Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Sukari imeshindikana sasa Hili la wanafunzi nalo ni wazi kachemsha is he a manager or a leader? i wonder
They call him patriotic [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Rais kwenye hili alikurupuka kama kawaida yake haiwezekani mwanafunzi anayesoma diploma miaka 3 akiwa na ufaulu mzuri wa kidato cha nne umfukuze chuo.
Mpaka sasa nimeshindwa kujua mantiki ya rais kwamba ukiwa form 4 huuruhusiwi kusoma chuo kikuu hata kama ni diploma kwa miaka 3? Mbona huu ni mfumo wa kawaida kabisa, rais anashindwa kujua hata vyuo vikuu wanatoa diploma na cheti.
Mfalme anajisahaulisha na hakumbuki hata yeye alianza na diploma!
 
humo kuna vilaza watoto wa vigogo wenye d mbili. hao ndio lazima kutemwa na wahusika kuwadahili wawajibishwe. programu ibakie na div i&ii wa sayansi tu ndio waendelee na ikibidi wsfidiwe usumbufu. wanaopiga kelele wanataka kutubabaisha ili taifa liendelee kubeba makapi kama ndio waalimu wa sayansi.
Makapi ni wale walioanzisha hii program, ambao ni Serikali ya Chama Cha Majipu (CCM). Una lingine?
 
Sheria ya mtandao inatubana sana,Mimi ninachotaka kuandika nashindwa kwa sababu ya sheria .

Ila huyo aliyempa taarifa mh. rais wetu mpendwa kuwa wanafunzi 7000 ni vilaza inabisi afukuzwe kazi kwa sababu atakuwa kilaza .
Muheshimiwa rais wetu mpendwa, malaika na mtakatifu nae kwanini alipokea taarifa kutoka kwa kilaza wakati nae jesca ni kilaza zaidi.
 
Mzee bado hajatuelewa tu

cc Nguruvi3
Mkuu taratibu watatuelewa

Tuliosimama kuhesabiwa siku za mwanzo tulionekana tunaishi jana wakati ni leo
'Tukabatizwa' majina yote mabaya yanayopatikana katika vitabu vikuu vya majina chafu
Tukaambiwa 'tusilimu' hata kama kufanya hivyo ni kuusaliti umma

Tulipewa majina ili tuadhibiwe kwa 'uhalali'.Tukasomewa mashtaka chini ya majina hayo hata uchunguzi haujakamilika. Tukapewa hukmu mbele ya umma bila kusikilizwa

Taratibu wanatuelewa. Itachukua muda lakini watatuelewa. Inaweza isiwe leo au kesho au mwaka huu, lakini tuna uhakika taratibu watatuelewa

The Boss Nyani Ngabu
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses
By Waandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.



Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?
....mzee Mkapa hakukosea, ni wazi "malofa" na "wapumbavu" wamejaa, Trump naye hakukosea kusema bado nchi za kiafrika zinahitaji miaka mia mingine kutawaliwa kikoloni, hoja ya Trump haitofautiani sana na Mkapa, ni kwamba malofa na wapumbavu bado wengi!! The Excellence Dk. Magu, yeye ndo kasiliba kabisa "vilaza", kwani uongo? Rais alikuwa wazi kwamba kuna div one, two, three na ama four zilikuwepo kwa waliokuwa wanachukua kozi special pale UDOM, akaenda mbali kidogo kwamba wenye sifa watatafutiwa nafasi!!! SASA MNATOKEA VILAZA KWA KUHITAJI HURUMA MNAAMINISHA UMMA KWAMBA RAIS AMEITA WOTE VILAZA, KWA HOJA JUMUISHI, mi nasema huu ni ujinga na ni ukilaza wa hali ya juu!!!!
 
Hahahahaha ungemuuliza kuwa alirisiti lini, Matokeo yakatoka lini, akadahiliwa lini, akaanza masomo lini, na admission akapata lini hadi Leo awe Mwaka wa Pili....
Labda huko Chuo kikuu kuna QT kama secondary
 
Kama baba Jesca kashindwa kutofautisha Division one two three na four na kuzichanganya na kuziita vilaza,pia kashindwa kutofautisha diploma na degree kisha kuwatimua Udom na kusahau kuwa wakati huo huo mwanae Jesca Division 4.30 yupo pale anasoma degree huku nae ni Kilaza, Je ataweza kweli kulielewa hili neno "Double Standard"? Si unamchanganya tu mkuu.
Sadam Rais wa Libya ,umeisahau hii
 
Rais Kikwete mimi binafsi sitakusahau ni Rais uliyekoselowa sana na ulisemwa maneno mabaya na ya kijeli pengine kuliko rais yoyote Afrika lakini hukuwazuia hawa vijina kuonyesha dukuduku zao na wala wapinzani huku wahofu na wala hakuna mbunge alifukuzwa kwa mtazamo wake kinzani, hii inamaana bunge la kipindi chako litakuwa historia itakayo simuliwa kizazi hadi kizazi. Hata vijana mponde vipi Kikwete, kwajinsi mambo yalivyo sasa, sisi tuliyo kua wakati wake hatutacha kusema na kukiri 'Bora Kikwete, bhana!'
 
Tatizo mnaongea sanaaaaa ila maamuzi ya Magufuli hayarudi nyuma
Haiwezekani serikali ibebe mzigo wakati wangeweza enda soka A level
Form 4 hata km una DIV 1 PTS 7 bado hustahili kusoma degree direct
Tatizo Bongo kila kitu Polifix
 
Rais Kikwete mimi binafsi sitakusahau ni Rais uliyekoselowa sana na ulisemwa maneno mabaya na ya kijeli pengine kuliko rais yoyote Afrika lakini hukuwazuia hawa vijina kuonyesha dukuduku zao na wala wapinzani huku wahofu na wala hakuna mbunge alifukuzwa kwa mtazamo wake kinzani, hii inamaana bunge la kipindi chako litakuwa historia itakayo simuliwa kizazi hadi kizazi.
 
Inaonekana kuna informer wa mkuu anayemlisha matango pori mbaya.
Inawezekana Mwanzoni kuna umbea alipatiapatia akaaminiwa jumla jumla.
Sasa anampeleka mkuu chaka kwa kutumia usafiri wa mwendokasi.
"The Enemy Within"
 
MTANDAO wa Wanafunzi Nchini (TSNP) umemuunga mkono Rais John Magufuli kwa kuwachukulia hatua za kuwawajibisha waliohusika kuwadahili wanafunzi wasio na sifa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Aidha, mtandao huo umeishauri serikali kusitisha programu maalumu ya kusomesha walimu wa masomo ya sayansi ili kutoa fursa kwa wanafunzi waliodahiliwa kumaliza masomo yao na pia serikali kupanga utaratibu mpya.

TSNP pia imeiomba serikali kuwaruhusu wanafunzi ambao wamebakiza mwaka mmoja wa kumaliza masomo yao ya Stashahada (Diploma) waendelee na masomo yao. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa mtandao huo, Alphonce Lusako katika mkutano wa kutoa tamko la mtandao huo pamoja na la wanafunzi waliofukuzwa UDOM.

Lusako alisema, hatua hiyo haiepukiki kutokana na wahusika kudahili kinyume na vigezo vilivyowekwa na serikali. Aidha, alisema mtandao huo ulikuwa ukifanya utafiti wa kina kupitia Idara ya Tafiti na Mafunzo ya mtandao huo kuhusu sakata hilo.

Alisema serikali ilianzisha programu hiyo kwa lengo la kutatua uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na kuwekwa sifa za udahili, lakini hatimaye Waziri mwenye mamlaka aliondoa na kuongeza kuwa ikitokea mwanafunzi au kundi la wanafunzi halitapewa haki zao, mtandao huo utashirikiana na wadau wa elimu zikiwemo Asasi za kiraia kufungua kesi mahakamani ili kudai haki zao.

Akisoma taarifa rasmi ya wanafunzi waliosimamishwa UDOM, Gibson Johnson alisema, wanaiomba serikali kuangalia uwezekano wa wao kuendelea na masomo yao.

“Tunaiomba na kuililia serikali iangalie wale wenye division I, II na III ituache tumalizie masomo yetu, lakini watakaokuwa na ufaulu wa chini kuanzia division IV itafute namna ya kuwasaidia,” alisema Johnson.

Wamemuomba Rais Magufuli na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kuona haja ya kuwarudisha chuoni ili kumaliza masomo yao kama ilivyopangwa, kama jambo hilo likishindikana serikali ifanye mkakati wa kuwatafutia vyuo stahiki ili wamalize masomo yao.
 
Back
Top Bottom