Wamama wajawazito kujifungua kwa gharama ya TZS.150,000/ Hospitali za Serikali. Je, Serikali hii inatupeleka Wapi?

"ukitaka kujua ubaya wa kifo nenda hospitali" by Dr. Remmy
Iko siku utajua kwa dhati kabisa kuwa hili ni miongoni mwa maswali ya hovyo kabisa umepata kuuliza mbele ya kadamnasi.

Hongera kwa kujaaliwa ukwasi.
Plan your life, bimbo, plan.
Nyie ndi mnazaa watoto mkisema kila mtoto ana riziki yake.
Halafu hata shule ya bure unashindwa kumpeleka kwa kukosa kumnunulia sare.
Ulimzaa wa nini?
 
Huku wameshapiga marufuku au bwana yule ndiyo kinara wa kuwaambia wananchi wake wafyatue kwa kwenda mbele

Ati MABEBERU wanatuletea uzazi wa mpango
Thats the problem.
Mtu anazaa without any resrvations, halafu anategemea FREE welfare service huku akifikiri simebody some where atalipa kodi ili apate free service.
China walipopiga marufuku kuwa unaruhusiwa mtoto mmoja tu, walijuwa wanafanya nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninavyofahamu kuna mikoa ambayo ilikuwa inatoa bima za bure kwa wajawazito ambazo zilikuwa zinafadhiliwa lakini mradi umefika mwisho hivyo kwa sasa suala la kulipia lipo japo sina uhakika ni shingapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa kabisa mkuu, inaitwa KFW,mama ukiwa mjamzito unapewa no maalum na unahudumiwa kama mtu wa NHIF na mojawapo wa wafaidika ilikua mkoa wa Tanga nami pia ni mmojawapo, japokua nina NHIF lakini niliwekwa kwenye mradi huo, Sasa kama umetolewa itakua shughuli pevu mana ilikua msaada mkubwa kwa wamama wasiojiweza kulipia matibabu, hiyo huduma bure kwa serikali ni uongo maana unaambiwa matibabu bure lakini unajinunulia kila kitu kuanzia dawa za kuongeza damu, mpaka mipira ya kuvaa mikononi yaani gloves na vingine vingi, nakataa hakuna matibabu bure si kwa watoto wala wajawazito, na gharama za huduma unalipia hasa hospitali za mikoa
 
Kama nakumbuka sawa Kujifungua Wamama Waja Wazito ilikuwa bure kabisa, lakini mambo yamebadilika Wandugu sasa hivi kwa Kujifungua kwa Njia ya Kawaida ni TZS.150,000/- na Kwa njia ya Upasuaji ni TZS.300,000/-. Naiona kasi kubwa ya kurudi kujifungulia akina mama kwa Wakunga ama Majumbani.


Kumbuka azimio la Meatu "zaeni watoto wengi"
Maana yake mapato yataongezeka
Lakini pia wanawake wengi wataelekezwa kwenye uzazi wa kupasuliwa ili kuinua mapato
Familia masikini zitajichuja na hatimaye kufutika kabisa kwenye ramani ya nchi
 
Kumbuka azimio la Meatu "zaeni watoto wengi"
Maana yake mapato yataongezeka
Lakini pia wanawake wengi wataelekezwa kwenye uzazi wa kupasuliwa ili kuinua mapato
Familia masikini zitajichuja na hatimaye kufutika kabisa kwenye ramani ya nchi
Na haswa ndiyo target yao! Kikubwa Serikali iache unafiki na Kuwadanganya wasioelewa!
 
Umetoa mahari ukaoa, mkafanya mambo yenu mimba ikatungwa toka mimba inaingia inakua kwa miezi tisa, mimba sio ajali kama ni MTU makini huna sababu ya kulalamika na vilaki 3, wapo watu wanaougua magonjwa kama presha, cansa na mengine mengi acha hao ndio wapewe huduma za bure maana magonjwa hayo yanakuja bila taarifa, sio wewe kwa starehe zako unataka na starehe upate bure! Ona aibu kupenda dezo sio wakati wake hutaki acha kuzaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujifungua ni bure ila kumpa mtu mimba ndiyo kuna kulipia chips, kuku, beer, gesti, vocha na nauli.
 
Back
Top Bottom