Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

1. Shida Siyo Binafsi Tu Kuna Shida Za Nchi Ambazo Mtu Binafsi Huwezi Kuzitatua, Unataka Kuniambia Huduma Za Afya Za Ulaya Unafanisha Na Bongo, Kama Una Watoto Unataka Kuniambia Elimu Ya Bongo Unafananisha Na Ulaya, Hali Ya Hewa Na Magonjwa Ya Milipuko Unafanisha Na Bongo Kweli?

3. Hapo Umedanganya Sababu Kubwa Ya Upambanaji Wako Ulaya Unakutaka Kufata Sheria Na Nyumbani Hilo Halipo Hivyo Usiseme Mara 100 Hata Kidogo Hata Bongo Ukipambana Kwa Kufata Sheria Ni Kama Ulaya Tu.

4. Ukiwa Na Fursa Hakuna Home sickness Mkuu

5. Fursa ziko Popote Ndugu Yangu Ni Jinsi Gani Ulivyojipanga Basi, Cha Muhimu Ni Kuangalia Basics Needs Za Mwanadamu Kwenye Fursa Ndiyo Muhimu
1.Sijafananisha afya na elimu ya ulaya na tz....hilo unalisema wewe.
2.Nimedanganya?! Unanifahamu wewe au unaongea tu?!
3.Una matatizo ya kuelewa? Home sickness nimekwambia wakati niko Ulaya sijawahi kupata huo 'ugonjwa' kwasababu nilikuwa na uwezo wa kurudi anytime i want.
4.Kama wewe unaona Ulaya kuna fursa kuliko Tz baki, mimi nimemjibu alieuliza kwanini mtu anaamua kurudi.
 
Siri ya kuishi nje ni hii: nenda kasome ikiwezekana mpaka hata PhD pata kazi yako nzuri work hard na hakuna atakayekusumbua. Bongo ni kuzuri sana mpaka siku ukipata medical emergency kama heart attack, stroke, kansa ...halafu uwe huna hela za kwenda India. Aisee unakufa ka mnyama. Niliwahi kusoma Boston USA kwa miaka 7 na yes kuna mambo mazuri na mabaya kila sehemu. Miaka 7 yangu sikuwahi kubaguliwa wala kutendewa vibaya na polisi na ukiwa serious hakuna atakayekugusa. Huduma za afya kwangu hasa ndo jambo linalonikera hapa Bongo. Mtu unapata medical emergency hakuna cha ambulance, helicopter wala paramedics. Mijitu inajazana kupiga soga na kukuibia if possible. Yaani unaweza kufia pembeni mwaka barabara ka mnyama. Hata hospitali huko nako mambo yale yale tu...
 
We huoni wageni walivyojazana Tanzania ndo ujiulize wanapapendea nini? Kama ni matatizo yapo kila sehemu hata hivyo unatakiwa utatue tatizo na si kulikimbia.

Na wewe umefanikiwa kuona fursa zipi kama hao wageni?

Ushawahi hata kuwaza kumiliki mgodi? Lakini wachina wanakuja ndani ya miaka miwili tayari wanamiliki migodi.

Fursa za Tanzania ni kwa ajili ya wageni na sio wananchi.

Jaribu kujenga kiwanda uone..
 
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, ni ngumu sana tena sana kurudi na kuendeleza maisha hapa bongo. Mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kutimka, ila sasa uzalendo umenivaa, nimeamua kubaki tz kulitumikia taifa langu. Changamoto kubwa ni miundombinu, na kutokuwa na mgawanyo wa majira. Unakuta Europe tulizoea kipindi cha xmass kuna kurudishiwa hela za kodi, bei vitu kupungua, xmass mood, etc. Na shoping za maana. Sasa hapa bongo labda uishi dar, ila mikoani ndiyo balaa. Kikubwa kinachotuweka hapa bongo ni uzalendo!

Unachokiona ni kama mimi..

Mambo mengi tanzania yanakera sana.
 
From horse's mouth....
5.Fursa Tanzania:Hii ndio sababu kuu hata wewe kama uko huko ukiona fursa Tz usiiache maanake wazungu wanawaacha huko wao wanakuja huku na briefcase tu wanarudi na mamilion ya $$.

Hapan unadanganya.

Ushawaza kujilinganisha na mgeni kwenye kumata fursa Tz?

Jaribu kufanya kile mgeni anafanya uone nani atapewa kipaumbele zaidi..
 
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, ni ngumu sana tena sana kurudi na kuendeleza maisha hapa bongo. Mimi mwenyewe nilikuwa na mpango wa kutimka, ila sasa uzalendo umenivaa, nimeamua kubaki tz kulitumikia taifa langu. Changamoto kubwa ni miundombinu, na kutokuwa na mgawanyo wa majira. Unakuta Europe tulizoea kipindi cha xmass kuna kurudishiwa hela za kodi, bei vitu kupungua, xmass mood, etc. Na shoping za maana. Sasa hapa bongo labda uishi dar, ila mikoani ndiyo balaa. Kikubwa kinachotuweka hapa bongo ni uzalendo!

Unachokiona ni kama mimi..

Mambo mengi tanzania yanakera sana.
 
Maisha Popote Tu, Ni Jinsi Utakavyojipanga Na Wengi Husema Maisha Ya Ulaya Magumu

Ni Kweli Magumu Kama Huna Mipango Ila Ukiwa Nayo Ulaya Au USA Safi Kabisa.

Uzuri Wa Ulaya Ni Mambo Makuu Matatu; Elimu Hususani Ukiwa Na Watoto, Huduma Za Afya Na Usalama.
tuko tunaendelea kupambana "positive vibrated" nje. maisha ni kuchagua.
 
Nyumbani ni nyumbani hata ikiwa pangoni.

Wewe unaona hapa shida wenzako tunaona raha kurudi nyumbani na mambo swaafi kabisa.

Kama kuna Watanzania walioishi nje ya Tanzania na kurudi kuishi nyumbani basi kwenye hiyo list ntakuwemo.

Niliondoka Tanzania mwaka 1974 na kwenda kuishi nje ya Tanzania kwa miaka mingi sana kabla sijarudi tena kwa ziara za mara kwa mara na mwishowe kurudi kabisa na huko nje sasa nnakwenda kwa ziara tu ingawa nna makazi yangu huko pia.

Na kuna Watanzania nnawafahamu hawajarudi kabisa na wapo niliowakuta huko nje na wapo walionikuta na wala hawana hamu hata ya kuja kutembea.

Maisha popote.
@?Tangazo mahsusi :Leo umekula like yangu ya kwanza.
 
Mkuu Watanzania ndo tunapenda sana nyumbani ila Wanaijeria, waghana, wavenezuela, waarabu (Pakstan, Iran, Iraq), East Africa yote kasoro Tanzania hawarudi nchini.

Nadhani tuna uoga wa kuishi mbali na nyumbani na nyumbani kuna fursa nyingi sana na uhuru pia
 
Siri ya kuishi nje ni hii: nenda kasome ikiwezekana mpaka hata PhD pata kazi yako nzuri work hard na hakuna atakayekusumbua. Bongo ni kuzuri sana mpaka siku ukipata medical emergency kama heart attack, stroke, kansa ...halafu uwe huna hela za kwenda India. Aisee unakufa ka mnyama. Niliwahi kusoma Boston USA kwa miaka 7 na yes kuna mambo mazuri na mabaya kila sehemu. Miaka 7 yangu sikuwahi kubaguliwa wala kutendewa vibaya na polisi na ukiwa serious hakuna atakayekugusa. Huduma za afya kwangu hasa ndo jambo linalonikera hapa Bongo. Mtu unapata medical emergency hakuna cha ambulance, helicopter wala paramedics. Mijitu inajazana kupiga soga na kukuibia if possible. Yaani unaweza kufia pembeni mwaka barabara ka mnyama. Hata hospitali huko nako mambo yale yale tu...

Hiyo ndo concern yangu kubwa.

Umeishi sehemu yenye huduma bora, unapaacha then unarudi Tz wenye huduma za hovyo hivi?
 
Mkuu Watanzania ndo tunapenda sana nyumbani ila Wanaijeria, waghana, wavenezuela, waarabu (Pakstan, Iran, Iraq), East Africa yote kasoro Tanzania hawarudi nchini.

Nadhani tuna uoga wa kuishi mbali na nyumbani na nyumbani kuna fursa nyingi sana na uhuru pia
Nadhani tuna uoga wa kuishi mbali na nyumbani na nyumbani kuna fursa nyingi sana na uhuru pia

Inawezekana mkuu.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom