Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,221
Mimi ni mwana CCM, kwanza nakubaliana na mama Samia kuwa tuwe na subra juu ya Katiba Mpya. Lakini mbadiliko ya Katiba ni lazima yatokee kuziba mapungufu makubwa tuliyoyaona Awamu ya Tano.
Mifano ya mambo tuliyaona yakikiukwa wazi wazi Awamu ya Tano:
1. Rais Lazima awajibike kwa Wananchi kupitia Bunge.
2. Mihimili yote, Serikali, Bunge na Mahakama isiingiliwe kiutendaji na mhimili mwingine, na iwe kosa la jinai kufanya hivyo.
3. Serikali lazima ichukuliwe hatua kama CAG aikiona mapungufu makubwa katika matumizi yasiyoidhinishwa(kumbuka 1.5Trilloin).
4. Kiongozi atakayekiuka Haki za Binadamu lazima awajibishwe.
5. Ukomo wa Rais kutoshitakiwa uwe wakati akiwa madarakani tu(Trump leo anashitakiwa kwa kukwepa kodi).
6. Serikali isiingiie Mihimili mingine( mfano Rais kumfukuza kazi CAG baada ya kugundua matumizi yasiyoidhinishwa na Bunge ya 1.5 tril).
7. Kuingilia mchakato wa uchaguzi iwe kosa la jinai kwa kiongozi yeyote-hata wana CCM wanajua kuwa uchaguzi wa 2020 haukuwa uchaguzi halali bali kiongozi kawachagua awapendao kuingia Bunge. Aibu ya wabunge wa chama upinzani 19, ni tusi kwa demokrasia.
8. Uhuru wa kuongea, na kutoa maoni, mradi mtu havunji sheria(Makamba na Kinana walichukuliwa hatua kwa kudukuliwa na kuongea ya kwao ya moyoni).
9...
10...
11...
Haya wana CCM, bado tunakumbuka yaliyompata mzee Mangula. Nchi ingekuwa ya kuwajibika na mihimili imekaa sawa kwa katiba yenye uwezo na nguvu, waliompa sumu wangekuwa wamesha wajibishwa.
Lazima pawepo REAL CHECKS AND BALANCE katika execution ya duties zote za kiserikali.