Wanachuo 300 wajiunga CHADEMA

kwa mbali naanza kumwona Mar.Baba wa taifa (J.K.N) akinyoosha vidole viwili juu ...kikubwa anafurahia utabiri wake kwa CDM..

Please Chadema take this,Tabora (Sikonge) ilikuwa ngome ya Cuf ila mara hii wameprove hawana tena chao,imebaki vacuum ya kisiasi make hata mbunge wa leo S.N hapendeki wala hana support yoyote ile...CDM come on, wellcome Sikonge
 
Njooni na Sikonge(Tabora) watu ni wengi hawana uongozi wa uhakika wanaisubiri CDM ..njooni haraka sana
 
kwa mbali naanza kumwona Mar.Baba wa taifa (J.K.N) akinyoosha vidole viwili juu ...kikubwa anafurahia utabiri wake kwa CDM..

Please Chadema take this,Tabora (Sikonge) ilikuwa ngome ya Cuf ila mara hii wameprove hawana tena chao,imebaki vacuum ya kisiasi make hata mbunge wa leo S.N hapendeki wala hana support yoyote ile...CDM come on, wellcome Sikonge
 
mbona hao ni wachache? Ukweli sifurahishwi na kasi ya chadema ktk kupata wanachama wapya, watu walijirejista online hawakupata majibu, hapa chuo 90% ni wapenz wa chadema ila bado si wanachama, nashauri waongeze bidii.
 
mwandishi ulikosea kuweka mwenyekiti badala ya katibu.... ila wote ni makamanda harakati zinaendelea tunampango wa kufungua pale kihonda morogoro tawi la chama, ni harakati mpaka kieleweke
 
DSCN3369.jpg DSCN3375.jpg DSCN3175.JPG DSCN3321.jpg hizo ndizo picha wakati wanachuo wakipokea kadi za uanachama toka kwa kamanda LEMA, HUKOOOOOO LOSHOTO
 
na Grace Macha, Lushoto
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.

NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.
ebu cheki hayo majina yenye nyekundu,hivi viongozi wa chadema lazima wawe watu wa maeneo yenye majina hayo! yani hapo chadema ndo inapoharibu na hicho ndo kitawamaliza kabisa! anyway hongereni pia kwa kupata watoto 300 maana kwenye hicho chuo kuna wanachuo zaidi ya elfu so kupata watoto 300 si haba!
 
Kazi nzuri.....kila mtanzania mwenye nia njema sharti ahunge mkono mbio hizi......
 
Duh another smell of sad story from CCM...yaani kama hii inshu ni kweli basi nawashauri CHADEMA msifunguie matawi kwenye mashule ya sekondari, bora hukohuko vyuoni coz ikitokea CCM wakajua kwamba kuna sekondari ina tawi la CDM nadhani madent watafanya kusikia tu abt University, sidhani kama kuna pua itagusa chuo.
Dah!! mkuu acha uwoga bana!!Ukizitambua haki zako utaweza kuzitetea so kitu wanacho fanya CHADEMA ni kumfanya kila mwananchi aujue wajibu na haki anazo stahili.
Inasaidia nini kupata elimu kwenye mazingira yanayo zidumaza fikra zako? Halafu isifikie hatua tukazifundisha akili kuzoea mazingira dumavu kwa kiwango hiki.
Hii ni Nchi yetu sote na naamini hawana kiburi cha kutuburuza kama wanabisha ngoja tungundue huo mpango mfu wao ..we c uliona ule mtiti wa kule Kanda ya ziwa?Waache tu wabeep waone niaje inakua watu kitaa washajimwagia PETROL cheche kidogo tu inatosha kuihamishia Libya hapa.

Bravo Lema tupo pamoja mwanzo mwisho.
 
Safi sana CHADEMA kwa kazi mnayoifanya,mpaka tunafika 2015 kwenye uchaguzi ujao tunaizika CCM.
 
Dr. Slaa is a gift from god to tanzania,chadema and other high rank members are blessedreminds me of mosses of the islaelits in exodus
jk,lwsa,ra are devilsreminds me of faraos in exodus

always god wins and the hg awaits jk
 
Nani kasema CDM haiwezi kuongoza nchi??? Hapo tayari kuna wakuu wa wilaya wa kutosha, wakurugenzi wa halmashauri na maafisa wengine kibao wa kuwa replace hawa waliopo saizi wenye mtizamo wa kifisadi. Mabadiliko ya kweli Tanzania yanawezekana na yataletwa na wasomi kama hawa waliojiunga na CDM
 
na Grace Macha, Lushoto
HARAKATI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) za kujiwekea ngome kwenye vyuo vya elimu hapa nchini zimezidi kushika kasi baada ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Sebastian Kolowa (SEKUCO) zaidi ya 310 kujiunga na chama hicho.
Wanachuo hao walikabidhiwa kadi za CHADEMA juzi na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho iliyofanyika eneo la Bondeni nje ya chuo hicho.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu wa CHADEMA mkoani Tanga, Benson Mramba, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Henry Kilewo, na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Nasari Joshua, wakazi wa maeneo ya jirani waliomba nao kupatiwa kadi za chama hicho.
CHADEMA tayari imeshafungua matawi kwenye vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo vile vya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo cha Mipango – Dodoma, Chuo cha Maadili –Dodoma, Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT), Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) na wako mbioni kufungua matawi kwenye Chuo Kikuu cha Meru, Chuo cha Maendeleo – Tengeru na Chuo cha Uhasibu –Arusha ( IAA).
Lema aliwataka wanachuo hao kuhakikisha wanakuwa jasiri katika kudai haki zao pamoja na jamii inayowazunguka na wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote na badala yake wajenge tabia ya kuhoji pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliwaeleza wanachuo hao kuwa watumie muda mwingi kuhamasishana kushiriki mijadala ya kisiasa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini, jambo alilosema litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaamsha wananchi wengine.

NAUNGA MKONO KAZI NZURI YA KIJANA GODBLESS LEMA.
KAZA BUTI KITAELEWEKA TUU.

Nice Job...nice focus....GOD BLESS CDM,...GOD bless all the CDMs flock...God bless Godbless Lema, the Arusha MP! Tupo pamoja na pamoja tutafika...Lazima akili zote za kizazi kipya zijengwe ndani ya dira na ukweli ktk ukombozi wa taifa hili lililotekwa na wezi na mafisadi na utawala uliooza.

Focus ya CHAMA iende hadi ktk wale walioko masekondarini yote Mikoa yote na hasa wanaoelekea kumaliza na hata waliomaliza FormIV na wanaoelekea FormVI (those between 15 years to 20 years, ambao ndio future strong members and voters). Vijana hao lazima wapate nao dira sahihi pasipo kuchelewa maana, tukumbuke ndio wao kati yao hasa wamekumbana na uozo wa CCM na sera zake mbovu zilizofanya karibu asilimia 85 ya wanafunzi wa FormIV kufeli vibaya. Ndani ya CDM hakuna sera mbovu na hakutakaa kuwe na uongozi uliooza hivyo ambao unaangamiza akili na future ya vijana wa taifa hili.

Investment on youth is an absolute assurance of strong party, strong future, focus and lenient leadership. That is the future of CDM...keep it running....speedy! WITH PEOPLE'S POWERS....YES WE CAN...!!!
 
iMEKAA VZRI MNOOOOO!!
Popote pale duniani mabadiliko huletwa na wasomi. Mapinduzi ya TZ yataletwa na wasomi kama watamua kujitenga na CCM.
Vijana walioko vyuo vikuu wakiungana kwa pamoja mapinduzi ya kweli yatapatikana.
 
Ndiyo CDM!! kuna tetesi ambazo sio rasmi nimezisikia mahali nataka wana JF mwe makini kuzichunguza na kuzitafutia tiba iwapo na endapo kweli zitakuja kutimia. tetesi zenyewe ni juu ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Februari 2011, inasemekana kuwa serikari ya CCM ina mpango wenye nia mbaya wa kupunguza ufaulu wa wanafunzi eitha kwa kuficha matokeo ama kuwafelisha wanafunzi kwa kiwango cha kutisha! Adhima na sababu iliyopo nyuma ya kusudi hili ni kwamba Vijana wengi wakijiunga na vyuo vikuu na vyuo vingine moja kwa moja wanaenda kuongeza idadi ya wafuasi wa CDM ambapo upinzani wao dhidi ya CCM unakuwa ni upinzani uliopevuka kiakili na kifikra. Hivyo wana JF natoa tahadhari mapema ili endapo hii hali ikitokea tujue jinsi ya kuwatetea wadogo zetu na wenzetu wa CDM, sio taarifa rasmi lakini inaleta hisia ya kujiweka tayari kwa sababu CCM sa ivi imeamua kuingiza siasa katika maslahi yanayomhusu mwananchi moja kwa moja kama njia mojawapo ya kutaka kujitetea dhidi ya shubiri inayotolewa na CDM. Tusifikiri kwamba ccm wamenyamaza tu kuona vijana wengi vyuoni wakijiunga na CDM na bado matawi yakifunguliwa vyuoni kwa kasi hivi!! CDM tuwe makini!

My comments are withheld. However it is not too late ------ get down there! Secondary students mostly have attained voting age. Go go go with the same zeal used for higher learning institutions.
 
Back
Top Bottom