Wana JF kwa wale wanao-oa mke wa pili au tatu... unamwambiaje mkeo uliye naye.!!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF kwa wale wanao-oa mke wa pili au tatu... unamwambiaje mkeo uliye naye.!!??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jay One, Jan 8, 2011.

 1. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Huwa sipatagi jibu, hivi ukisha oa mke wa kwanza, then unataka kuoa mke wa pili, tatu
  4...... unamwambiaje mkeo uliyenaye? na mke wa kwanza si atakataa tu au wanalazimishwaga nini, maskini, mapenzi haya, utumwa kibao

  1. kwamba naoa ili uwe na familia kubwa? na una discuss naye
  2. naoa mke wa tatu, nne ili mfanye kazi pamoja ambayo najua haiwezekani
  3. au mwanaume anamwmabia naoa ili nisitoke nje ya ndoa
  4. Au dini inaruhusu, bila kujali mawazo ya mkeo uliyenaye
  5. au nimemwona mwanamke mzuri heri nioe tu, ila bado nakupenda mpenzi usijali
  6. au nina uwezo wa fedha unamwabia acha nioe mke mwingine ila ww ndiye mama
  mkubwa na ndio una mamlaka yote.... au, au, au....... UONGO KIBAO, tamaa tu unaficha.
  7. AU NI ZINAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA....tu mwanaume hataki kuwa wazi

  Nimemaliza, assist me plse, mm jibu namba 7 ambalo halisemwi ndio sahihi kwangu,
  period...
   
 2. s

  shosti JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kwanza huwa hawasemi,wengi wao ni wababe sana katika ndoa zao
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  :playball: Uko sahihi kuhusu namba saba na una majibu ambayo wengi wao husema...........ila umesahau kuna wanawake ni wagonjwa au wanamatatizo au wako busy sana kama wabunge na wanasiasa so wanaume pia hutumia hiyo sababu kuoa mke mwingine...............pia mila nyingine zinaruhusu kama wamasai etc etc
   
 4. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  thanks shosti, hata mm nadhani wanwaburuza tu mke aliye naye, kwani anajua tayari kazaa naye atakwenda wapi? yaani baasi no love
   
 5. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  MICHELLE, hi
  kwenye matatizo ya kuto kuzaa wapo kweli, ila ni wachache mno. ila wengi nafikiri wana waonea kwa mabavu ili waoe mke 2,3,4, kutimiza

  tamaa zao, ila watakwambia nimeongea na mke wangu kasema hamna shida, uongo tupu
   
 6. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I often wonder myself !
   
 7. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  unataka kuoa wangapi? je sababu gani?
  huwa kuna mengi kwa kila mtu
   
 8. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  walau tupe basi 1 au 2 za msingi, still i can't figure out, unasema nini hasa kumshawishi mkeo kumoa mwingine, kaaaaazi kweli, hapa
  ni UBABE unatumika i think.....maana kuna walio kama Paka na Mbwa wake zao ni maadui wakubwa, na ni wengi hawaelewani, sasa unaona inakuwaje kama walijadiliana?
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mimi na qualify kukujibu kwa sababu nna wake wawili na nnataka kuongeza watatu.

  Nimeoa Mke wa Kwanza miaka kadhaa iliyopita lakini Mwenyeezi Mungu hajatujaaalia kupata watoto na tukafanya njia zote zinazostahiki kujuwa ni nani mwenye matatizo, kwa bahati mbaya (au nzuri) ikakutikana ni mke wangu, kipenzi cha roho yangu, tuliyeanza nae maisha ndie mwenye matatizo yaliyoshindikana kutibika. Nakumbuka, ni Doctor Andrew ndie alietufanyia uchunguzi mara ya mwisho baada ya kuhangaika sana (miaka 15), yeye ndie alikuwa shupavu na kusema kuwa, "mama, wewe ndie mwenye matatizo", una fibroids za muda mrefu ambazo zimezuwia njia za uzazi na dawa ni kuzitowa la sivyo zinaweza kuleta matatizo zaidi ya kiafya, na katika kutowa kwake, jinsi zilivyokaa, tutajitahidi lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa hutoweza kubeba mimba tena. Tukajishauri na tukaamuwa kuyatoa hayo ma-fibrosis.

  Baada ya hapo, na miaka mitatu baadae, tukashauriana sana na kipenzi mke wangu naye akaniambia, "mume wangu naomba kaoe kwa sharti moja tu". Ukipata mtoto unipe mimi nimlee.

  Baada ya hapo ikanichukuwa tena miaka miwili kabla sijaoa mke wa pili. Nikaoa na Mwenyeezi mungu akatujaalia kupata mtoto wa kwanza, kama tulivyokubaliana, nikampa Mke wangu wa Kwanza amlee, na mpaka sasa tuna watoto wanne na huyu mke wa pili, na watoto wote wanalelewa jointly. Mpaka inafikia hawajui mama yao mzazi ni nani.

  Mwenyeezi Mungu katujaalia hivyo, baada ya muda kupita, na kushauriana sana na wake zangu, tumekubaliana, ikibidi niowe mke wa tatu wao wako tayari kwa hilo. Kwa sababu zisizo zuilika kwa sasa.

  Inabidi niyaweke haya wazi uelewe kuwa, kila aongezae mke ana sababu zake na si vizuri kuzitangaza.

  Kuoa kihalali zaidi ya mke mmoja si zinaa. Zinaa ni kwenda kinyume na kuingiliana na mke/mume wa mtu ambae hamjaoana.

  Jee, bora uongeze mke wa halali au ufanye zinaa? Kama Daktari wetu maarufu wa kanoni?
   
 10. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  kama kijeba kinakula mzigo daily ....kabla hakijaenda kazini anapiga,mchana anaomba ruksa kazini kuja kula anamwita wife anachakachua,akirudi kazin jion anakuli tundi,usiku kabla y kulala anashtua tena anambabatov(vi3) .....mwanamke hapo lazima akufuate mwenye akwambie anahitaji msaidiz ....eeee! msaidizi unafikiri nn
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mgonjwa huyoo si mzima na wala si sifa,awe anashinda na kulala na njaa ili asiwe na nguvu.
   
 12. s

  shosti JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Uadilifu upo lakini au ziro
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hi Mr President,
  Unajua kuna namna wanaume wamepewa ubinafsi na hawana roho za kuugua na yale mabaya wanayofanya kama kudanganya wanawake,mi nilishadanganywa na mume wa mtu kuwa anataka kumuacha mke wake kwa kuwa ana kansa ya kizazi,kwa hiyo alitaka anioe mimi kimila........instinct zangu zikaniambia huu ni uongo nikampotezea kimoja,siku moja niko hospitali namuona huyo na mkewe mjamzito na kumbe ni mdada tumesoma nae na tukakumbatiana kwa furaha na yule dada as hatukuwa tumeonana siku nyingi...........alipoingia kwa Dr nilimuomba tuongee nje,nikampiga kibao na kumwagia maji..................ndipo nilipojua mwanaume akitaka uchi wako hashindwi kukuambia ametoka kumzika mkewe juzi......ni waongo mno,so mi sishangai kusikia akija na uongo wake,ntakachofanya ni kuangalia kama nakubaliana nae au lah,siwezi naachia ngazi namuachia aoe mke mwingine,maisha yataendelea tu bila yeye.
   
 14. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Katika mazingira yafuatayo mke wa 2 au wa 3 haepukiki. Mke akizidiwa na ligwaride, lazima atakubali uoe mwingine. Akizidiwa na majukumu ya kiuchumi, akiwa na afya yenye mgogoro. Kwa wale ambao sheria za dini zinatuzuia kuongeza mke, tunashauriwa kutumia sheria za makabila katika kufikia maamuzi na nadhani hakuna kabila linalokataza labda wanaofuata MATLINIA SYSTEM but am not sure.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tofauti na udhaniavyo na nnadhani kuna kina Dada au Mama humu watanisaidia. Si mara ngapi kwa siku unafanya! ni vipi una-fanya.
   
 16. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mi kwanza ningeuliza,wat if mwanaume ndo ana matatizo?would you bare seeing your wife na mtu mwngne,in your house?.secondly,i have seen a difference btn wazungu na waafrika,wen it comes to kids,mzungu anaeza hata kuadopt..and embu fikiria m2 ana matatizo and unamuongezea heartaches being with anthr woman infront of her,bora umuache!there are many women smiling but dying in their hearts bkoz of ths,na that vow ya in cknes and in health,where does it go?.Men preach about being patient but most cant,ni mwanamke tu ndo anatakiwa avumilie everythng,ukiumwa,ukiwa broke,.na wanawake wengne juu..bora mbreak kwakweli,Mungu pekee ndo mwenye njia..nt human.
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kumbuka, uadilifu una uigo mpana kuliko unavyoufikiria. Mpaka uwe ndani ndio utapojuwa upo au haupo. Kinachotakiwa ni kuwa na nia njema na kujitahidi kadri uwezavyo. Mengine Unamuachia Judge wa Ma-Judge.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  No its not the way you think! Uzuri wa uIslam, ikifikia kuwa mwanamme hatimizi kindoa, kimaisha na mahitaji ya kila siku, na ikiwa ana matatizo ya kiafya, basi mwanamke ana haki ya kumuacha mwanamme.

  Kwa hiyo, kama mwanamme ndio ana matatizo, ni simply mwanamke anatowa talaka! Huo mama ndio uIslam. Haki.
   
 19. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kuna matatizo machache mno, ila most of time ni ZINAAAAAAAA, ngono as Mr President ulivyosema, ni tamaaaaaaa, ngonoooooooo
  hamna mapenzi ng'oooooo, mke wa 2 au 3...... ni uzinzi tu hamna lolote, hakuna mwanamke anayekubali mumewe aoe kama kuku
   
 20. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Mhhh wakati mwingine kuna mambo yanashangaza sana,

  Umeoa wa pili baada ya kuona mkeo hazai- Je kama wewe ungekuwa huna uwezo wa kuzaa, ungemruhusu mkeo azae na mtu mwingine?

  Haya umesema umeoa baada ya 15 years kukaa na huyo wa kwanza, na ukajaliwa kupata watoto 4, that means kama kwa wastani ulioa ukiwa na miaka 28-30 hadi unaoa mke wa pili ulikuwa kati ya (28+15=43) au (30+15=45) , haya ukazaa na mke wa pili watoto 4 , tuasume mke wa pili alikuwa anazaa kila mwaka i.e. 43+4 au 45+4 hivyo ulikuwa 47 au 49, haya mara tena ukashauriana sana na wake zako hao wawili kuongeza watatu that means uliingia kwenye ndoa ya tatu ukiwa na takribani miaka 50.

  Binafsi haiingii akilini katika mipango ya kawaida ya familia, tayari una mke, umekiri sababu ya kuongeza ni watoto haya wa pili kazaa watoto 4, haya una miaka 50 tena unataka mapenzi mapya , huoni kuanzisha familia ingine ukiwa na miaka 50 ni kujipa tu presha na watoto kukuita babu.

  Kwa maoni yangu naona kila binadamu (ikiwa mwanamke) ameumbwa na hisia , akubalike, apendwe pamoja na mapungufu yake ya kimaumbile. Nadharia ya ndoa kiafrika bado ni ngumu sana, watu wanaingia kwenye ndoa ili kuwafurahisha wengine (wazazi, ukoo, jamii) na hawajakubaliana kwa udhati wao wawili ni nini hasa maana ya wao kuwa kwenye ndoa), je ni watoto ndio wanakamilisha ndoa? ni furaha ya wawili au ni nini? pale tu wapenzi wanapojua maana ya ndoa kati yao basi pamoja na mapungufu ya kimaumbile ambayo mwenyezi Mungu anaweza akampa yoyote basi watu wataendelea kuishi kwa mapenzi na kuvumiliana.

  Dhana ya kusema nilimwomba mke wangu / wake zangu wakakubali siafiki nalo kwa mawazo yangu. Ni binadamu gani anapenda apunguziwe upendo? ni nani hapendi kuthaminiwa, kuonekana muhimu ? Napata wakati mgumu sana kukubaliana na dhana ya mwanaume kuwa na wake wengi licha ya imani kuruhusu. Maana ni lazima utampenda mmoja zaidi na kumsononesha mwingine.
   
Loading...