Ni kweli Nina hasira sana, ni kwa sababu jambo kubwa linatutokea ambalo lilikua ndani ya uwezo kulizuia lisitokee
Mtu unamwambia ule ni moto anaamua kwenda kuweka mguu hapo hapo,
Mwisho wanakuja watu kukulaum ww uliemtahadharisha asipite kwenye moto
Otherwise nashukuru kwa uelewa, infact napona haraka kwa comment za namna hii kuliko wale wanaokimbilia kusema nilitaman mirathi, wengine Nina wivu, wengine Nina gubu, yaani nilitamani kuipiga sim chin kwa hasira
Nimekaa zaidi ya saa mbili kuandika ile post Jana, nikijaribu kwa kadri ya uwezo wangu kuwa mkweli, kueleza kwa uwazi kabisa
Nimefikia hatua ya kueleza kwamba mke wangu ni mwaminifu na sijawahi kumshika kwa uzinzi pamoja na kumwekea morden surveillance ya 24 hrs
Sasa ningelisema hili kweli mkuu kama ningekua biased kwenye post hiyo?
Kosa langu ni kujitenga na hiyo kesi, na hii ni kwa sababu ya ghadhabu niliyonayo moyoni
Binafsi nimeomba likizo kazini kwa ajili ya hili Nina uchungu mno