Wamama wajawazito kujifungua kwa gharama ya TZS.150,000/ Hospitali za Serikali. Je, Serikali hii inatupeleka Wapi?

Kama Kichwa cha Habari Kinavyojieleza!

Kama nakumbuka sawa Kujifungua Wamama Waja Wazito ilikuwa bure kabisa, lakini mambo yamebadilika Wandugu sasa hivi kwa Kujifungua kwa Njia ya Kawaida ni TZS.150,000/- na Kwa njia ya Upasuaji ni TZS.300,000/-. Naiona kasi kubwa ya kurudi kujifungulia akina mama kwa Wakunga ama Majumbani.

Bila shaka ndiyo Utekelezaji wa Serikali ya Wanyonge hii!

Tuendelee kufurahia Utawala wa awamu ya 5!

Ushahidi, Ndugu yangu Katoa pesa kiasi hicho wakati anajifungua.

Eeh Mfalme wetu Uishi milele!
Tuwekee picha ya risiti aliyopewa huyo ndugu yako kama wewe sio mzushi.

Bomba Mvua
 
Hii ishi nilikuwa Mbeya wiki iliyopita nikakuta kuna bodaboda wanaijadili kuwa enzi za Mama zetu kujifungulia nyumbani zitarudi kwa kasi na hofu yao ni kwa wanawake wa sasa kuwa hawana nguvu na uwezo wa kujifungulia majumbani na idadi ya wakunga wa jadi imeshapungua kwa hiyo kinachofata ni tujiandae kuzika vichanga kibao huko tuendako. Maana kuihalisia maisha ya wananchi hayafanani wewe unaweza kuona 150,000/= au 300,000/= ni ndogo ila hiyo watu wanaisotea kuipata, yaani pesa wanayopata ni hand to mouth ya vijikazj vidogovidogo yaani inatia hofu kwa watu wa kipato cha chini
 
Mwaka Jana nimeenda kumchukua wife pale muhimbili hospital kuna mama alikuwa amezuiliwa kuondoka hadi alipe deni, mmewake alikuwa anahangaika kutafuta izo pesa wiki nzima hajapata tu, nakumbuka ilikuwa laki moja na elfu sabini deni kamili.
Nilikuwa nimebakiwa na laki moja mfukoni nikaigawa kati kumwachia yuel mama imsaidie kupunguza deni mana wife alinambia huyo mama alimsaidia sana hasa hasa nyakati za usiku.

Hali zetu zinatofautiana sana, kuna watu hawana kabisa huo uwezo wa kutoa hizo gharama.
Ulifanya sahihi mkuu,lakini uliuliza hasa hilo deni ni la nini? Maana hospital kuna mambo mengi zaidi ya kujifungua mkuu.

Bomba Mvua
 
Mbona unaenda kulaumutu!
Je kuna tangazo ambalo linasema hivyo?
Au umetoa rushwatu kwa madaktari wasiofuata maadili?
Kama Kichwa cha Habari Kinavyojieleza!

Kama nakumbuka sawa Kujifungua Wamama Waja Wazito ilikuwa bure kabisa, lakini mambo yamebadilika Wandugu sasa hivi kwa Kujifungua kwa Njia ya Kawaida ni TZS.150,000/- na Kwa njia ya Upasuaji ni TZS.300,000/-. Naiona kasi kubwa ya kurudi kujifungulia akina mama kwa Wakunga ama Majumbani.

Bila shaka ndiyo Utekelezaji wa Serikali ya Wanyonge hii!

Tuendelee kufurahia Utawala wa awamu ya 5!

Ushahidi, Ndugu yangu Katoa pesa kiasi hicho wakati anajifungua.

Eeh Mfalme wetu Uishi milele!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulifanya sahihi mkuu,lakini uliuliza hasa hilo deni ni la nini? Maana hospital kuna mambo mengi zaidi ya kujifungua mkuu.

Bomba Mvua
Hapana sikuuliza mkuu, ila kwa wazo la haraka ni kwamba amejifungua mtoto na amezuiliwa kuondoka hadi alipe deni maana yake ni kwamba huduma hiyo haitolewi bure.
 
Nakupongeza kwa moyo wako, lakini enzi za Welfare State zimekwisha.
Huduma za hospitali ninkodi za wananchi, kodi zenyewe hazitoshi.

Sasa miaka hii kuzaa watoto ningharama, achilia mbali kumtunza mtoto hadi masomo.
Tusijidanganye matamko ya majukwaani, huduma za mahospitalini siyo bure kabisa.
Lakini namba moja kila siku anatuhimiza tufyatue watoto kwa wingi
 
Mimba upachikwe na mwingine siku ya kujifungua wataka free service toka serikalini... hapana kila.mtu abebe mzigo wake. Labda tufanye bonus kwa mtoto wa kwanza nawapili. Watatu na kuendelea jibebe na starehe zako
Unaleta uchochezi.... unapingana na Amiri jeshi Mkuu? Katuambia tufyatue watoto kwa wingi... kwa kuwa tuko kwenye laiti tlaki kwenye Afya na Elimu.
 
Mimba upachikwe na mwingine siku ya kujifungua wataka free service toka serikalini... hapana kila.mtu abebe mzigo wake. Labda tufanye bonus kwa mtoto wa kwanza nawapili. Watatu na kuendelea jibebe na starehe zako
J e watajuaje kama huyu ni moto wa tau na kuendelea?
 
Aache uongo mimi mke wangu juzijuzi tu kajifungua bure tena kwa bima ya bure wanayopewa na wizara na inadumu kwa mwaka 1
 
Back
Top Bottom