Wana-JF: Ujumbe Mzito Toka Serikali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana-JF: Ujumbe Mzito Toka Serikali!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Feb 25, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Ninawaomba ndugu zangu wote JF, mnipe nafasi nisilifanye hili kuwa siri bali ujumbe kwa ndugu zangu wote hapa JF. Katika siku mbili tatu zilizopita nimekuwa nikifanya utafiti wa kina ya yaliyojiri mpaka kuelekea kwenye yaliyotukuta karibuni, nimegundua mengi sana yanayotuhusu na yasiyotuhusu hapa JF, ninaomba niseme machache kati ya yanayotuhusu,

  Pamoja na ujumbe mwingi niliopewa na wakulu, leo nimepewa ujumbe mzito usiokuwa na mjadala, na nitaufikisha kwenu ndugu zangu kama nilivyopewa, kwamba tuache matusi ya nguoni, tujadili hoja na zijibiwe kwa hoja, matusi tuache, nimeambiwa ndoa za viongozi na hata wananchi wengine ziachwe maana tunagombanisha wakulu na wake zao na familia zao kwa ujumla, maneno ya magonjwa ya viongozi ambayo sio public right tuyaache, unless kama yamesemwa wazi na officially, au unless mtu ana clear evidence azimbatanishe na hoja yake, nimeambiwa kuwa tunakubalika sana na serikali tunapokuwa na hoja na wapo nasi hapa kila siku, lakini tunaharibu na matusi na hasa siku za karibuni, wanasema zamani tulikuwa makini, lakini recently tumetoka nje ya mstari sana na wamenipa evidence mbali mbali kutoka topic nyingi hapa, humbly as a man nimezikubali na kuomba radhi kwa niaba ya wote hapa JF.

  Sio nia yangu kujifanya wa maana sana kuliko wengine hapa, isipokuwa nimejitahidi kwa uwezo wangu kuombea kikombe cha damu kipite pembeni, na nimeahidi kwa niaba ya wote hapa JF, kuwa tutajitahidi kurudi tulikokuwa zamani, yaani kwenye hoja kwa hoja. Mkuu Invisible, please ndugu yangu na mods ninawaomba mnisikie ndugu zangu kuweni more serious na kufuta anything unlogical. Nimeamua kuyasema haya hadharani hapa hapa, ili kuondoa lawama mbele ya safari, na kuondoa usiri usiokuwa na maana kwenye hili. Na huu ujumbe unanihusu hata mimi pia, sio nyinyi ndugu zangu tu!

  Ndugu zangu sina maswali wala majibu kwenye hili, anayetaka anisikie, asiyetaka ndio demokrasia yenyewe, lakini I hope kuna watakao nisikia. Ndugu zangu tumuamini Mungu, lakini tufunge milango ya magari yetu na funguo.

  Field Marshall Es,

  JF Kumkoma Nyani Giladi, Mchana Kweupeeee, na Where We Dare To Talk it out Openly!
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu FMES

  Huu ndio tunauuita uungwana........wana JF inabidi tujitahidi wakati mwingine kuhimili emotions zetu

  Tuwape kudos ma-mods wetu wamekuwa wanajitahidi kuweka mambo sawa pale wanpokuwepo online na pale tunapowataarifu.....ofcourse under the guidance ya the mighty robot Invisible
   
 3. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu mzee es, hapa kidogo naomba kutofautiana.

  freedom ni all inclusive, ukianza kuweka mipaka what is allowed to be discussed and what is not, unarudi kule kule kwenye censorship.

  who cares watu wa serikali wanasema nini, wao waendelee kulimit hoja kwenye vyombo va serikali, but here we can discuss anything na kama ni pumba then viongozi hamna haja ya kujali.

  unasema serikali wanasema tufanye this and that, are u kidding me///
  is jf another idara a serikali au//


  mkuu es, waambie serikali wafanye kazi tunazolipia kwa kodi zetu, huku online wachukue wanavyopenda na wakiona kuna vitu havina mpango watuache kama tulivyo.

  who are they kupanga what is to be discussed//

  freedom is absolute no compromise on that.
  ukianza exceptions then unakuwa kwenye slippery slope.

  mimi binafsi sipendi kina mama na dada zangu wanapojadiliwa period, so mnaweza na mimi kunipa exception tukajadili wanaume tu///////

  give me a break
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ES

  I am deeply offended na huo ujumbe ulituletea hapa na nadhani kuwa wewe unazo akili tosha za kuwajibu kuwa watu hawajadili hawa watawala out of nothing.

  Hawa watu walikupa ujumbe ni wajinga,wala rushwa na mafisadi wakubwawasiokuwa na uchungu hata kidogo na Tanzania. Wako more interested private lives zao zisijadiliwe huku wananchi wakawaida wanazidi kuwa na hali mbaya
  [​IMG]
  BOT
  RICHMOND
  NGORONGORO
  BUZWAGI

  yote yametokea while they were there na hawakufanaya lolote zaidi ya SAMUEL SITTA kudai eti hawawezi kudiscuss sources za internet!!
  [​IMG]

  In short hatuna IMANI na watawala wetu na hatuwezi kuwaamini kwa lolote lile watakalo tuambia


  Wajibu kuwa nothing changes huku JF.

  As long as wao ni public figures an wanaishi kwa kodi za wananchi then maisha yao BOTH PUBLIC na PRIVATE ni haki za watu kujua
  [​IMG]

  Na mwisho zaidi waambie kuwa hawawezi kutuambia how to run our house. Na zaidi waambie kuwa kama wanataka tuwaelewe then waweke expenses zao ONLINE ili tuhjue kama ni wakweli au la


  waambie hao wapuuzi tunataka hawa watu waweze kuishi kama vile binadamu na sio kutufuatilia humu

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  Next time hebu tuspare bandwidh na umalizane nao hao jamaa huko huko. The least you could have done ni kuchangia simu alizokuwa akipiga Mwanakijiji. That dude ha sacrificed a lot PLUS his own safety ili tupate hii freedom halafu wewe unakuja kuleta ujumbe ambao ungeujibu huko huko

  ES nakuheshimu sana lakini kama unataka kuendelea kumaintain heshima yako mwambie Slava na hao watumwa wengine waje kujibu hizi hoja hapa


  Dude, how low can you go ? whats next.? utataka threads zao zifutwe kisa watu wanaquestion private lives za watawala wetu?
   
 5. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Very well said FM,na nnahisi licha ya Kukusikia WENGI Tumekuelewa.thankx4 Ur word of advice.
  **Ila Mkuu naona hata hiyo kauli Mbiu hapo juu itabidi ibadilike sasa!!
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  WTF is wrong with you man?

  Wale watoto wamespend 12 hours wanahojiwa utafikiri wanataka kupindua nchi halafu leo unakuja kuongea upuuzi huuu?

  Sikiliza bwana sisi JF ni family na mmoja wetu akikutwa na jambo ujue kuwa wote sisi tunaumia.

  So please shove it na huuu ujinga wa kutaka kucompromise na hao wapuuzi upeleke huko huko

  Kama wangekuwa wanafanya kazi yao basi zile pesa za EPA zingekuwa zishawalipa mafao yao hawa wazeee


  Emotions my ar$$$se!

  wanategemea nini baada ya kutudemonise? Obviously tutadevelop siege mentality na hiii ishakuwa doa

  wao wanayo website yao ya TAIFA wajibu mapigo basi kule


  [​IMG]
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  BRAZAMEN nimekupata mkuu
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu ES kishanichevua vibaya sana

  I was in a very good moood mpaka nikaona UJUMBE TOKA SERIKALINI

  kwani ES umekuwa SALVA RWEYEMAMU?

  serikali ina vyombo vingi tu vya kuwasilisha ujumbe kama vile

  WEBSITE YA IKULU


  WEBSITE YA HABARI NA UTANGAZAJI


  TUME YA MAWASILIANO


  WEBSITE YA TAIFA

  sasa who is ES mpaka apewe vijimessage kuleta kwenye internet forums?

  Kama wanataka kujibu hoja waje kutueleza kuhusu upuuzi wanaoendelea kuufanya kule ATC
  GATEI LA TAIFA
   
 9. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Nina point tatu.
  1. Si sawa kupangiwa na serikali cha kujadili.
  2. Si sawa hata hivyo kutumia matusi hapa. Si sawa vile vile kusema vitu kama ugonjwa wa mtu. Hata daktari haruhusiwi kusema ugonjwa wa mtu, sembuse wana JF?
  3. Si kweli kwamba freedom ni absolute. We are free to do good; but no one is free to do evil. It is an axiom in Philosophy that freedom is not absolute. Truth is absolute but freedom is not.
  Kwa hivyo basi, nakubali kwamba tuwe na standards hapa, lakini ziwe za kujipangia sisi wenyewe na sio kupangiwa na serikali.
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Can we get definition of matusi? Will Mijnga, Mzembe, Mvivu, Mbangaizaji, Msanii, Fuska, Mhujumu, Mbabaishaji qualify as matusi?

  Let them Serikali and Watendaji live a clean life and no word will come around. Have you heard any personal scandal about Pinda, Hussein Mwinyi, Mwandosya, Chiligati or Marmo? No!

  You will always here stories about same names and faces. A matter of fact, wote wanaotajwa sana ni waliotuleta hapa tulipo leo ambapo Serikali imekuwa Mangimeza na ni sisi Wananchi kutumia uhuru wa mawazo na maoni kuaanza kukata ishu na kujadili udhaifu wa viongozi wetu kutokana na maamuzi yao potofu ambayo yameruhusu hujuma na hata kukomaa kwa umasikini.

  Wewe ni mjumbe hivyo mabango si kwako, bali kwa Serikali na kwa kuwa wanasoma hapa, basi tunawaomba waanze kw kujisafisha kiutendaji na hata kitabiandipo watapata wafuasi na madongo yataacha kuwafikia.

  Ni ajabu sana, kiongozi mlafi, mwenye tamaa ya mali, mlevi au mzinzi ambaye katuletea mikataba mibovu au anahujumu uchumi kwa makusudi anaomba tuzungumzie Utendaji wake serikalini na si tabia zake?

  Chanzo chake cha levi au ufuska ni nini? kama yupo ndani ya ndoa halafu anateleza kupiga nje ya ndoa, jee ni mangapi katika kazi ambayo anayafanya kwa kuteleza ili kujipatia ziada?

  Integrity and morals have no boundaries. Being a public figure you are exposed to such scrutiny.

  Naomba uwaambie salamu tumezipokea, lakini hatutaacha kuwashikia bango mpaka kieleweke. Kama wanahofia ndoa, basi wajiulize kwa nini wanazini na kuwa na nyumba ndogo? kwa nini sisi kama Taifa na Jamii tujue kuwa wana nyumba Tandika, ilhali wake au waume zao wanaachwa Solemba!

  Hivo ni vitisho vya kitoto. Infact, for them to even dare to give us an ultimatum and censorship it means the war is wide open. I will say bring it on!
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  Hivi mnapo zungumzia STANDARDS mnataka standards zipi?

  we had standards before na hazijabadilika ni zile zile au mnaposema tuwe na standards mnataka nini cha zaidi?   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 13. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Ujumbe ni mzuri lakini ni lazima waelewe huu ni wakati tofauti duniani na huwezi kuzuia mawasiliano kwani itakuwa kuzuia maendeleo.

  Mfano kama mtu ana website yenye server USA utaizuiaje na ni website ngapi utazizuia? Hivyo huwezi kumonitor kila mtu kwenye website lakini vilevile siyo culture yetu kutukana.

  Kama atatokea mtu kutukana hatutahitaji wanaseriali watuambie kwani huyo Mtanzania mwenzetu atahitaji kuelimishwa ili asitukane tena na sisi wana JF. Hakuna mtu anayeshabikia matusi lakini kuna watu wana hasira sana kwenye hoja zao na wanatukana hivyo kitu kimoja cha kujua ni kwenye mtandao msichukue kila kitu personal.

  Kuna mtu anatukana leo na kuomba msamaha kesho kwasababu mawazo ya watu wengi ni ya hali aliyoyonayo wakati anaandika. Tanzania dunia imebadilika hivyo mfanye uamuzi je mnaipenda nchi na mnahita mawazo? Je mnathamini nchi kuliko aibu za rushwa na ufisaji? na je mnataka vizazi vijavyo viishije?.

  Kuzuia JF ni kuzuia maendeleo. Kama hawa jamaa wa JF wangekuwa na nia mbaya ni kwa nini basi wameweka anwani zao??
   
 14. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ndugu yangu pse don't misquote me out of context.

  u know very well the context hapa ni freedom of expression/speech online.
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Ujumbe ni PUMBA tupu I dont see uzui wowote wa humo.
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mzee ES na wadau wote,

  Ujumbe wako mzuri. Nikitazama upande mwingine wa shilingin nakutana na BRAZAMENI. Analeta ujumbe wa hasira na kuweka vielelezo vya PICHA. Ninaikubali ujumbe wake pia.

  Mimi ninachoomba ni kuwa tuna sheria zetu hapao JF. Naomba sote humu tuziheshimu. Nakumbuka ktk zile sheria hakuna inayoruhusu matusi.

  Tuheshimu sheria zetu na Serikali nayo iheshimu sheria zake (sio kukamata bila uchunguzi wa kina). Basi na sisi tutaheshimu sheria za serikali nao wataheshimu zetu.

  Ngoma droo tunaendelea.................
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......again nasema matusi sio zangu

  hao watoto wamespend 12hrs ulifanya juhudi gani kuwasaidia......msiwe mnakuja na matusi bila ya sababu.......we toa maoni yako tutaona kama yanaleta sense tutakuambia lakini sio kwa matusi
   
 18. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nikuunge mkono Mwl Moshi kwa yote matatu kimsingi, lakini natofautiana nawe kuwa hata "truth" sio "absolute" ndio maana mambo mengi bado yako debatable. Mambo mengi yanayochukuliwa kuwa "truth" ni makubaliano tu ya jumuiya fulani (wanataaluma, jamii, nk) kuwa yachukuliwe hivyo, na siku ushahidi tofauti ukipatikana kilichokuwa "truth" chaweza kubadilika kuwa sivyo tena (na hivyo wanakubaliana juu ya "ukweli mpya"). Mifano iko mingi. Kwa hili peke yake, si sawa hata kidogo kuzuia watu wasijadili jambo fulani, kwa sababu hata hiyo dhana tu ya kuwa mjadala huo uwepo au usiwepo ni debatable. Kwa mfano tunapozungumzia maisha binafsi ya kiongozi, tunamaanisha nini, na kwa mujibu wa nani? Kujadili afya ya kiongozi ni sawa au si sawa? Kimsingi hakuna mwenye jibu ambalo tunaweza kulichukulia kama "absolute truth" kuhusu swali hili, wengine watasema ni sawa na watatoa sababu, wengine watasema si sawa, na sababu watakuwa nazo, na zote zinajadilika. Kinachopaswa zijadiliwe zote, hoja "nyonge" itajifia yenyewe, na zile zenye nguvu zitabakia.

  Labda kama Field Marshal ES anataka kubadilisha slogan ya JF iwe kuwa "We no longer dare to talk openly!" lakini tukumbuke members wengi wako hapa kwa kuwa wanapata nafasi ya ku-ventilate. Jibu la kuwapa hao serikali ni sisi kuendelea kujadili hoja yoyote inayofika ukumbini humu, zile zenye udhaifu zitajifia zenyewe na zile zenye nguvu kimantiki zitadumu na kuleta impact kama ambavyo tayari imeshatokea huko serikalini na kwingineko zitakakogusa.
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  waungwana tusonge mbele, sheria zetu zipo na kwa sasa sioni kama zina mapungufu, cha msingi tuzifate na kuzisimamia vema sote mm na ww

  mawazo hayagombi yeyote ana haki kutoa mawazo yake wasitoke nje ya wigo tuliojiwekea
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Look man.Please do not question role yangu katika kuwasaidi wale vijana...I dont need to shout nilifanya nini lakini all i can tell you kila mmoja humu aliplay his part.So please do not PATRONIZE us

  inaonekana kuwa WATAWALA kutukanwa kuna kuuma sana kuliko wizi wanaofanya

  situation hapa ni mbaya na taratibu we were getting back to normality. Sasa the last thing we needed was someone giving us lectures jinsi gani ya kujiconduct humu ndani

  Kama uko offended then deal with it lakini I was more offended pale:

  WENZETU WAWILI KUKAMATWA

  KUTOPEWA ACCESS TO LEGAL AID

  KUHOJIWA KWA MASAA 14

  WEBSITE KUFUNGWA

  WATU KUINGIA GHARAMA ZA KUANZA KUWATAFUTA

  SERIKALI KUDAI KUWA JF NI CHOMBO CHA KIGAIDI

  THEN BAADA YA KUWATRAUMATISE WALE WATOTO FOR 14 HRS tukaambiwa kuwa Ohhh there was some misunderstanding!!!


  Kama kama siyo incompetence to the max ni nini hiyo?

  Imagine wale wangekuwa wadogo zako ungejisikia?

  Imagine wazazi wao wako kwenye pressure ya namna gani?

  Siamini kama upuuzi huu ulifanywa na Uslama wa Taifa ambao kama wangekuwa wanafanya kazi zao vizuri tusingekuwa na STICKY threads za UFISADI serikalini

  guess what?

  Few days afterwards ES anakuja kutupa lectures jinsi gani ya kujiconduct na what we shouldnt say

  Yes narudia tena watwala wetu ni worse than PIGS...haingii akilini wako sharp kuwakamata watu wanaotoa mawazo yao akini wako kimya kuhusu UFISADI kila sehemu huko serikalini
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...