Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,876
- 29,057
Tanzania ni nchi ya maziwa na asali yasiyo ya nyuki wala ng'ombe
Nadhan tulipofikia sasa,kumng'oa huyu mdudu CCM si kwa kura,kuna namna wanataka iwe maana wengi hatuna kitu,wachache wanaishi duniani.
Kama kuna sehemu imelemewa na kodi mbalimbali za serikali basi ni kwenye chombo cha usafiri,
Baada ya kutubana kwenye road license, fire extinguisher, petrol na diesel, vipuri na lubricants nk nk leseni za udereva, kulipia ukaguzi, ongezeko la import duty, nk nk sasa maumivu safari hii yameletwa kwenye bima
Kwanza bima ilipandishwa kutoka elfu 50 third party mpaka laki moja, na comprehensive nazo zikapanda kwa kiwango vyake, wamiliki tulalalamika kidogo lakini tukaridhia.
Sasa limeletwa la VAT kwenye hizo bima, sasa hivi ukinunua bima ya kiwango chochote nk shurti ulipie na ongezeko la thamani 18%, huku ni kuzidi kunyonga na kuwaumiza wananchi kwakweli.
Tunaelekea ni kurudi kwenye enzi ileile ya kumiliki gari inakuwa kama kitu cha kifahari na gharama kubwa, ukija kujumlisha utitiri wa malipo unayofanya kwa gari dogo tu la milioni 8, ni gharama ambayo kwa maisha ya mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu na akifanya hivyo anaumiza bajeti kwenye mambo mengine ya muhimu.
Serikali hii na watoa maamuzi wake sijui wanaishi dunia gani kushindwa kuyaona haya.....
october ifike tu aisee
Ni rahisi kuliangalia kwa mtazamo huu lakini comprehensive sio magari binafsi tu bali ni magari yote yakiwemo ya mizigo na abiria
Kila senti inayoongezeka kwenye chombo chochote kinachoitwa gari maumivu ya mwisho huja kwa mwananchi wa kawaida, kulipa kodi ni ada lakini je tunaangalia ni maeneo gani yanapaswa kubanwa na maeneo gani yanapaswa kupewa unafuu?
Makampuni ya simu na migodi, mahoteli na uwekezaji mkubwa maliasili na utalii huko kuna kodi nyingi sana zinaachwa au kusamehewa wakati ni watu wenye uwezo wa kuzilipa halafu anakuja kuumizwa mntu wa chini na bado tunatetea...!!???kweli!?
kuna mpya ambayo sijaiona kokote , ,eti uki purchase kitu supemarket inabidi ulipie na mfuko utakao fungiwa ulichonunua , wote sasa tutahamia dukani kwa mangi ukinunua chumvi ya shilingi mia tano anakuwekea kwenye mfuko bila ya kukuomba mia ya mfuko
kujenga uchumi ni mbinu na lengo ni kupunguza fedha zinazotoka kupitia inports hasa katika vitu visivyo vya msingi au katika vitu ambavyo watu wanaweza kupata kwa gharama nafuu.
tuna tatizo la taifa kutokuwa na wachumi sababu za taifa kutokuwa na wachumi waliokuwa dedicated kudirect uchumi wa taifa sote tunajua .
lakini kama wangekuwa makini wangetambua kuwa kuwa na basi zuri linasafirisha watu 60 kutoka gongo la mboto mpaka posta taifa linakuwa linafanya vizuri kiuchumi kuliko kuwa na magari ya binafsi kama 40 barabarani yakiwasafirisha hawa watu.
kama taifa mnatengeneza mifumo ya kuwezesha watu wasafiri kwa kutumia usafiri wa umma na kuondokana na usafiri binafsi. jiulize basi moja kubwa linanunuliwa kwa shilingi ngapi? kwa mwaka linatumia spea shilingi ngapi na mafuta kwa mwaka linakula kiasi gani. alafu angalia magari hayo 40 yamenunuliwa kwa shilingi ngapi? spea na mafuta yote arobanini kwa pamoja kwa mwaka yanatumia kiasi gani na hapa kinachotafutwa ni usafiri wa kutoka gongo la mboto kwenda posta sasa jiulize ni njia ipi taifa linafilisika kwa kitu kilele yaani watu 60 kutoka g/mboto kwenda posta.
kutokuwa na wachumi ndio maana kilichotizamwa ni kuongeza mapato na sio kuangalia kupunguza gharama kwa taifa kwa usafiri huu.
lakini bado hata gharama zikiwekwa kote bado inakuwa ni vizuri maana inasapress magari ya binafsi zaidi kuliko hiyo gharama kuchangiwa na public wanaotumia kwa pamoja.
jambo moja linalotupotosha wananchi ni kukosa maarifa maana badala ya kudai kila mwanya ubanwe ili tuboreshe uchumi wetu sisi tunadai kama kuna sehemu imeachwa basi maeneo yote yaachwe.
jambo moja la kufahamu ni kuwa tukiambiwa rushwa ni adui wa haki hatuelewi na sisi wananchi tunakuwa mstari wa mbele kuzilea lakini jambo la kutambua ni kuwa hoteli inamirikiwa na mtu, mgodi unamirikiwa na watu na katika mazingira ya rushwa ni rahisi sana wamiriki au waajiriwa kutoa rushwa kwetu sisi wenyewe au viongozi wetu na kodi stahili isikusanywe lakini niambie nani anaweza kwenda kutoa rushwa ili kuzuia kodi hizi unazozisema?
biashara kubwa kubwa na za sekita binafsi tunaweza kuzidhibiti kwa kudhibiti "corruption" lakini kabla ya hapo sisi wanyonge ni lazima tuendelee kukamuliwa ili uwezo wetu angalau wa serikali kutekeleza majukumu yake usishuke. mkiambiwa ni hatari matajiri kukumbatia serikali hamutambui mnabaki kuangalia misaada ya kupewa lift njiani na kupewa chakula kama una njaa lakini ukweli ndio huo kuwa matajiri wanajiweka kwa serikali ili wasilipe kodi, ili wapate kandarasi zote na mengine.