Wamiliki wa magari wazidi kuumizwa

Wamiliki wa magari wazidi kuumizwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,396
Reaction score
867,044
Kama kuna sehemu imelemewa na kodi mbalimbali za serikali basi ni kwenye chombo cha usafiri,
Baada ya kutubana kwenye road license, fire extinguisher, petrol na diesel, vipuri na lubricants nk nk leseni za udereva, kulipia ukaguzi, ongezeko la import duty, nk nk sasa maumivu safari hii yameletwa kwenye bima

Kwanza bima ilipandishwa kutoka elfu 50 third party mpaka laki moja, na comprehensive nazo zikapanda kwa kiwango vyake, wamiliki tulalalamika kidogo lakini tukaridhia.

Sasa limeletwa la VAT kwenye hizo bima, sasa hivi ukinunua bima ya kiwango chochote nk shurti ulipie na ongezeko la thamani 18%, huku ni kuzidi kunyonga na kuwaumiza wananchi kwakweli.

Tunaelekea ni kurudi kwenye enzi ileile ya kumiliki gari inakuwa kama kitu cha kifahari na gharama kubwa, ukija kujumlisha utitiri wa malipo unayofanya kwa gari dogo tu la milioni 8, ni gharama ambayo kwa maisha ya mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu na akifanya hivyo anaumiza bajeti kwenye mambo mengine ya muhimu.

Serikali hii na watoa maamuzi wake sijui wanaishi dunia gani kushindwa kuyaona haya.....
 
Unahisipesa za escrow watazirudishaje..
 
……kuna mpya ambayo sijaiona kokote , ,eti uki purchase kitu supemarket inabidi ulipie na mfuko utakao fungiwa ulichonunua , wote sasa tutahamia dukani kwa mangi ukinunua chumvi ya shilingi mia tano anakuwekea kwenye mfuko bila ya kukuomba mia ya mfuko
 
Kwani zimepanda tena?

Hiyo laki 1 kwa third party mbona ilikuwepo tojea julai mwaka jana...
 
Kwani zimepanda tena?

Hiyo laki 1 kwa third party mbona ilikuwepo tojea julai mwaka jana...

Hiyo sasa unatakiwa uongezee na VAT 18%, mwaka jana haikuwa na VAT
 
Kama kuna sehemu imelemewa na kodi mbalimbali za serikali basi ni kwenye chombo cha usafiri,
Baada ya kutubana kwenye road license, fire extinguisher, petrol na diesel, vipuri na lubricants nk nk leseni za udereva, kulipia ukaguzi, ongezeko la import duty, nk nk sasa maumivu safari hii yameletwa kwenye bima

Kwanza bima ilipandishwa kutoka elfu 50 third party mpaka laki moja, na comprehensive nazo zikapanda kwa kiwango vyake, wamiliki tulalalamika kidogo lakini tukaridhia
Sasa limeletwa la VAT kwenye hizo bima, sasa hivi ukinunua bima ya kiwango chochote nk shurti ulipie na ongezeko la thamani 18%, huku ni kuzidi kunyonga na kuwaumiza wananchi kwakweli
Tunaelekea ni kurudi kwenye enzi ileile ya kumiliki gari inakuwa kama kitu cha kifahari na gharama kubwa, ukija kujumlisha utitiri wa malipo unayofanya kwa gari dogo tu la milioni 8, ni gharama ambayo kwa maisha ya mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu na akifanya hivyo anaumiza bajeti kwenye mambo mengine ya muhimu
Serikali hii na watoa maamuzi wake sijui wanaishi dunia gani kushindwa kuyaona haya.....

Jipe moyo kaka.
Mungu huyo huyo aliyekupa nguvu ukanunua gari ndo huyo huyo atakuwezesha kulimiliki na kulitunza.
Piga moyo konde wakati tuna Uninstall CCM na kuINSTALL UKAWA Magogoni.
 
……kuna mpya ambayo sijaiona kokote , ,eti uki purchase kitu supemarket inabidi ulipie na mfuko utakao fungiwa ulichonunua , wote sasa tutahamia dukani kwa mangi ukinunua chumvi ya shilingi mia tano anakuwekea kwenye mfuko bila ya kukuomba mia ya mfuko
Ukisoma Merchantile Law/Law of Contract hii ni-kinyume cha sheria za mauzo na manunuzi. Kwa mujibu wa sheria muuzaji anatakiwa akufungashie au akupe mfuko au kibebeo kwa kila bidhaa utakayonunua kwa gharama yake
 
Mmhh!!!

Hivi bima nayo hulipiwa VAT?
Kiukweli huu ni unyonyaji. Yaani mwaka huu wananchi tutagharamikia kampeni mpaka tukome. Ile bajeti ya trillion 22 wengi walifikiri ni kwa manufaa yetu ila kuikweli havi such a big budget inamaanisha a lot is to be drained from the tax payers. Sasa na ukinunua umeme wa LUKU kuna makato yameongezwa, sijui ni VAT pia?
 
do you agree to uninstall..................ccm? yeeeeeees
 
Umejiandikisha?tuing'oe ccm ndio dawa.saa ya ukombozi ni sasa.
 
Mshana mbona bima yangu inayoisha mwezi ujao nililipa laki,hiyo ya 50 ilikuwa ya chombo gani
 
Serikali iliyopandisha bei ya mafuta ya taa ili mtu mmoja asichakachue diesel.

Okutoba 25 Fanya hisani kwa nchi yako
 
Back
Top Bottom