Wamemuingiza cha jiji halafu wanejitenga naye!

Wamemuingiza cha jiji halafu wanejitenga naye!

hiyo mingine tunahitaji kuiona kwasababu hata tusipoiona kuna siku tu kiongozi mwingine kama magu ataingia na tutaijua. ila naamini kwenye katiba na sheria, vifungu vya adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa wahujumu uchumi vinatakiwa kuwepo. china wameendelea kwasababu ya sheria hizo. hawana kuremba kwenye mali ya umma. na hizi kinga kwa viongozi, unaweza kukingwa ila mali kama uliiba tuwanyang'anye wabaki mikono mitupu.
 
Niliwahi kuingizwa cha kike!
Nikachomekewa demu, nikaingia kichwa kichwa! Nikaambulia kuumbuliwa na aibu ya mwaka! Kuwafuata walioniiletalea msala wakanikimbia!

Wamemchomekea akasaini mikataba thenashara mara tatu kasoro 4.. Mmoja tu uliovuja umeshaleta taharuki kubwa sana! Haufai haufai haufai.. Vipi hiyo mingine 31 ya siri?
Inasemaje?
Itavuja lini?
Itasambazwa lini?
Masharti yake ni yapi?
Nknk
Kwa mtazamo wa haraka sana hiyo mingine 31 haina tofauti na huu wa 32.. Labda kwenye eneo husika
Miundo mbinu reli
Miundo mbinu airports
Miundombinu barabara
Miundombinu mawasiliano
Kilimo
Ufugaji
Maliasili madini
Maliasili misitu
Maliasili mbuga
Maliasili utalii
Maliasili maeneo ya kihistoria
Kodi
Utawala
Siasa
Elimu
Imani
Mingine siifahamu

Master mind wa hii mipango wapo lakini hawajitokezi waziwazi wanasukuma gari kwa nyuma mbele huwaoni ila unaona gari linasonga
Likikosea njia
Likifanya ajali
Likivunja sheria
Lawama ni kwake kwakuwa ndio wamemuweka kwenye usukani lakini hawezi kuwazoom hata kwenye sight mirror maana wako nyuma ama kwenye blind spot!
Wamemuingiza pabaya hawezi kuchomoa ama kuchomoka na hawezi kulazimisha la sivyo ama zake ama zao! Ameshika kwenye makali wameshika kwenye mpini!

Kumkoma nyani jiladi..!
Muda pekee ndio utaokoa ama kuzamisha jahazi ama la kudra za mwenyezi Mungu mweza wa yote!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ubongo haufanyi kazi ya kufikiri vizuri lazima haya yatokee
 
Heshima ulojijengea hapa jamiiforum unaishusha kwa kasi sana kwa ambazo alitakiwa kuanzisha ziro iq unaanzisha ww
 
WaTz mnajifanya mnajua kuandika mnajificha nyuma ya keyboards zenu... Uhalisia WaTz ni maandazi tu 🤣😅 tokeni barabarani muonyeshe hisia zenu... Ndiyo maana hata viongozi wa darasa la 7B wanawaburuza watakavyo kwasabab hamjitambui
 
Yote haya ni uduni wa elimu. Pale unapounga unga certificates kadhaa halafu upewe vitu vinavyohitaji elimu ya kweli lazima uvurunde.
Ni sawa na kudanganya kwenye CV kuwa unajua kifaransa ilhali hujui, akija mfaransa lazima uishie kusema bonjour mwanzo mwisho.

Na jamaa wana akili, wamemvika kilemba cha ukoka kwa kumtunuku udaktari wa heshima ili na yeye ajione wamo huku nyuma wenye elimu, udaktari wa kweli, ujanja na akili zao wanakula kiulaini.

Hii ni ithibati kuwa sio kila anaeonekana anakushangalia huwa anakushangalia, wengine huwa wanakuzomea. Huu ni mwanzo wa kuzomewa kwake huku akiwa anadhani anashangiliwa, akija kuamka na mawe yatakuwa yanarushwa pamoja na kuzomewa huko.
 
hiyo mingine tunahitaji kuiona kwasababu hata tusipoiona kuna siku tu kiongozi mwingine kama magu ataingia na tutaijua. ila naamini kwenye katiba na sheria, vifungu vya adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa wahujumu uchumi vinatakiwa kuwepo. china wameendelea kwasababu ya sheria hizo. hawana kuremba kwenye mali ya umma. na hizi kinga kwa viongozi, unaweza kukingwa ila mali kama uliiba tuwanyang'anye wabaki mikono mitupu.
ila naamini kwenye katiba na sheria, vifungu vya adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa wahujumu uchumi vinatakiwa kuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimegundua haters wa mama hamna akili, mambumbumbu mliojaa wivu na husda......lakini pia WASHAMBA a.k.a WAPORIPORI. Hamna hoja mmebaki kupiga ramli chonganishi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom