Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,972
- 22,933
Kuwa na mchepuko ni siri chafu ya mwanamume aliyeko katika ndoa ya - siri hiyo huenda sambamba kwa mwanaume kumdanganya mke wa ndoa kuwa anampenda yeye tu! Akiingia mtaa wa pili ana mchepuko, huko hufanya uzinzi kwa kwenda mbele.
Mchepuko sio mkeo wa pili.
Katika tamaduni ambazo mitala inatekelezwa, kuoa wake 2, 3, 4,…,nk huwa si siri – wanafamilia wote wanafahamiana na kukubaliana – licha ya ushindani baina yao kati ya nyumba na nyumba hakika huwa wanatambuana na kuheshimiana.
Binafsi sitetei ndoa ya wake wengi bali ninatetea sana ndoa ya Mume Mmoja, Mke Mmoja.
Tangu awali mpango wa Mungu kwa wanadamu kuhusu ndoa ulikuwa Mwanamume Mmoja, Mwanamke Mmoja.
Yesu alisema ".. na hao WAWILI watakuwa mwili mmoja"
Mathayo 19:5.
Maana yake hawatakuwa 3, 4, 5,…, waje kuwa mwili mmoja.
Pamoja na hayo ulimwengu huu umevunjika na uko mbali na mapenzi kamili ya Mungu. maana Mungu aliruhusu mitala kinyume na mapenzi yake kamili. Napenda kumtumia Yakobo kama mfano - Wana 12 wa Yakobo - walizaliwa kutoka kwa wanawake 4 tofauti - wakawa mababa wa makabila 12 yaliyobarikiwa ya Israel - waliobarikiwa kutokana na mitala!
Katika 1 Mambo ya Nyakati 3:1-9, Biblia inaorodhesha wake 7 wa Mfalme Daudi - Ahinoamu, Abigaili, Maaka, Hagithi, Abitali, Egla na Bath-sheba. Na Daudi alikuwa na wanawake wengine ambao majina yao hayakutajwa katika Biblia. Hata hivyo, Mungu hakuwahi kumhukumu Daudi kwa mitala - Mungu alimhukumu tu Daudi kwa kuchukua Bathsheba mke wa Uria.
Naamini kuoa wake wengi ni katika MAPENZI YA RUHUSA ya Mungu lakini SIO katika MAPENZI KAMILI ya Mungu.
Katika Agano Jipya, Paulo aliwataka maaskofu kuoa mke mmoja tu ili kutoa mfano wa muungano kati ya Kristo (Bwana harusi) na Kanisa (Bibi-arusi).
1 Timotheo 3:2 - Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja.
Sababu ya Paulo kutoweka hitaji hili la mke mmoja katika kanisa la kwanza ni kwa sababu na ndugu wengi ambao walikuwa na wake wengi. Aliongeza neema, sio hukumu.
Ni heri ubaki na mke mmoja pasipo mchepuko, au uongeze mke wa pili na sio kuzini na huyo mchepuko wako.
Mchepuko sio mke wako wa pili.
Ubarikiwe.