kindikinyer leborosier
JF-Expert Member
- Jan 6, 2018
- 430
- 780
Hello bila shaka mu wazima, poleni kwa wale wenye changamoto za hapa na pale, Mola awape ujasiri wa kukabiliana nao na kuushinda!
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina mchumba wangu, nimemtambulisha mpaka nyumbani na kwa ndugu zangu, sijawahi kufanya hivi kwa mwanamke yeyote, hiki ni kiashiria cha kwanza nilizama.
Changamoto inakuja hapa, mwezi mmoja uliopita hatukua kwenye mawasiliano mazuri, yeye akidai anakua amebanana na kazi, kitu ambacho ni sahihi, na mimi pia nikaamua kuwa busy pia baada ya kumwona mtu haelewi kila siku unapomwambia madhara ya mpenzi kuwa amebanana sana!
Ghafla wiki kama mbili na siku kadhaa zilizopita akanitaarifu anataka kuja mkoa nilipo kuja kulijengea kaburi la baba yake, nilimkaribisha na kumwambia atafikia kwangu, na nilifurahi pia kwani tulikata mwaka mzima unaelekea wa pili hatujaonana, eti tumebanana na kazi za watu.
Hakuniambia tarehe husika anakuja lini, cha kushangaza kesho yake namtafuta, akaniambia yupo stendi anaanza safari, sikua na shida kwa sababu hamna maandalizi ningepaswa kuyaandaa au nahofia eti labda kuna mwanamke angenikuta nae.
Alifika usiku sana, nilimkaribisha na wote tulifurahi sana, kwa kuwa alifika usiku aliwakuta wadogo zangu wamelala chumba chao, hivyo ikanilazimu nilale nae.
Asubuhi kulipokucha wadogo zangu kidogo hawakuelewa, maana haijawahi kutokea hata mara moja anakuja mwanamke analala kwangu, niliwaeleza yule ni nani, na nikawaambia wakae nae nyumbani, walizoeana sana na kufurahi pamoja, mapaka akawanunulia zawadi bila mimi kujua. kwa kuwa mimi nilikua sina likizo nilikua natoka na kurudi jioni.
Alifanya mambo yote kijijini kwao ya ujenzi wa kaburi la baba yake, nahatimae siku anarudi akanikaribisha kwa baba yake mdogo, nikaenda tukakaa tukala, tukaaga na kurudi kwangu!
Kesho yake akaniaga na kurudi kazini, nilimsindikiza akapanda basi, na kuondoka na mambo yakaendelea.
Baada ya kurudi, tukawasiliana sana, hata ule ubize ukapungua, chakushangaza wiki ya pili sasa hapatikani, simu amezima marafiki zake hawampati hewani, nimejiuliza mengi sana, mpaka nimeona pengine labda ndo amepanga tuachane kwa hivyo!
Mwanzo alinipa namba ya mama yake lakini ile namba ilikuja kupotea, nimejiuliza mengi sana, nimekosa majibu, ushauri wenu wana jamvi!!