Nyati
JF-Expert Member
- Mar 6, 2009
- 2,489
- 1,814
Wakuu,
Kumekuwepo na tetesi za muda mrefu kuwa wakati wa Mwalimu kuna watu waliitwa Ikulu wakatandikwa viboko baada ya kuenda kinyume na taratibu. Jana nilihakikisha hilo wakati wa kipindi cha Mwanzo Mwisho - TBC1. Tetesi zilieleza kuwa baada ya kuamuriwa kuwa watu waende JKT. Vijana wa Chuo Kikuu walianzisha kile wanachokiita KUNJI i.e MGOMO. Basi Maofisa usalama wa Taifa wakawaongopea viongozi wao kuwa Mwl. kawaandalia Ubwabwa wa nazi Ikulu. Nao bila kushtukia mtego uchwara huo wakapanda magari kwenda Ikulu. Kufika huko wakaambulia BAKORA sita matakoni badala ya UBWABWA. Na kusimamishwa chuo pia. Watu walihabarisha pia kuwa baada ya watu hao kupata madaraka wali-livenji kwa kuiua JKT.
Watu wengi wamekuwa wanatoa majina ya waliocharazwa ambayo yamekuwa yanatofautiana mara kwa mara. Hivyo kama wewe wawafahamu waliocharazwa na aliyekuwa anawacharaza tupe majina