Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 898
Nikuunge mkono Mwl Moshi kwa yote matatu kimsingi, lakini natofautiana nawe kuwa hata "truth" sio "absolute" ndio maana mambo mengi bado yako debatable. Mambo mengi yanayochukuliwa kuwa "truth" ni makubaliano tu ya jumuiya fulani (wanataaluma, jamii, nk) kuwa yachukuliwe hivyo, na siku ushahidi tofauti ukipatikana kilichokuwa "truth" chaweza kubadilika kuwa sivyo tena (na hivyo wanakubaliana juu ya "ukweli mpya"). Mifano iko mingi. Kwa hili peke yake, si sawa hata kidogo kuzuia watu wasijadili jambo fulani, kwa sababu hata hiyo dhana tu ya kuwa mjadala huo uwepo au usiwepo ni debatable. Kwa mfano tunapozungumzia maisha binafsi ya kiongozi, tunamaanisha nini, na kwa mujibu wa nani? Kujadili afya ya kiongozi ni sawa au si sawa? Kimsingi hakuna mwenye jibu ambalo tunaweza kulichukulia kama "absolute truth" kuhusu swali hili, wengine watasema ni sawa na watatoa sababu, wengine watasema si sawa, na sababu watakuwa nazo, na zote zinajadilika. Kinachopaswa zijadiliwe zote, hoja "nyonge" itajifia yenyewe, na zile zenye nguvu zitabakia.
Labda kama Field Marshal ES anataka kubadilisha slogan ya JF iwe kuwa "We no longer dare to talk openly!" lakini tukumbuke members wengi wako hapa kwa kuwa wanapata nafasi ya ku-ventilate. Jibu la kuwapa hao serikali ni sisi kuendelea kujadili hoja yoyote inayofika ukumbini humu, zile zenye udhaifu zitajifia zenyewe na zile zenye nguvu kimantiki zitadumu na kuleta impact kama ambavyo tayari imeshatokea huko serikalini na kwingineko zitakakogusa.
..ujujmbe wa kamanda ungeweza kuwa na mantiki kama angeutoa kama maoni...yake,lakini umeonekana kama vile serikali inataka kutu dictate...nahisi watu watakuwa mbogo zaidi...i look this in pycho angle!!!
HATA HIVYO SERIKALI WAKITAKA KWENYE WEB YAO YA IKULU WAWEKE FORUM AU PALE TVT..NDIO WAWEKE MASHARTI...MIMI NADHANI WANA JF NI WATU HURU.....HAWASTAHILI KUSHURUTISHWA
Ni vizuri umeleta ujumbe huo ili na sisi tukupe vipande vya kuwapelekea.
Lakini kwa nini wasije wenyewe wanakutuma wewe?
Nauliza hivi kwa sababu hapa JF mtu yeyote anaweza jiunga akasema kile anachodhani ni sahihi.
Nadhani bado unamkumbuka Kaka Mcha, alikuja hapa akamtetea Lowassa kwa uhodari,nguvu na uaminifu wake wote, mwisho kama vile kutabiri anguko kuu la Lowassa aliachia ngazi ili kijiwe kipate kuendelea kwa desturi yake.
Kaka mcha alikuwa na mchango fulani hapa JF,lakini 75% ya hoja zake zilikuwa pumba ambazo zilimlemea akalazimika kuwajibika hapa JF.
Umesema tusijadiri maisha yao binafsi kwa sababu tunawagombanisha na wake zao?
Sidhani kama sababu ya kuongelea maisha yao binafsi ni kuwagombanisha wao na wake au waume zao.
Wao ni Public Figure kwa hiyo Twenty four seven wako Under Scrutiny wanataka au hawataki.
Sababu kuu ya msingi ya kusema maisha binafsi ya Viongozi wa seruikali ya SISIEMU na nyingine yeyote itakayo kuja ni kuhakikisha , maisha ya kiongozi haya create matatizo na tamaa kiasi cha kumfanya aanze kuuza vyandarua vya msaada, au kutumia fedha ya maendeleo vijijini kufanya makongamano ya kukata kwa mundu huko Bagamoyo.
Umalaya ni mzigo mkubwa sana ndani ya nchi.
Umalaya wa viongozi wetu ni chanzo cha tufani nyingi za kujitakia.
Umalaya wa viongozi ni chanzo kikubwa cha kuyumba na kurudi nyuma kiuchumi kwa Familia za viongozi , jamiii na Taifa kwa ujumla.
Umalaya wa viongozi wetu ni gharama ya nyongeza juu ya mzigo mkubwa wa umasikini ambao nao asili yake vile vile ni uongozi wao usio na vision.
Kama kiongozi anataka kuwa na wake 7 basi awe mkweli aoe hao wake 7 tujue moja. Lakini mchezo wa kutembea wanavua kaptula kila mtaa wanakaribisha Riwaya za kashfa za kujitakia hapa JF
Wewe rais mzima kwa nini ukatembee na mke wa mtu??
Kwa nini usijichagulie kidosho katika vidosho waliojaa tele katika kila kona ya Tanzania uka specialize kama yule mnyama Fungo anaye kunya sehemu moja tu maisha yake yote???!!
Haya tunajua uloda wa mkeo unausikia tu kwa vile ni miaka kibao tangu mpeane visogo. Kwa nini msipeane taraka kama rais wa Ufaransa na kuanza life na kimwana mpya ukatunyima sababu za kusema?
Mchezo wa kutembea na wake za watu, watoto wa shule na wafanyakazi wa chini yakoambao si wake zako kisheria na kiimani na mara nyingi kwa kutumia rungu tulilo kupa UFE.
Nasema UFE.
Sisi hapa JF hatujadiri maisha ya viongozi wenye wake wengi, tunajadiri maisha ya viongozi wanao tumia vibaya Vitumbua na kuni zao, kibay zaidi kwa gharama zetu walipa kodi.
Kiongozi akiwa na nyumba ndogo 3 akipeleka nyumba moja London kwenye shopping na nyingine zilizo baki zitadai kwenda, ili kujitoa kimaso maso Kiongozi huyo inabidi abebe gharama na kufadhiri shopping za vimada wake wote. Kwa vile mshahara wake na maluplupu hayana uwezo wa kukidhi gharama hiyo,ni wazi kwamba ataihamishia gharama hiyo kwetu wananchi matokeo yake ni haya ya kusaini mikataba ya ovyo na kupokea Rushwa kwenye kila jambo na kujenga tamaa nyingi za ajabu.
Hivi unajua kila tunapolipa ziada ya Bill za umeme Lowassa Rostamu na Timu yao nzima wanapata fedha za kunulia wake zao na vimada wao Poda za bei mbaya na hata Kukodi ndege kwenye ziara za kuendeleza ufisadi.
Sisi tukikung'aza kwenye Rada zetu tutauweka wazi udhaifu wako. Lengo la kuweka wazi aibu yako ni kuuonyesha umma asili ya tamaa yako na jinsi ambavyo kiongozi wewe ni bomu la machozi na mzigo kwa kila mwananchi. Mkeo au mumeo akijua udhaifu wako hiyo inakuwa ni by the way na si lengo la shughuli nzima ya kuanika maovu yako ya nguoni.
Uhuru ni Uhuru, Uhuru wa kuweka mipaka na mtu yeyote yule si uhuru ni utumwa.
Serikali ina sehemu nyingi sana za kutoa maagizo yake RTD na TvT magazeti na Mikutano ya hadhara. Binafsi sioni sababu wao kutumia member wa JF kutoa maoni yao yasiyokubalika na yenye kutaka sisi wana JF tuone simanzi.
Mke wa Malecela mama ANNA KILANGO kwa maneno yake mwenyewe alisema yuko tayari kwenda kinyume na mzee Malecela kama mzee huyo ataleta hoja utumbo ili kulinda maslahi ya walio mchagua na wananchi wote wa Tanzania.
Kifupi ni kwamba tutatoa siri ya kiongozi yeyote asiye muadilifu kwa staili yeyote tuitakayo bila kujali wadhifa na heshma yake.
Heshma ipi wakati kesha ipindisha?????!!!
Naamini serikali wana lengo zuri la kuhakikisha kuwa maadili mazuri yanafuatwa na Watanzania mahali popote walipo. Kama ujumbe huo ni wa kweli (na assume hivyo) basi ninaomba serikali yetu katika kutusaidia kutekeleza ujumbe wao huo.
a. Watangaze kwenye magazeti ya serikali, redioni, TV n.k kuwa matusi yamepigwa marufuku na Mtanzania yeyote awe chumbani kwake, kijiweni, sokoni, n.k haruhusiwi kusema neno lolote la matusi na watutangazie adhabu itakayowapata watakaokiuka.
b. Pia itakuwa vizuri watuwekee maneno ya matusi ambayo yanapigwa marufuku kusikika au kutumika pamoja na vitendo. Uhuru wa maneno ni mkubwa zaidi kuliko uhuru wa vitendo. Hivyo wakituorodheshea matusi na madaraja ya matusi (kama first class, second class, nk) tutajua ni maneno gani tunaweza kuyatumia. Hivyo watatusaidia kujua kama fuska, mjinga, mzembe, fisadi n.k ni matusi ya daraja gani?
c. Wakishatoa hiyo definition tunaomba waongeze maafisa usalama wa maadili (Moral Police) ili washinde mitaani na kwenye mtandao kutafuta nani amesema nini na kuchukua hatua mara moja.
d. Wakimaliza kwenye maneno ninawashauri waanze kuangalia mavazi ya Watanzania ili tujue watanzania wanatakiwa kuvaa nguo za namna gani kama alivyojaribu Bi. Hawa Ghasia. Kwa sababu baadhi ya nguo zinachochea mawazo ya matusi, naamini itakuwa vizuri kama serikali itatangaza nguo za namna gani zivaliwe na Watanzania. Nashauri vazi la kanzu, gagulo na kaniki yawe ni mavazi ya lazima kwa Watanzania!
e. Wakimaliza hayo ninawashauri waje na utaratibu wa kuhakikisha kuwa watu hawachukuliani mademu au wanaume. Hii itapunguza maneno mengi ya mtaani ambayo huchochea maneno ya matusi. Utaratibu huo unaweza kuhusisha teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ambapo kama Mbunge mmoja wa CCM alivyowahi kupendekeza wale wote wanaochukua wake/waume za watu wawekwe alama. Napendekeza wavae ribbon za aina fulani hivi. Za rangi ya zambarau ni nzuri zaidi.
f. Kwa vile maafisa wengi wa serikali na utumishi wa umma wanatumia muda mrefu kutumia email za matusi na picha za ngono (ushahidi upo) na vichekesho ambavyo wakati mwingine vinapakana na vya "kighaidi" napendekeza serikali iweke nembo kwenye compyuta zote za serikali ili wale wanaoependa kuangalia picha za ngono kompyuta zao zigome na waendelee na kazi.
g. Kwa vile ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni tatizo dogo nchini, napendekeza watawala wetu waendelee na kuhangaika na Jambo Forums na wapange vikao vya jinsi gani ya kuishughulikia huku wezi wa fedha za umma na wanaotumia mabaya madaraka yao wakiendelea kutanua. Kwa vile JF ndio tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi, napendekeza "task force" mpya iundwe na Waziri Mkuu (wanaweza kumuomba Mhe. Lowassa kwa ushauri wa jinsi ya kufanya hivyo) ili iweze kushughulia dharura hii ya Jambo Forums.
Wakishafanya hivyo, mimi nawaunga mkono kwa ushauri wao huo wa bure!!
Mkuu Sana Mzee ES
Naomba kabla ya kujibu, print haya majibu uwapelekee wakupe majibu ya hoja hizi. Mwanzo niliposoma nilielekea kukubaliana na wewe hila
naona hoja zimekuwa kali sana kinachotakiwa wapelekee print out ya majibu, uone kama kweli wameridhika.
Kama ndoa zao zinavunjika jamani si ni kutokana na matendo yao? kwani JF ndio wanavunja ndoa au wanawatuma mkafanye ufuska? Kama mtu ni mzizi tumuite nanai? kama mtu ni fisadi tumuite nani? na kama mtu ni muongo tumuite nani? Mwizi aitwe mwizi hakuna tofauti wa mwizi wa silaha na wa kalamu wote ni wezi tuu. Kijiko kiitwe kijiko na sepeto liitwe sepeto hicho ndicho kinachofanyika hapa JF.
Mimi kwa mtazamo wangu naona wataridhika na watafarijika na majibu yaliyotolewa, kwa kifupi JF hakuna matusi, na nifedhea kwa watu wazima kama Sisi kutwambia tunatoa matusi kinachoongelewa hapa ni kwa Uwazi na UKweli(hatufanyi UFISADI)
Nina point tatu.
Kwa hivyo basi, nakubali kwamba tuwe na standards hapa, lakini ziwe za kujipangia sisi wenyewe na sio kupangiwa na serikali.
- Si sawa kupangiwa na serikali cha kujadili.
- Si sawa hata hivyo kutumia matusi hapa. Si sawa vile vile kusema vitu kama ugonjwa wa mtu. Hata daktari haruhusiwi kusema ugonjwa wa mtu, sembuse wana JF?
- Si kweli kwamba freedom ni absolute. We are free to do good; but no one is free to do evil. It is an axiom in Philosophy that freedom is not absolute. Truth is absolute but freedom is not.
"Kama tukianza kuchafuana hapa,sidhani kama kuna Mwanasiasa yoyote atabaki" Edward Lowassa!