakiwa na kazi ndogo tuu ya kusukuma mlevi.
-Jamani hichi chama cha ccm hata kikipewa simtank zima la dawa ya babu hakiponi tena
 
na Grace Macha, Lushoto
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.

NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.

Nimeipenda hii kazi. GO chadema Goo
 
Hao wote wachaga. Mwl alituasa na watu hao. tena wakabilaaaa hao!!!!
 
ebwana naomba chadema muendelee na uzi huo huo, hii ni kudhihirisha kwamba watu ambao kwa kweli wameshajitambua hawawezi kuendelea kujikomba ccm, nafurahia kutangaza kifo cha CCM.
 
jamaní n kazi nzuri sana imefanyika kuongeza wanaharakati wa kuikomboa Tanzani toka kwenye makucha ya mafisadi. Ila kuna vjana wa vyuo wengi sana hapa mwanza wanahtaji kadi za uanachama cdm. Kuanzia saut, bugando, cbe, misungwi na chuo cha uvuvi ngaza. Viongozi tunaomba mśaada wa kufungua matawi na kuonana wanachama.
 
kuna shule moja ya msingi vitoto vinalazimishwa kuvaa fulana za njano na scurf za kijani. CCM wanasahau kuwa hao ni watoto na wadogo zetu sisi tulioko vyuoni.

Ndiyo upwambafu wa sisiem huo. Huo ujanja wa kuvisha watu tshirt na skafu mwisho wake unakaribia. Watanzania sasa wanataka maendeleo siyo sketi wala blauzi.
 
na Grace Macha, Lushoto
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.

NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.

Hapo kwenye red ni chuo cha madini dodoma, sio chuo cha maadili.

hii ni kazi nzuri. tuko pamoja na vijana wetu. haa dodoma teyari matawi ya vyuo yameishafungua akaunti za bank na supporters tunasaidia kuyarun. teyari pia kuna shirikisho la vyuo vikuu kanda ya kati - chadema na ina uongozi. ni vyema vijana hawa wa lushoto wapate mwanachadema academic staff ambaye atakuwa mlezi. either kimkoa au kichuo. atawaonyesha na kuwaelekeza the where smooth path lies.

Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania!
 
This is gud news na demokrasia ya ukweli vyuoni. Nakumbuka chuo nilichokuwa mimi kama wewe sio CCM unabaguliwa kwenye mambo mengi kisa serikali ya wanafunzi walikuwa CCM watupu. Trip za kwenda kutembelea Bunge kama wewe sio mwana CCM huendi, unaonyesha kadi ya CCM kwanza ndio unasajili jina kwenda bungeni. Pakupeleka malalamiko hakuna. Wengi tulichukua kadi za CCM ili twende kutembelea bunge kipindi hicho na bado tukaachwa kwenye mataa na kadi zetu.

CHADEMA tembeleeni vyuo vyote mna wafuasi wengi sana.
 
niliziskia speech za Lema na Nassari Joshua, hawa jamaa wapo vizuri na wana vision ya tanzania nyingine chini ya dola ya chadema. Very inspiring. Kazeni buti tupo nyuma yenu mpaka ukam ilifu wa dahari. aluta continua
 
na Grace Macha, Lushoto
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.

NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.

mbona chuo kikuu Mzumbe kimesahaulika?? CHADEMA msiache kwenda Mzumbe though ni ngome ya CCM, nina uhakika vijana wengi wanawaunga mkono kule.
 
Duh another smell of sad story from CCM...yaani kama hii inshu ni kweli basi nawashauri CHADEMA msifunguie matawi kwenye mashule ya sekondari, bora hukohuko vyuoni coz ikitokea CCM wakajua kwamba kuna sekondari ina tawi la CDM nadhani madent watafanya kusikia tu abt University, sidhani kama kuna pua itagusa chuo.

you have a point.
 
huku tunapoelekea chadema tutafika tu kwa njia yyeyote tutamwangusha adui ccm
 
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA). Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa. Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.
 
Huo mpango wa kuhujumu maendeleo ya vijana hata kama utakuwepo hautasaidia,inabidi wahonge na wasimamizi na wasahihishaji wa mitihani,hata kama msimamizi/msahihishaji atachukua fedha itajulikana tu,nani anajua walichopewa wahariri waliokwenda kwa al adawi,lakini mbona tulijua sababu ya kufanya hivo?
 
Nimeipenda, kazi nzuri vijana! Urazini na mapinduz ya kweli huanza na wasomi, so keep it up.
 
Back
Top Bottom