Bluray
JF-Expert Member
- Mar 25, 2008
- 3,449
- 128
Kuhusu kuua huyu mzee hakuwa muuaji hata kidogo. Hapa tumpe haki yake kabisa. Hata wale waliostahili kuuawa yeye hakusaini wauawe. Katika uongozi wake wa zaidi ya miaka 20 nasikia alisaini wauawe watu wawili tu ( ambao hata wewe ungesahini). Ina semekana mmoja alimuua binti yake ili apate malipo ya bima.
Vile vile nakumbuka Marehemu Mohamed Babu (RIP) kusema kuwa Nyerere alimwokoa asiuawe, hivyo alikuwa anawajali hata watu wengine mzee wa watu.
Kwa upande wa kuwatandika Bakora kama ilivyoanishwa na TBC katika kipindi chake Mimi siungi mkono kabisa, nafikiri hapa alipotoka. Mwanzoni nilifikiri ni porojo kumbe wapi.Hii inaonyesha ni jinsi gani akishaona jambo lina manufaa,.alikuwa anajituma kupita kiasi kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa.
Kwa ujumla mzee huyu alikuwa na nia nzuri kabisa karibu katika kila move aliyoianzisha mfano JKT, vijiji vya Ujamaa n.k. Lakini katika kila jambo kuna uzuri na ubaya wake. Kwa vijiji vya ujamaa ukitembelea vijiji vya nchi nyingine kama Kenya na Uganda ndipo utajua uzuri wa wazo lile. Huku kwetu kuna mpango angalau lkn kwa wenzetu ni tofauti kabisa.
Tukirudi nyuma kuna mtu kaongelea porojo juu ya viongozi wetu wakuu, hasa Mwl. Na mzee Kawawa kweli kwa watanzania Documentation ni sifuri. Mambo mengi ya uongo yanasemwa, kwa kuwa hakuna anaye yakanusha yanaonekana ya kweli wakati sivyo.
Mwisho mjadala huu ulianzishwa kwa nia ya kupata mawazo ya watu juu ya mambo yaliyojiri siku za nyuma, Hii itatusaidia wakati mwingine tukipewa nafasi tujue jinsi ya kukabiliana na changamoto mbali mbali katika utendaji kazi.
Majina yaliyotumika mwanzoni BMW na JKN ni ya kusadikika tu kwa nia ya kuanzisha mjadala na kichwa cha habari kwa nia hiyo hiyo pia.
Tatizo standards zetu lax za kiafrika tunataka kuua rais mpaka aamrishe majeshi kama alivyoamrisha Ben Mkapa Jan 17 visiwani, au achinje kinyama kama Iddi Amin.
The "Great Leap Forward" na "Cultural Revolution" (tulipokopi Siasa ni Kilimo na mambo mengi ya Azimio la Arusha) the two Maoist initiatives killed millions in China, and Mao is held responsible even though he may not have ordered soldiers to kill people directly. Ukiendesha villagization bila ya kufanya a small pilot na kuona effects vizuri halafu watu wakafa kutokana na bad policy and implementation hujaua?
Tuache kuwa na lax standards, hizi ndizo zinatusababisha tubaki kwenye umaskini day in day out.