Wamiliki wa Mabasi na mafuso hutoa wapi hela?

Wamiliki wa Mabasi na mafuso hutoa wapi hela?

Mkuu unacho sema ni sahihi kabisa,Matajiri wengi ni Mikopo na bila hiyo huwezi kuendelea financially but tunaanzaje sasa kupata hata ghorofa 1 pale Kariakoo.
Tatizo watu wanaleta elimu humu bila kutuambia chanzo cha hizo assets zisizohamishika. Zilipatikanaje.

Ili upate hela lazima uamini watu wanachapa kazi na si vinginevyo. Lkn ukweli konekshen za utajiri Ni nyingi Sana. Utajiri wa haraka.
 
Kuna mtu namfahamu Ana Shimo pale mererani, shimo lake lina uwezo wa kutema vyombo kila mwezi,makinikia ndio usiseme.

Huyu akisema anakopa Anauwezo wa kukopa kununua hayo mabus yote uloyataja na chenchi ikabaki.

Kuna watu wana miliki Assets ambazo ndio maisha yao, Nyingi zisizoonekana.

Mabus na Malori ni vinyongeza tu...
Chanzo chake mkuu hujaelewa.

Unafikiri kumiliki mgodi Ni shughuli ya kitoto, Tena Mirerani.

Tatizo mnazungumzia matokeo. Hayo unayoyaona Ni matokeo ya Siri na chanzo cha fedha usichokijua.

Kwasababu huyo mtu hakutoka tu nyumbani asubuhi akapanda gari akaenda Mererani akaanza kumiliki mgodi.
 
..ngoja nikupe mfano mmoja tu wa jinsi wanapata pesa....uone wanavyopiga hela.....chukua basi moja la sh. mil.300...anakopa benki mil.300..ananunua basi......hili basi lina viti hadi 55....kwa safari ya dar moshi nauli sh. 45,000/...kwa viti 55 ni sh. mil. 2,475,000/ kwa trip moja kwenda dar (hapo hujaweka bei ya mzigo)....hapo ukitoa mafuta na service labda mil. 1....anabakiwa na mil. 1,475,000/anakunja kwa siku....piga mara siku 30 (mwezi)....ni mil.44,250,000/ kwa mwezi....piga kwa mwaka (miezi 12) unapata mil. 531,000,000/ hilo ni basi jingine jipya na baki zaidi...hapo ni basi moja limeleta hiyo pesa......kama ana mabasi mawili??au matatu??...kila mwaka ana uwezo wa kununua basi...hata mawili.....na alianza na mkopo wa mil.300 tu benki.....HAKUNA UCHAWI HAPA...NI KUJARIBU TU...KWA KUAMINIWA NA BENKI....SASA HAWA WENYE MABASI WANACHUKUA HELA BENKI WANAVYOTAKA....HIYO NDIO SIRI...

Ww acha uongo hakuna bus ya namna iyo
Bus ynye vit 45 inaweza kuondoka na abiria 30 tuu siti nyingine wazi mpk mwsho wa safari na katk hao abiria 30 sio wote wanafika mwsho wa safari ivyo nauli inashuka
 
Mkuu unacho sema ni sahihi kabisa,Matajiri wengi ni Mikopo na bila hiyo huwezi kuendelea financially but tunaanzaje sasa kupata hata ghorofa 1 pale Kariakoo.
Sio lazima uwe na ardhi kariakoo.... tafuta milion 5 kanunue shamba huko ndani ndani lima mkonge au parachichi au pamba au kahawa au nazi. Then tumia hyo ardhi kupata mikopo ya pesa ndogo ndogo ambazo utazizalisha mpaka uweze kununua gari au uweze kununua ardhi yenye thaman ya milion 500....... Kidogo kidogo utakua kama BM Coach
 
Wewe naona unataka kuelekezwa waganga walipo kijanja

Matangazo ya waganga yalivyojaa mjini bado nikufuate wewe 🤣 🤣 🤣

Sitaki mganga, sitaki unielekeze kitu, nipe majina tu ya hayo mabasi na mahala yalipo niende mwenyewe. Hili nalo utashindwa sababu ulisimuliwa na wewe ukaamini moja kwa moja kama nyumbu ndo maana nasema story za ushirikina zinaaminiwa na watu mazwazwa wavivu wa kufikiri.
 
Chanzo chake mkuu hujaelewa.

Unafikiri kumiliki mgodi Ni shughuli ya kitoto, Tena Mirerani.

Tatizo mnazungumzia matokeo. Hayo unayoyaona Ni matokeo ya Siri na chanzo cha fedha usichokijua.

Kwasababu huyo mtu hakutoka tu nyumbani asubuhi akapanda gari akaenda Mererani akaanza kumiliki mgodi.

Wabongo wengi wana comprehension disorder wagumu kuelewa na kung'amua mambo.
 
Pesa za majini zipo. Niko apa Nmekaa. Huwezi kujua kila kitu.

Achana na pesa wewe. Wewe ndio una mawazo ya kifukara kuamini hizo fedha za aina hiyo hazipo.

Nenda kalime matembele na mihogo. Upate hela ununue Marco Polo 50 km Dar Exoress anazomiliki.
Siwezi kukubishia mkuu kwakuwa wewe umeamua kuamini hivyo. Unaweza ukalima matembele na ukawa bilionea vilevile iwapo utafanya tofauti na mazoea.
Watu wengi wenye pesa wanafikiri na kutenda tofauti na malofa.
Malofa ndo washirikina wakubwa, muda mwingi wanautumia kuloga watu wenye mafanikio na wao wanaendelea kuwa malofa.
Mkuu endelea kufikiria kuwa pesa ndefu lazima ufuge majini.
Utakufa ukiwa lofa mwandamizi.
 
Unajua utajiri nikuona fursa kabla ya watu wengine hawajaiona nayo inachangia kuwa Tajir mfano kunakipindi m-pesa ya vodacom wakat inaanza ilikuwa ina tafuta wakala mkuu wa kanda mabosi wengi walifatwa na vodacom wakaambiwa wengi waliikataa hawakuamini kama itakuwa na deal inaelezwa kuna boss mmoja akaweka mzigo meza akachukua uwakala wa kanda fulani sasa unaambiwa yule boss anakula commission ya si chini ya million hamsini kwa mwezi na wenzie waliokataaga wanaishia kujilaumu had leo wAna jilaumu kwanini waliikataa ile fursa na jmaaa alitemgeneza mawakala kibao wa mpesa na kila hela wanayo pata mwamba anapata chake cha juu sasa hyoo ni aliweka tuu sio ulikuwa mchongo wake main asa mtu kama huyo si anakimbiza sana hata Mo dewj aliulizwa nibkitu gani ulikpuuzia unajilaumu had leo alisema kuupuuzia mitandao ua simu nakuamini haitamletea Hela nyingi siku za usoni na akati Nilikuwa na uwezo wakuweza huko :::halafu old school wengi wananidhamu ya fedha tofauti na generation ya saiv mtu akapata profit ya 20 anaweza piga hata millon 2 kiberit kwa starehe .so mambo ni mengi chungulia fursa jilidhishe choma ndani acha kusuasua
 
Kuna mtu namfahamu Ana Shimo pale mererani, shimo lake lina uwezo wa kutema vyombo kila mwezi,makinikia ndio usiseme.

Huyu akisema anakopa Anauwezo wa kukopa kununua hayo mabus yote uloyataja na chenchi ikabaki.

Kuna watu wana miliki Assets ambazo ndio maisha yao, Nyingi zisizoonekana.

Mabus na Malori ni vinyongeza tu...
Mererani kwa sasa nasikia ni njaa tupu watu wana ambulia Chenga....
 
Kuna mmiliki mmoja wa mabus tulikutana nikawa namuuliza chanzo Cha yeye kuwa tajiri (bilionea ) aliniambia alikuwa anafanya biashara ya mazao ndo akapata mtaji ila tulipo zoeana aliniambia ukitaka kuwa tajiri kuwa "MWIZI" tena usiibiwe wananchi utauliwa ibia serekali maana yete analetaga bus 10+ kwenye kila bus anaweka vipuri vyenye saman ya hilo bus tena alafu analipa Kodi kidogo kwenye bus vipuri vinaputa free
 
Imagine, kuna haya mabasi

Ester Luxury
Tilisho
Happy Nation
Sauli
New Force
Arusha Express
Shabiby
Abood
Machame Express
Kapricon
Kilimanjaro Express
Dar Express
Zube
Saratoga
Mgamba
Kimbinyiko
Abc
Ally's
Saibaba
etc etc

Malori ndiyo usiseme.

Unakuta mtu ana basi 10, 20 au 60. Basi moja bei yake ni Milion 300, 400 hadi 500. Jamaa wanapata wapi hela aisee?
Hizo hela unazoskia kwaa CAG znapigwa kila siku unahis znaendaga kufanyia nin.
 
Kabla hawajawa na hayo mabasi wanamiliki "real estate" za maana sehemu tofauti.

Ukiwa na Plot 1 tu pale k.koo msimbazi, una uwezo wa kukopa Bank hela ya kufata Yutong zako hata 10 na ukapewa.

Matajiri hao, sifa yao kuu ni 1 "wanakopesheka" Muogope mtu anaeweza kukopa 1B na akapewa muogope sana huyo mtu.

Mpaka upewe kuna vigezo vingi taasisi za ukopeshaji huziangalia ikiwemo mali zisizo hamishika.

Wewe unayaona mabus na malori lakini Hizo taasisi wanajua mali za thamani zaidi ya hayo ma bus na malori.

Ungezijua hizo mali wanazomiliki mpaka wakawa na sifa ya kukopesheka hivyo ndio Ungeandika Thread GAZETI na ???????? ungeanza nazo mpka unamaliza nazo.
Kaka.. weng wao 90 wanapata pesa nying hzo kwenye chains za wezi wa pesa za serikal unazoskia CAG kila siku anatolea maelezo... Mim nna ndugu yangu ndo michongo yake hyo.. na ana 28 yrs tu ana malori kama 6 hiv.. viwanja sinza kinondon. Kama vi3.. ana magar binafsi kama 6 hiv.. mtoto mdogo tu... Akiienda kidimbwi ana mil15 kwenye gar.. na ana kundi lake hilo ni chain ya watoto wa vigogo tupu.. so it is what it is.
 
Ukiwataja wazazi wa wengine na wako lazima watajwe kwa uzembe wa kutotafuta mali

Unajua uwezo wa wazazi wangu? Na ni lazima wazazi wawape watoto mashamba? Kwahiyo kuwataja inamaanisha wazazi wangu ni wazembe? Hao ni watu nawajua na ndo njia walizotumia tukiwaona. Haimaanishi ni lazima wazazi wanipe mashamba na mimi niwekeze kwenye mabus, Wakinipa kampuni/miradi je?

Huu ndo ubaya wa JF unaweza kuta unabishana na mpangaji wako na unamdai kodi.
 
Hela za magumashi zipo acha kujifanya kama wewe huishi dunia hii tunayoishi.
Wewe sema hutaki ushirikina lakini usiseme hazimo. Tumeona mabasi hayaondoki mpaka yazungukwe na mazezeta na zezeta atakacho mwambia konda au agent wa gari atampatia.
Nimeona tajiri mmoja wa vyombo vya usafiri yeye gari zake hazilali nje ya nyumbani kwake na kama unakodi ukisema hairudi usiku huo basi biashara inakufa. Gari hizo kilasiku usiku hukojolewa. Sasa hiyo kawaida?

Yupo mmoja kila alhamis nadhani kama sio ijumaa lazima aanguke kifafa na akishajisaidia hajakubwa ndio anaenda kufungua duka. Sasa wewe unabisha nini? Huwezi jua kilakitu. Ishi,uliza na tembea sana uone mengi

Habari ya kutaka kutajiwa majina achana nayo
ACHana nae aamin anavoamin me nilikua na ndugu yang kabisa Alikua na ela chafu ila anavokaribia kufa aliongea yoteeee Mbele yetu tena alituita kwasabab ni mdogo wa mshua hii dunia ina mambo
 
Wanakopa benki..hujanisoma unakurupuka kuuliza....

Una comprehension disorder and it shows.

Huko bank unakopa bila dhamana? Dhamana yako ni nini na unaipataje au unaokota hiyo dhamana?

Mtu mwenye genge la nyanya za buku anaweza kwenda bank kukopa 300M?

Swali ni wanawezaje kufika to that point ya kukuposheka hela nyingi? Sijui mlienda shuleni kusoma ujinga.
 
Back
Top Bottom