Wamarekani wanatembea na silaha

Ritz ndio maana nikasema mimi kama mimi!. Labda nina bahati... Hahaa!. Halafu nadhani hukunielewa kuhusu sehemu ya kuishi, sijakushutumu; nilikua natoa mfano tu!. Siri kubwa ya kuepuka hizo adha ni DISPLINE!.
 
Tatizo kubwa sana la US ni haki na uhuru wa raia yeyote kuwa na bunduki na kutembea nayo. Imepunguza sana kujiamini kwa Polisi wanaposhughulika kukamata na kudhibiti watuhumiwa wa uhalifu. Na ile stereotype ya watu weusi na uhalifu ndio mambo yanazidi kuharibika.

Siamini kama tatizo la ubaguzi wa rangi ni kubwa hivyo. Tena US kuna afadhali kuliko katika baadhi ya nchi zetu za dunia ya 3. Wao wasipodhibiti huo uhuru wa mtu kujikusanyia bunduki anavyotaka basi hali itaendelea kuwa taabu mtindo mmoja. Watu wanaishi kwa kuogopana. Malumbano ya kawaida tu watu wanatoleana pisto! Usikatize jirani na uzio wa mtu huko suburbs anaweza kukulipua akihisi tishio.

Huyo jamaa mweusi aliyeuawa na Polisi kwanza ile kubugudhiwa na ombaomba tu kamtolea pisto. Haya huyo aliyeua polisi alikuwa na zana za uhakika hadi jamaa wakaamua kumpelekea bomu kwa robot kummaliza! What a country!
 
hicho ulichosema rais Philippines amekisema kwenye sikukuu ya eid
 
Ndiyo, hali siyo mbaya kabisa na hizo picha wala hazihusiani chochote na mauaji ya hao jamaa wawili.

Mnalazimisha mambo na kutamani sana Marekani ichafuke lakini haitotokea.
Hamna anayelazimisha hali halisi ndiyo hii huko Marekani hii Dallas.
Hii Atlanta.

Hii Alabama.

 
Hamna anayelazimisha hali halisi ndiyo hii huko Marekani hii Dallas.
Hii Atlanta.


Sasa huoni kwamba hao watu wanaandamana kwa amani kutoa dukuduku lao?

Hali ingekuwa mbaya kihivyo unadhani hao watu wangepata hata hiyo fursa ya kuandamana na kurudi makwao salama?

Halafu waandamanaji wala siyo weusi tu....uthibitisho kwamba idadi kubwa ya walio wengi, licha ya rangi zao za ngozi, wanakataa matendo ya polisi wachache walio waovu.
 
Sasa hivi tumeshazoea kusikia wamarekani wakimalizana wao kwa wao....
USA BABY[emoji631] [emoji631] [emoji631]
 
Hii Phoenix.

Halafu tunaambiwa hali ni swali.
 
Dukuduku la nini?
 
"DUNIA KAMWE HAITOTULIA MPAKA TUPATE ADUI KUTOKA NJE YA DUNIA"
Umetumia akili kubwa sana mdau hadi kuongea hilo jambo,
Ni kweli " Dunia kamwe haitotulia mpaka tupate adui kutoka nje ya dunia"
Hongera sana kwa huo ukomavu wako wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…