Hiyo mbinu nayo inakaugumu kake. Kutokana na wizi na ujambazi uliokuwa umekithiri kwa maboat ya abilia goziba walianza kutumia mbinu hii miaka mingi tu. Ili mtu asisafiri na pesa ila tatizo linakuja kuwa kuna mazingira ambayo yanapokea pesa ila hayatoi na kuna mazingira yanatoa sana pesa kuliko kupokea. Endapo hiyo kampuni itafanya hivyo kuna muda itabidi yenyewe itumie tena miamala ambayo imewakwepesha nyinyi.
Mfano
Watu wengi hutuma sana pesa kutoka dar kwenda mkoani ila hawatumi kutoka mikoani kuja dar. Hivyo ofisi za kampuni za mikoani zitagawa zile pesa mpaka zinaishiwa huku ofisi ya dar ya kampuni ikiwa imejaza magunia ya noti ndani. Hivyo kampuni itahitaji kusafirisha tena hizo noti ama itumie miamara ya kibenk ama miamala ambayo imewakwepesha nyinyi. Kwakifupi huo mchakato unaharufu ya kufirisi mtu
Sent from my TECNO K7 using
JamiiForums mobile app