Samahani wapendwa,Mimi siyo mwandishi mzuri Ila naomba mnielewe kwa chochote nitakacho kuwa nime andika.
Kuna mwanadada Nimekuwa na mahusiano naye toka mwezi wa kwanza,Naweza kusema mahusiano yetu yame anzia Facebook.
Huyu mdada mim sikuwahi kumtongoza kwa sababu alikuwa akimpost mwanaume ambae alionekana ni kama mchumba/mpenzi wake.
Mara nyingi nilikuwa nacomment na kumsifia huyu Dada kutokana na uzuri wake huku rohoni nikiumia kila ninapo ona akimpost yule jamaa wamekumbatiana wakiwa sehem nzuri nzuri za starehe.
Kutokana na pigo na mwonekano wa huyu mwanadada nilikuwa najisemea kimoyo moyo kuwa Mimi siyo type yake kabisa, Hasa ukilinganisha na maisha yangu yalivyo.
Ikumbukwe huyu Dada toka kipindi tuwe marafiki fb hakuna aliye wahi kumtafuta mwenzie inbox (messenger), Mawasiliano yetu yalikuwa yana ishia kwenye comment pale,Naweza kusema huyu Dada,Hakuna siku niliwahi comment kwenye post zake akaacha kureply,kitu ambacho nilikuwa navutiwa naye.
Nakumbuka Mwez 1 alipost picha akiwa na jamaa yake,Kutokana na walivyo kuwa wamependeza ilibidi tu nicomment Hivi *Daah aisee wakubwa wenye hela wana faidi*,Isivyo kawaida yake hiyo comment hakujibu,Nikaanza kuhisi ntakuwa nime mkera,Nikataka Nikaidelete ile comment ila nafsi ikagoma.
Kusema ukweli Nilishinda siko Sawa mana nilihisi atakuwa kakasirika sana,Siku hyo mida ya usiku nikiwa nimepumuzika nikapata wazo nikadelete ile comment,Kabla sijaenda kuifuta nikawa nimeona text imeingia messenger, kuchek hivi ni yule Dada,Haikupita Hata 2sec nikawa nimejibu ile text,Katika kuchatchat ndo akanambia kuwa hajapenda nilichocomment,Nika mwambia anisamehe,Akajibu usijari sisi binadamu wote ni Sawa,Pia haitoshi niko simple sana,
Nakumbuka siku ile tulichat mpaka saa 6 usiku,Akaniuliza nafanya kaz gan,Nikamjibu mishe ninazo fanya,Na yeye akanielezea vitu vyote vinavyo mhusu mpaka familia yao yote,Na akawa ame niambia kuwa ana mchumba (yule anae mpost) na harusi yao ni mwez wa 10 mwaka huu.
Licha ya kuchat naye usiku huo lakin sikumwomba namba ya simu mana nilikuwa nishajiona kwake ni kama mbingu na Aridhi,In short Kwa huyu demu nilijiona sina thaman mbele yake,Na kilicho kuwa kinaniboa zaid alikuwa ananiita mdogo wangu.
Ilibidi nimfanye kama rafiki tu basi.
Huyu Dada licha ya kuniambia kuwa ana mchumba wake Lakini alikuwa anapenda akiwa ana chat na Mimi Mara kwa Mara,Mara aingize masuala ya mapenzi Mara hivi,Ikumbukwe muda wote huo tuna chat tu fb.
Nakumbuka mwez wa pili mwaka huu ndo alinitumia namba yake ya simu,Alinambia amechoka kuchat fb so tuhamie offline,Nikamcheki tukawa tunachat sana,Mara aniite mpenz,nikawa nashangaa tu,Akiwa amelala ananitumia sms tukalale wote mana anahisi baridi.
Baada ya kuona huyu demu anazidi kuniletea za kuleta ikabidi siku moja nijitoe fahamu,Nilimwomba tufanye game ya kirafiki siku moja,Daah huwez amini hiyo text aliisoma lakin hakujibu chochote mpaka inafika nusu saa haikujibiwa,Nikazima data nikalala,Nilivyo amka asubuhi nikawasha data ili kucheki kama amejibu nikakuta holllaaa,Nikasema potelea mbali siwez chat na demu ambaye sijui mwisho wake,Nikaingia kwenye contact list nikadelete namba yake,Haiwezekan asome text alafu aache kunijibu,
Zilipita kama siku mbili hivi ndo nikaona text yake cz namba yake nilikuwa naijua tarakimu mbili za mwisho,Ikabidi na mim nimwonyeshe jeuri,Alituma kama text tano za kulalamika why namchunia ndo kidume nikajibu nilikuwa busy,Hapo hapo demu yeye mwenyew akaomba tukutane,Ikumbukwe muda wote huo mim na yeye tulikuwa hatujawahi kukutana zaid ya kutumiana picha na video call,
Mwezi wa 4 Demu aliniomba niende kwao singida,Nikamwambia labda tufanye mwez 5 coz kuna mishe flani nafanya mwez wote wa 4,Akakubali japo kinyonge,Hapa sasa naweza kusema tulikuwa ni kama wapenzi kabisa mpaka nakawa nahisi huyu Demu alinidang'anya yule siyo mchumba wake,Tulikuwa tunapigiana video call WhatsApp usiku akiwa uchi kabisa,Nikimwuliza,Hivi una mchumba Kweli? Ana kasirika,Ikabidi hayo ya yeye kuwa na mchumba nimwachie yeye, atajijua.
Bahati nzuri mwez 5 nikawa nimepata dili la kufata gari La mzee mmoja Dar, Ieleweke mim hii pia ndo kazi yangu kusafirisha magari,Dar to mwanza,Dar to Rwanda,Kongo,n,k,,Nafanya hyo kazi kama Niko likizo lakin,
Tarehe 2 mwez 5 mim na yeye huyu demu ndo tulikutana naye kwa Mara ya kwanza uso kwa macho nikiwa nimetoka Dar na Harrier ya watu[emoji3][emoji3][emoji3],hakuwa na utofaut na picha zake wala video call zake,Ilibidi anipeleke mpaka kwao,kusema ukweli wana maisha mazuri sana hasa ukilinganisha na fala mim,Pia ndo nikajua yeye ndo ana simamia biashara za mama yake hasa maduka ya vipodoz mawili na saloon pamoja na mgahawa mkubwa tu pale singida.
Baada ya kumaliza kusalimia Ikabidi nimwambie nataka kuendelea na safari yangu kurudi mwanza,Akasema huwez kwenda lazima ulale hapa,Daah kwa hyo nilale hapa na haitoshi kanitambulisha kama rafiki,,nikajisemea kimoyomoyo hapa natoka kapa,
Ilivyo fika mida ya saa moja kama na nusu demu akanambia twende ukapumuzike,nikamwuliza wapi,akasema wew twende tu,Ikabidi tuingie kwenye gari akawa ananielekeza njia ya kupita mpaka tukafika lodge moja,Nikapaki gari tukaingia mpaka mapokez then tukapewa funguo,Tumefika room sikutaka mambo mengi nilimvaa kama short ya umeme,Ikawa ndo Mara yetu ya kwanza kukutana kimwili (sex),Mida kama saa 6 Usiku akanambia nimpeleke nyumban kabla ya mama yake hajarud,Ilibidi nifanye hvo then mim nikanyoosha moja kwa moja mpaka mwanza.
Huyu demu naweza sema toka tuanze kukutana mwez wa 5 nimesha kutana naye zaid ya Mara 6 mana kila weekend lazima aje mwanza,Na kinacho nishangaza zaidi amekuwa ni mtu wa wivu sana,Juzi kuna demu kacomment kwangu fb kuwa amenimiss,kamtukana sana,Ikabidi nimwambie yule ni classmate wangu na saivi yuko pale UDSM ni dent,nikamwomba asifikirie vingine,tukawa tumeelewana vizuri,Chakushangza tena zaidi amekuwa akiniambia kuwa nisije kumuacha[emoji22][emoji22]
Mara ya kwanza nilikuwa nahisi hana mchumba labda ananiongopea tu, lakin huo ndo ukweli mwez wa 10 ni harusi na vikao vishaanza,Pia akimpost mchumba wake kule fb unakuta pia marafiki na ndugu wana comment kuwa wameisubiri harusi yao kwa hamu mwezi wa kumi.
Tangu mim na yeye tuanze mahusiano amewahi kunipost Mara mbili kwa kusema mim ni rafiki yake,Hyo mim siyo mbaya ila huwa nabaki njia panda anapo sema kuwa nisije kumsaliti na wakati anajua kabisa yeye ana olewa!!,,Na anasema lazima tuzae Mtoto,Ukimwuliza tutazaaje Mtoto na wakat una olewa,Ananuna na kubadirika kabisa.
Ikumbukwe Huyu Demu kamaliza UDOM mwaka juzi.
Nimeanza kuwa na wasi wasi na huyu Demu ndo mana nimeamua kuja kuomba ushauri huku.