Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
JUMA Kassim Ally maarufu kama ‘Sir Nature’, alizaliwa mwaka 1980 katika hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya msingi katika shule ya Kurasini.
Maisha yake ya shule ya msingi yalitawaliwa na soka na kwa kuwa alikua mchezaji mahiri sana wa soka katika timu nyingi za mitaani maarufu kama "cha ndimu" aliamini kuwa kipaji cha soka ndicho kingemtoa maishani na ndio ilikua fani yake haswaa.
Kutokana na ugumu wa maisha ya uswahilini alisoma kwa shida sana elimu yake ya msingi na kubahatika kumaliza japo kwa misuko suko mingi na kutokana na elimu ya miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90 kuwa ngumu sana na kutokuwa na uwezo wa kifedha alifeli darasa la saba, hakufanikiwa kuendelea na shule ya sekondari.
“Elimu ya ‘kibongo’ bila kuwa na mpango mbadala wa masomo ya ziada(tuisheni), ni vigumu kufaulu. Wenzangu waliokuwa na uwezo walisonga mbele mimi nikaishia hapo, “anasema Nature.
Kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo wa kumsomesha, binafsi alikuwa na moyo wa kusoma na aliazimia kufanya kila analoweza ili ajiunge na sekondari mwaka unaofuata ikiwa ni pamoja na kuzunguka majalalani kusaka vyuma chakavu , baada kusota nyumbani kwa mwaka mmoja baada ya kumaliza elimu ya msingi.
“Nilikuwa nikiishi uswahilini, biashara ya kwanza wakati ule kwa watoto kama mimi, ilikuwa kuuza vyuma chakavu, hivyo nilikuwa kiguu na njia kutafuta malighafi hiyo na kuuza, lengo likiwa kutafuta ada,” anasema Nature.
Kazi ya kusaka vyuma chakavu majalalani haikuweza kutosheleza makusanyo ya ada, hivyo ilibidi ajiingize katika upasuaji wa mawe maeneo ya kurasini, kusukuma mikokoteni ya maji na mizigo, kucheza kamali, kuokota mkaa na kuuza vitumbua, mpaka akafanikiwa kupata ada ya kuendelea na masomo ya sekondari.
“Baada ya kukusanya fedha hizo nilipata fedha ya kianzio za kulipia shule binafsi iliyopo maeneo ya Temeke (hakupenda kuitaja),”anasema.
Anaeleza kuwa alisoma huku akiendelea kufanya kazi hizo ili kujikimu katika mahitaji mbalimbali ya shule, ikiwamo kulipia mitihani ya kila wiki, kununulia madaftari, vitabu na vifaa vingine vya shule.
Alipofika kidato cha tatu ndipo alipata hisia za kupenda muziki, ambapo yeye na marafiki zake kadhaa wa shule walikuwa wakienda katika kumbi za starehe na kukutana na vijana waliokuwa wakiimba kutoka shule mbalimbali.
Miaka hiyo ya 90 wakiwa shuleni, kulikuwa na mpango maalumu wa waimbaji wa muziki kutoka mashuleni kupelekwa katika semina ili kuhamasisha kujikinga na maradhi ya Ukimwi, matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Nature na wenzie walikuwa wakifanya uhamasishaji katika Ukumbi wa Amana Center uliopo Ilala na pamoja na Ukumbi wa Ruaha Galaxy uliopo Kimara, hapo ndipo alianza kutunga mashairi akioanisha na kile walichokuwa wakifundishwa na kuimba peke yake akijikumbusha. “Hapo nilihisi kuna kitu kipo ndani yangu kuhusu muziki.”
Hisia hizo za kitu hicho ndizo zilimfanya awashawishi vijana wenzake watatu kuanzisha kikundi kilichokuwa likijulikana kwa jina la For Skills Gangstar (FSG), ambalo kiongozi wake alikuwa yeye akitumia jina la Nature Man.
Wenzake wengine katika kundi hili walikuwa ni Mark 2 B, Chriss na Dollo.
INAENDELEA.....