Wajawazito hawastahili bima ya afya?

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,826
2,843
Hivi kwa nini serikali inalazimisha wajawazito wachangie miaka miwili ndipo WALIPIWE GHARAMA ZA KUJIFUNGUA? Sio JUBILEE, Siyo NHIF wote wanasema ili alipiwe gharama za matibabu wakati wa kujifungua LAZIMA awe amechangia mfuko wa NHIF at least mwaka mmoja, wakati wakijua fika UJAUZITO NI MIEZI TISA TU!

Yaani serikali inaona sawa kuwaongezea mishahara na marupurupu Wake za viongozi huku wakiweka vigezo vigumu kwa watumiaji!

Sijaamua kuzungumzia, TOTO AFYA CARD, nimegusia tu hili la wajawazito mnamaanisha nini kwa mama zetu Hawa? Au mkishapanda mav8 yenu na kutibiwa huko AGA KHAN na REGENCY mnasahau watanzania?

Kuna maana gani kuwahimiza watanzania kutumia NHIF ilhali mkijua wajawazito WATATAKIWA KULIPIA ILI WAPATE HUDUMA?

CCM na WAPINZANI WOTE kwanini hamlioni hilo?

Nasubiri mapovu, Mungu akubariki waziri wa afya UMMY MWALIMU 🙏
 
Back
Top Bottom