Hatimaye matokeo kamili ya uchaguzi wa vijiji na vitongoji uliofanyika wilayani Iramba yametangazwa.
Katika uchaguzi huo CHADEMA kwa mara ya kwanza ndiyo kimesimamisha wagombea karibia katika nafasi zote.
Matokeo rasmi yanaonyesha kwamba CHADEMA kwa mara ya kwanza kimeweza kupata vitongoji 2 na wajumbe wa Halmashauri za vijiji 40.Ikumbukwe kabla ya uchaguzi huu vitongoji vyote na wajumbe wote wa halmashauri za vijiji walikuwa CCM.
Pamoja na kwamba CCM iliweza kurejesha viti vya uenyekiti 8 bado wenyeviti hao wataongoza vijiji hivyo kwa mchanganyiko wa wajumbe wa CCM na CHADEMA ambapo kabla ya hapo hakukuwa na mjumbe hata mmoja wa CHADEMA.
Matokeo haya ya CHADEMA yamechangiwa na kazi kubwa iliyofanywa na Kiongozi wa kampeni Kamanda Ally Bananga.