Siyo siri
Katika miaka ya hivi karibuni CCM imekuwa weak kutokana na kukosekana itikadi na taratibu zinazojenga mshikamano ndani ya chama.
Na Said Kubenea
JAKAYA Mrisho Kikwete, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, anapaswa kushitakiwa kwa uchochezi.
Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake mjini Dodoma leo, Kikwete alichochea wanachama wa CCM kuwapiga wapinzani kwa kudai kuwa, Uvumilivu una kikomo.
Amewataka wana CCM kuacha unyonge kwa madai kwamba wapinzani wamekuwa wakiwapiga huku wao wakisubiri polisi kuchukua hatua za kisheria.
Hii ina maana kwamba, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewataka wanachama wa CCM, kuchukua sheria mkononi. Ametaka wananchi kuumizana, kupingana na kuuana. Huu ni uchochezi unaoweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa, kidini na kijamii.
Kama Kikwete alitaka urais, bila shaka alijipima na kujiona anaweza kufanya kazi hiyo. Kama alikuwa anajua anakwenda Ikulu kujaribu, basi alikuwa amekosea. Ikulu siyo sehemu ya kujaribu.
Kauli ya Kikwete ya kutaka wananchi wajibu mapigo, ni ishara kwamba ameomba kazi ambayo haiwezi.
Rais wa nchi hawezi kuchochea raia wake kupigana. Anapaswa kutumia vyombo alivyonavyo kusimamia sheria.
Ni lazima akumbushwe kwamba nchi hii ikiingia katika machafuko au mauaji ya halaiki, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuulizwa. Anaweza asiulizwe na vyombo vya sheria vya hapa, lakini ataulizwa na vyombo vingine vya dunia.
sijaielewa hii kauli ya kikwete alikuwa anamaanisha nini.
ameyasema hayo wakati wa kikao cha NEC alipokuwa anazungumzia machafuko yanayotokea kwenye chaguzi ndogo especially ile ya kahama.
amewataka wana CCM kuacha unyonge. hapa nimeshindwa kumuelewa; anataka wana CCM wareact vipi? kwa kuua au?
na amejihami kwa kusema kwamba hata kama alichokisema kitakuwa ndio habari nzito kwenye vyombo ya habari sawa tu.
source: news, TBC1
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?
Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?
Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?
JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.
Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.
Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.
Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?
Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.
Acha uchochezi we Kubenea. Unadhalilisha taaluma ya uandishi wa habari maana siku zote habari zako zimejaa majungu tupu. Umeshindwa kuuona uchochezi unaofanywa na akina Slaa, Mbowe na Msigwa kwenye majukwaa kila siku, umeiona kauli ya Kikwete tu. Laanakum sheitwan mk...ubwa wee!
Mbona hukusema haya wakati wana CCM wamechomewa nyumba, wamekatwa mikono na kutolewa macho huko kahama?
Mbona hukuwashitaki Mbowe na Slaa wanaotembea kwa chopper kushinikiza ngumi na mapanga kila siku?
Mchochezi ni nani? Umemwelewa JK we Kubenea au ni muendelezo wa majungu yako ya kukosa kuteuliwa nae tangu 2005?
JK hakumaanisha mapanga wala ngumi, na kama unapenda haki dhidi ya wachochezi basi faili la kwanza Mahakamani washitakiwe Mbowe na Slaa pamoja na wabunge wao kwa uchochezi na utekelezaji wa mauaji.
Nenda Bugando Mwanza ukawaone majeruhi ndo uje uandike makala yenye haki.
Kubenea unajiaabisha.
Hata wao chadema watakushangaa kama unasimama kuwatetea.
Ushahidi wa mwanzo ni namna wananchi walivyoamua kuwakataa kupitia kura na kuambulia kata 3, je unadhani hiyo ni kawaida?
Kubenea vua miwani ya ushabiki uitendee haki kalamu yako.
Amechoka na amani ana taka kujaribu kwanza ya Rwanda na Burundi.
Alicho sema sawa tu.
Kama vyama vingine vina fanya uhuni na ugaidi ili kuwatusha watu wasipige kura njia nzuri ni kujibu mapigo kwa kuwalinda wakapige kura.
Wakizongea vituo vya kuisabia kura nao ccm wazongee
Fujo za uchaguzi za wengine jawabu ni jino kwa jino