Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,102
- 53,360
- Thread starter
- #81
Moja, ni familia yangu hapa. Pili sipati "peace of mind" Bongo . (hali ya siasa ni ya ukandamizi wa wananchi, uoneaji kwa wapinzani wa serikali, kutokuwa na mahakama huru). Napata uchungu sana kuona wananchi wanapasuliwa vichwa na FFU hata wakijisalimisha. Siku Watanzania wakiweza kuandamana bila ya kupigwa mabomu wala kupasuliwa vichwa, pengine nitawaza kurudi.
Tatu, binafsi, quality matters more than quantity. Kuna mchangiaji aliandika nyuma kuhusu tiba. Kuwa na tiba bora ni muhimu kuliko bilioni mia katika benki yangu. Mwisho, napenda kuishi kwenye nchi iliyo na sifa za kidemokrasia.
Pengine, sababu muhimu ni kuridhika na ninachokipata hapa.
That's inspiring.
Huwa ndicho huwa najiuliza. How comes mtu ameishi nchi yenye demokrasia, uhuru wa kujieleza, elimu na afya bora, miundombinu iliyotukuka ila anaacha anarudi Tz kwenye shida za kila aina?