Huyu jamaa hana makosa, amekiita Chuo cha Kata, lakini hata angekiita Chuo cha shina, bado si tatizo. Utendaji siku zote ndio unaotazamwa na kupimwa, si jina la Chuo. Ingekuwa hivyo basi Serikali isingepoteza muda kugharamia ule ujenzi. Labda afahamu kitu kimoja cha ajabu sana kuhusu UDOM. Katika College ya Medicine, Ipo Kituo ya Uchunguzi wa Afya (Diagnosis Centre) Ambacho kikikamilika, hakuna Mtanzania atakayekwenda India kutibiwa, mambo yote yataishia Pale, Kituo hicho hadi mwisho wa mwaka 2012/2013 ujenzi wake umekamilika kwa asilimia kama 35-40 hivi. Sasa kukiita Chuo cha kata mi nadhani amekipa hadhi ya chini bado, angekiita chuo cha shina kabisa kwa sababu huenda baada ya miaka 6-7 ijayo basi kikawa ndicho chuo cha msingi hapa Tanzania. Hii inafuatana na tetesi ambazo nimepata kuzisikia, ( Na huenda wana JF wengine pia wamepata kuzisikia) Kuwa kwa Hadhi ya UDSM, kwa sasa kuna mpango kiwe kinatoa Masterz na kuendelea, kusiwe na undergraduate pale UDSM, then vyuo vikuu vya serikali vitakavyokuwa na hadhi ni vingapi? Namsihi mtoa uzi, akisikia vijiumbea kama hivyo awe anajibu kwa hoja, anabungua bongo yake ndipo aje Jf!
Nawasilisha.