Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

Moja, ni familia yangu hapa. Pili sipati "peace of mind" Bongo . (hali ya siasa ni ya ukandamizi wa wananchi, uoneaji kwa wapinzani wa serikali, kutokuwa na mahakama huru). Napata uchungu sana kuona wananchi wanapasuliwa vichwa na FFU hata wakijisalimisha. Siku Watanzania wakiweza kuandamana bila ya kupigwa mabomu wala kupasuliwa vichwa, pengine nitawaza kurudi.

Tatu, binafsi, quality matters more than quantity. Kuna mchangiaji aliandika nyuma kuhusu tiba. Kuwa na tiba bora ni muhimu kuliko bilioni mia katika benki yangu. Mwisho, napenda kuishi kwenye nchi iliyo na sifa za kidemokrasia.

Pengine, sababu muhimu ni kuridhika na ninachokipata hapa.

That's inspiring.

Huwa ndicho huwa najiuliza. How comes mtu ameishi nchi yenye demokrasia, uhuru wa kujieleza, elimu na afya bora, miundombinu iliyotukuka ila anaacha anarudi Tz kwenye shida za kila aina?
 
Kwa kawaida mtanzania anapokwenda kusoma nje ya nchi au hata kufanya kazi anapaswa kufuata masharti ya scholarship aliyotunukiwa kama ni mwanafunzi au mkataba wa kazi kwa mwanataaluma ambao ameingia na huyo mwajiri wa nje ya nchi. Moja kati ya masharti muhumu ya mkataba au scholarship ni kipengere cha kurejea nyumbani baada ya kumaliza masomo au kwisha kwa mkataba wa kazi. Usimamizi wa scholarship/mkataba unafanywa na watu wa ubalozi kwa ushirikiano na wizara iliyopitisha kibali cha kwenda kufanya kazi nje ya nchi. Kwa watanzania wanaotaka kuhama kabisa nchi pia wana utaratibu wao ambao huratibiwa na ubalozi wa nchi unayotaka kuhamia,lakini pia kuna wazamiaji ambao wanaamua kwenda mpaka kwa mpaka hadi huko walikokusudia kwenda, lakini mwisho wa yote kama umekwenda nje kwa masomo au kazi,mkataba ukiisha ni lazima urudi tu au ukaombe kuongeza muda au uamue kuishi kiujanja ujanja mpaka hapo utakapopata uhalali wa kuishi nje nchi yako.
Mkuu jifunze japo kuweka paragraph kwenye uandishi wako,itapendeza zaidi kusomeka na kwa uwazi zaidi.
 
Income Kubwa Unapata Kwenye Nini? Na Fursa Ipi Unayoongelea Wewe, Ya Kujiajili Au Kuajiliwa?

Hata hao wageni wanakuja kwasababu ya mazingira ya ujanjajanja yaliyo Tanzania. Ila ukweli ni kwamba hakuna business environment inayowekwa na serikali kuwavutia wawekezaji wa ndani.
 
Kwa kawaida mtanzania anapokwenda kusoma nje ya nchi au hata kufanya kazi anapaswa kufuata masharti ya scholarship aliyotunukiwa kama ni mwanafunzi au mkataba wa kazi kwa mwanataaluma ambao ameingia na huyo mwajiri wa nje ya nchi. Moja kati ya masharti muhumu ya mkataba au scholarship ni kipengere cha kurejea nyumbani baada ya kumaliza masomo au kwisha kwa mkataba wa kazi. Usimamizi wa scholarship/mkataba unafanywa na watu wa ubalozi kwa ushirikiano na wizara iliyopitisha kibali cha kwenda kufanya kazi nje ya nchi. Kwa watanzania wanaotaka kuhama kabisa nchi pia wana utaratibu wao ambao huratibiwa na ubalozi wa nchi unayotaka kuhamia,lakini pia kuna wazamiaji ambao wanaamua kwenda mpaka kwa mpaka hadi huko walikokusudia kwenda, lakini mwisho wa yote kama umekwenda nje kwa masomo au kazi,mkataba ukiisha ni lazima urudi tu au ukaombe kuongeza muda au uamue kuishi kiujanja ujanja mpaka hapo utakapopata uhalali wa kuishi nje nchi yako.

Kuna scholarship za chuo ambazo hazina vipengele vya kurudi nyumbani. Kama umepelekwa nje kusoma na Serikali kwa kutumia msaada wa nchi tajiri (kwa mfano, unasoma udaktari Finland au UK), inabidi urudi ukimaliza masomo.

Kama umepata scholarship binafsi, haina vipengele hivyo. Muhimu ni kuishi bila ya kuvunja masharti ya sheria za uhamiaji. Kama upo USA, unaomba H1B viza (unaombewa na mwajiri), baada ya hapo, una haki ya kufanya kazi kisheria. baada ya hapo ni Green Card.

Wengine wanaoa ili wapate haki haraka, wengine wametoka familia tajiri na wanawekeza Marekani ili wapate haki ya kuishi haraka. Nadhani ulikuwa unaongelea scholarship za Kiserikali.

Unaweza kuhama kihalali kwa kutumia elimu yako, ili mradi tu kama elimu yako inahitajika na nchi husika. Huhitaji kibali cha aina yoyote. Ni elimu na fedha yako tu.
 
That's inspiring.

Huwa ndicho huwa najiuliza. How comes mtu ameishi nchi yenye demokrasia, uhuru wa kujieleza, elimu na afya bora, miundombinu iliyotukuka ila anaacha anarudi Tz kwenye shida za kila aina?

Nadhani ni kutaka kuwa karibu na wazee, kutaka fedha nyingi zaidi, kuwa na marafiki wa karibu, na kutoweza kupata maisha aliyoyategemea huko nje. Wengine, hawajazoea utamaduni wa kazi za nchi magharibi.

Marafiki zangu wote waliorudi, wanaendelea vizuri kimaisha kuliko walipokuwa nje. Nchi changa huwa ina opportunity zaidi. Tanzania, hata ukiuza chips kuku unaweza kujenga nyumba.

Kwa wengine, kusaka utajiri ni muhimu kuliko kuishi katika hali ya kidemokrasia na tiba bora. Wakikosa, wanarudi kusaka nyumbani.

Siamini kwa ajili ya Uzalendo. Uzalendo unakuja baada ya kushiba.
 
this thread potrays the mindsets of many africans,who can not think of themselves. I support Trump on this agenda to export illegals and especially Africans. Tumezidi sana kujitharau na kujizalilisha.
Mtu yuko radhi ajenge nchi za watu badala ya kuendelea kuwaeka bdii katika kazi huku nyumbani. Marekani hakuna kitu kinaitwa ameerican dream kwasasa. Kila mtu atabeba mzigo wake.
 
Hata hao wageni wanakuja kwasababu ya mazingira ya ujanjajanja yaliyo Tanzania. Ila ukweli ni kwamba hakuna business environment inayowekwa na serikali kuwavutia wawekezaji wa ndani.

Kabisa Especially Kipindi Hiki Matamko Ya Chuki Na Fitina Kibao, Na Wengi Walikuwa Kipindi Cha Nyuma Sidhani Kama Idadi Itakaa Sawa Miaka Hii 2 Ukulinganisha Na Miaka Ya Nyuma
 
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, ni ngumu sana tena sana kurudi na kuendeleza maisha hapa bongo. Mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kutimka, ila sasa uzalendo umenivaa, nimeamua kubaki tz kulitumikia taifa langu. Changamoto kubwa ni miundombinu, na kutokuwa na mgawanyo wa majira. Unakuta Europe tulizoea kipindi cha xmass kuna kurudishiwa hela za kodi, bei vitu kupungua, xmass mood, etc. Na shoping za maana. Sasa hapa bongo labda uishi dar, ila mikoani ndiyo balaa. Kikubwa kinachotuweka hapa bongo ni uzalendo!
Haha nikisikia hili neno uzalendo ama kulisoma tena ndani ya ardhi.hii ya tz hua nacheka kwa.masikitiko.
uzalendo unakufa njaa
 
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, ni ngumu sana tena sana kurudi na kuendeleza maisha hapa bongo. Mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kutimka, ila sasa uzalendo umenivaa, nimeamua kubaki tz kulitumikia taifa langu. Changamoto kubwa ni miundombinu, na kutokuwa na mgawanyo wa majira. Unakuta Europe tulizoea kipindi cha xmass kuna kurudishiwa hela za kodi, bei vitu kupungua, xmass mood, etc. Na shoping za maana. Sasa hapa bongo labda uishi dar, ila mikoani ndiyo balaa. Kikubwa kinachotuweka hapa bongo ni uzalendo!
Kwa niliyofanyiwa nchi hii neno uzalendo nilisha li flash kwenye choo
 
We huoni wageni walivyojazana Tanzania ndo ujiulize wanapapendea nini? Kama ni matatizo yapo kila sehemu hata hivyo unatakiwa utatue tatizo na si kulikimbia.
Wageni kutoka nchi gani?
Na kuna aina ngapi za wageni wanaokuja nchi hii?
 
Hayo maneno tu, sehemu ka US, EU, hakuna mwenye muda na wewe, unafit in kama vile umezaliwa huko, they can't tell kama ni foreigner kaa hawajasikia accent maana black guys kule ni wengi mno.

Ubaguzi mnaoona kwenye media upo ila sio kama mnavyohisi, nimekaa nje miaka mingi na sijawahi baguliwa hata mara moja, na mimi ni mtu ambaye nakaa na watu weupe daily. Mambo sio mabaya kiasi hicho. Ukiheshimu watu watakuheshimu most of the time.
Bora umesema ukweli
 
Home ni home tu ndugu yangu. Mara nyingi wanasema moyo wa binadamu hauriziki. Utakaa nje unapata ulichokuwa unatafuta, kama ni pesa unapata, then what? At last you realize home ndo kila kitu.

Kama uliondoka bongo kwa amani kabisa,, hujakimbikia kitu, ameacha ndugu na marafiki utarudi tu.
 
Aisee yaani sisi Watanzania sijui tukoje kwenye maisha ukijishusha unategemea mgeni aje afanyaje??,,
Yaani wewe unaanza kulinganisha Tanzania Na USA-UK, Mataifa enye kalne na kalne, sisi tuna rais wa 5, Marekan wana Rais wa 45, Hapi na Wapi??

Kipindi cha utawala wa Mh. Jk sisi hawahawa Wa Tz kutwaa Ooh Rais Gani wa kucheka cheka tu,,

Ameingia Jembe oooh Rais Gaidi Mala likali sasa wewe ufanyiwe nini!!!

Serikali ilisha legeza mashaariti ya kutoa pass ya kusafilia International, sasa inakuwaje mtu anaanza kuomba ushauri wa kwenda kuishi njee au kuomba ushauri kwa watanzania wanao ipenda nchi yao wamerudi na ku invest kwenye nchi yao!!

MH. Rais aendelee kuweka sawa tunamuombea,,
Ajili za mavi hizi
 
Dunia ya leo, huwezi kukaa nchi moja kutafuta maisha bora.

Kuna watu wanazama baharini kujaribu kuingia nchi za Ulaya kutafuta maisha bora. Na hapo hapo kuna maelfu ya raia wa nchi hizo hizo wanaondoka kwenda kuishi Asia kila mwaka.

Thailand, Singapore, Indonesia au Malaysia imejaa raia wa Ulaya wanafanya kazi.

Hao wageni Bongo wameona opportunity wazawa hawazioni kama Wazungu wanaoishi Asia. Huku Asia, dogo aliyemaliza chuo mwezi huu anaweza kupewa kazi ya kufundisha watoto kwa mshahara wa $3000 kwa mwezi. Mshahara huu hawezi kupata kwao hata kama ni Mmarekani au hata Muiingereza. Angepata asingekuja huku kutafuta. Waiingereza wenyewe wanaomba nchi yao ikubali maombi ya Australia ya kuruhusiwa raia wao kufanya kazi bila ya viza ili wahame huko. Wanasema ni bora kuwaruhusu Australia kuliko Waromania au Wabulgaria wasiojua Kiingereza.

Kwa maoni yangu, kutafuta maisha hayana Uzalendo. Tumbo kwanza. Sina subira.
Hahaha umeongea kweli mkuu ..ndo mana hua simuelewi mtu anayeongea neno uzalendo..simuelewi kabisaa..
 
Mi binafsi , home Tz my land ni pazuri sana aisee,
Sema labda kama unataka kuwa mjanja mjanja utapaona Tz kuwa pabaya. Niko nje ila mara nyingi sana na mara zote napamiss home.

Kwa ujumla fahari nikuwa na projects zako home Tz, kwani huku nje kila mtu anazo projects na hela, hivyo wakuulizeni home kwenu vipi watekeleza project zepi sasa hapo lazima jibu uwe.nalo kama.hauna hapa home wachekwa.na kuonekana ovyo kabisa.

Kwa hiyo, hapa nyumbani ndiyo kila kitu ukiwa nje.
 
Wengine wamekosa ujanja wa kuishi nje.

Wengine wana nafasi kubwa ya kupiga mingo kubwa Tanzania kuliko nje (kwa familia yenye connections Tanzania mtu anaweza kufanya biashara kubwa na kupata maendeleo makubwa Tanzania kuliko nje, ingawa umeme wa TANESCO utakuwa unakatika kama kibatari kilichokosa mafuta na standard of living ya manati)

Kuna wengine wazalendo.

Wengine wana majukumu ya kifamilia.

Wengine wana ngiri hawawezi kuishi kwenye baridi.

Wengine ni lazima wawe katikati ya wabongo, kuishi mbali na nyumbani wanaona karaha.

Wengine wana ndoto za kuongoza nchi.

Ila mimi tangu naondoka bongo nilikuwa nishaamua kuwa naondoka kimoja, kama kurudi ni likizo tu.
 
Back
Top Bottom