MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,268
Hata kama.....Nyinyi kama chama tawala hampaswi kutumia nguvu kubwa kwenye majukwaa ya kisiasa baddala yake mnapaswa kutimiza ahadi mlizotoa na si vinginevyo.
Pamoja na kwamba mmeweka huo mkakati sijui operesheni lakini kama hamjatimiza ahadi mlizotoa ama wananchi hawajaona lolote la maendeleo tangu walipowapa madaraka, huo mkakati wenu hautafanikiwa na huyo mnayetaka kumchakaza ataendelea kung'ara na kupendwa.
MKAKATI WENU NI SAWA NA KUZIBA TUNDU LA PANYA KWA MKATE, mmechelewa!
Iramba political problem SOLVED.
Tunatumia majukwaa kufuta uongo unaotumiwa na viongozi wa upinzani kuwalaghai wananchi wasiojua kile kinachoendelea kisiasa. Tumefanya hivyo Iramba na Matokeo yake yako kwenye ofisi za tume ya uchaguzi kwa sasa.
Huwezi kutuchagulia njia na jinsi ya kufanya siasa wakati tuko tangu 1977 kwenye ulingo wa siasa. Tunafahamu kile tunachokifanya.