Waliowahi kushiriki semina ya IYF Tz tukutane hapa.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,376
24,928
Habari wakuu..

Kwa wale ambao mmewahi kushiriki semina ya kimataifa , International Youth Fellowship (IYF) kwa Dar ambayo ilikuwa ikiratibiwa na ndugu zetu kutoka Japan chini ya mkuu wao Pastor Ock So Park.


Kiukweli ni semina ya aina yake iliyoweza kuniunganisha na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali Africa na duniani kwa wakati mmoja, pia kiroho na kimaisha ilinipatia msingi mzuri sana.


Nakumbuka tulikuwa tukikutana ukumbi wa sabasaba na malazi yalikuwa chuo cha Uhasibu (TIA) Dar, semina ilikuwa ya mwezi mzima! Ukitoka hapo umebadilika kifikra na kimtazamo,.


Workshop kwa ajili ya kujifunza lugha, biblia, taekwondo, keyboard, computer ilikuwa kurasini karibu na baraza la maaskofu.


Sijajua kama hii semina kama bado inafanyika maana kila mwaka walikuwa anafanya.


Nimeikumbuka sana Gracious choir , hii ni kwaya ya wajapan walikuwa wakiimba nyimbo za kiswahili mwanzo mwisho.


Dah acha tu...
c9944df941f94d10e679f2ff7bb7f216.jpg
851035a5f4e5cac1a364ce205ffe6c64.jpg
7f5273cfeffbbc3c9e2fc5bc2350d907.jpg
26d8d59e74729e7e37676c1f7eb64778.jpg
b8f86f3be045480d54a85e1a8683ea82.jpg
 
Back
Top Bottom