Mi nina buku!Mbona unalialia?kwani wewe umejipangaje?
Na mimi pia naelewa hivyo, mkuu mshana jr ufafanuzi tafadhali
Kama kuna sehemu imelemewa na kodi mbalimbali za serikali basi ni kwenye chombo cha usafiri,
Baada ya kutubana kwenye road license, fire extinguisher, petrol na diesel, vipuri na lubricants nk nk leseni za udereva, kulipia ukaguzi, ongezeko la import duty, nk nk sasa maumivu safari hii yameletwa kwenye bima
Kwanza bima ilipandishwa kutoka elfu 50 third party mpaka laki moja, na comprehensive nazo zikapanda kwa kiwango vyake, wamiliki tulalalamika kidogo lakini tukaridhia.
Sasa limeletwa la VAT kwenye hizo bima, sasa hivi ukinunua bima ya kiwango chochote nk shurti ulipie na ongezeko la thamani 18%, huku ni kuzidi kunyonga na kuwaumiza wananchi kwakweli.
Tunaelekea ni kurudi kwenye enzi ileile ya kumiliki gari inakuwa kama kitu cha kifahari na gharama kubwa, ukija kujumlisha utitiri wa malipo unayofanya kwa gari dogo tu la milioni 8, ni gharama ambayo kwa maisha ya mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu na akifanya hivyo anaumiza bajeti kwenye mambo mengine ya muhimu.
Serikali hii na watoa maamuzi wake sijui wanaishi dunia gani kushindwa kuyaona haya.....
Ngumu sana mkuu kui-uninstall CCM,wajinga ni wengi sana,unakutana na kijana mdogo tu tena mjanja kabisa wa town unakuta anatoka mapovu na mishipa ya shingo inamtoka just kuutetea uchafu huu CCM.Mwisho wa manyanyaso na kodi zote ambazo ni unreasonable ni October.
kwa mtizamo wangu binafsi ni jambo zuri sana na wasiishie kwenye magari tu bali vitu vyote vinavyotoka nje viweke mazingira magumu ya kununua na kuviendesha na hivyo ndivyo tutalinda uchumi wetu. ukisikia wajapani wanatajirika ni kwa kutuuzia magari, sasa mpaka lini fedha yetu itawaajiri wajapani wanaotengeneza magari na kuacha kutoa ajira kwa watoto wetu?
jambo la msingi ni serikali kuboresha usafiri wa umma ili usafiri usiwe shida.
acheni kulialia lipeni kodi....
Ni rahisi kuliangalia kwa mtazamo huu lakini comprehensive sio magari binafsi tu bali ni magari yote yakiwemo ya mizigo na abiria
Kila senti inayoongezeka kwenye chombo chochote kinachoitwa gari maumivu ya mwisho huja kwa mwananchi wa kawaida, kulipa kodi ni ada lakini je tunaangalia ni maeneo gani yanapaswa kubanwa na maeneo gani yanapaswa kupewa unafuu?
Makampuni ya simu na migodi, mahoteli na uwekezaji mkubwa maliasili na utalii huko kuna kodi nyingi sana zinaachwa au kusamehewa wakati ni watu wenye uwezo wa kuzilipa halafu anakuja kuumizwa mntu wa chini na bado tunatetea...!!???kweli!?
Siku hizi toka july 1, 2015 ukiingiza gari kuna kodi unalipia inaitwa Railway Development Levy kwa walioingiza magari toka tarehe moja july mtakuwa mmeshakutana nayo ilikuwa haipo kabla
Ni kweli hiyo Railway Development Levy eti wameiweka kwa ajili ya kupata hela ili waendeleze miundombinu ya Reli