Amani gani wewe!
Tatizo ni kwamba mnapandikizwa chuki na propaganda nyingi sana ili kutuchafulia Uislam wetu, lakini kwa kuwa sisi ni waerevu wala hatuna shaka, tunawaangalia tu.
Basi hizi Dini unazozidharau ndizo zinazosaidia sana kwa mtu mwenye Imani yake.
Dini zinatufundisha unyenyekevu, kutodhulumu, kutoiba, kutokuua, kutofanya Zinaa na mambo mengine mengi sana ambayo sihitaji kuyahorodhesha hapa.
Nijuavyo mimi Dini zetu uwe Muislam au uwe Mkristo (naomba nilenge hizi Dini mbili kwanza) zinatufundisha Amani, Upendo na Kupendana kwa ujumla.
Mimi nimezaliwa kutoka kwenye community ambayo Muislam na Mkristo ni ndugu Msiba wa Muislam, Mkristo atahudhuria na msiba wa Mkristo, Muislam atahudhuria, na si kwa ajili ya matatizo tu hata sherehe. Na maisha yetu ya Uswahilini ndivyo yalivyo, sasa sijui wewe sio Mtanzania!
Mimi hapa unaeniona ni Muislam halisi, lakini huwezi amini nimeshaingia Kanisani mara nyingi sana ikiwemo kufanyiwa maombi kabla ya kufanya Mitihan(pepa), nimeshaingia Kanisani kwa ajili ya kupoteza mshikaji/washikaji wa karibu, siku tunayoenda kuzika tunaingia Kanisani yanafanyika maombi yote tunapiga magoti tunarudi kukaa kisha tunapiga tena magoti mpaka tunamaliza tunatoka na mwili kuelekea makaburini kwenda kuzika. Kitu ambacho sijawahi kufanya nikiwa Kanisani pale kwenye kupanga mstari kisha mnalishwa sijui kitu gani na Mzungu, ile sijawahi ila mambo mengine yote nimeshawahi.
Na kwa kukuongozea nishaingia Kanisani siku za Jumapili Misa tofauti tofauti, na hii yote sababu ya walimbwende, kuna baadhi ya warembo wakati mnapokuwa kwenye uhusiano wanapenda kampani "kama vipi kesho nikupitie twende Kanisani" mimi huwa sikataagi huwa najibu "wala usihofu Mamaa niambie saa ngapi niwe tayari", na kweli siku inayofuata tunaenda wote Kanisani.
Mimi nimezaliwa kutoka kwenye community ambayo Muislam na Mkristo ni ndugu Msiba wa Muislam Mkristo atahudhuria na msiba wa Mkristo Muislam atahudhuria, na maisha yetu ya Uswahilini ndivyo yalivyo, sasa sijui wewe sio Mtanzania!
Kwahiyo sioni cha ajabu mimi naona mambo mengi yanafanana, njia inaweza kuwa tofauti lakini tunapoelekea ndio huko huko, ya mbele tunamuachia Mwenyezi Mungu