Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

Hapan unadanganya.

Ushawaza kujilinganisha na mgeni kwenye kumata fursa Tz?

Jaribu kufanya kile mgeni anafanya uone nani atapewa kipaumbele zaidi..
Nadanganya?! Nadhani unataka niseme unachotaka kusikia wewe.

Kwani wewe umeuliza kushindana fursa mimi na mgeni au kwanini nimeamua kurudi?

Nimeamua kurudi kwasababu nimmeona TZ kwangu mimi kuna fursa kuliko Ulaya. Kama wewe unaogopa wageni kaa tu huko uliko,maisha popote.
 
1.Sijafananisha afya na elimu ya ulaya na tz....hilo unalisema wewe.
2.Nimedanganya?! Unanifahamu wewe au unaongea tu?!
3.Una matatizo ya kuelewa? Home sickness nimekwambia wakati niko Ulaya sijawahi kupata huo 'ugonjwa' kwasababu nilikuwa na uwezo wa kurudi anytime i want.
4.Kama wewe unaona Ulaya kuna fursa kuliko Tz baki, mimi nimemjibu alieuliza kwanini mtu anaamua kurudi.

Mkuu Inawezekana Kabisa Uelewa Wangu Unamatatizo Lakini Ningependa Kukurudisha Jinsi Ulivyomjibu Bavaria Kwamba Inawezekana Kurudi:

1: Courage Ya Kurudi: Ukaifanunulia Kwanza Ni Malengo Na Nia Uliyoondokea, Ukasema Wewe Malengo Yako Ulikuwa Urudi Ni Sawa Kabisa, Tatu Ukasisitiza Kama Ni Shida Zilikuondoa Basi Mpaka Upake Uhakika Wa Kuwa Zimeisha Ndiyo Unarudi. Ndiyo Maana Nilikujibu Shida Si Binafsi Tu Kuna Shida Za Kitaifa.
Hakuna Aliyekuja Duniani Kuteseka Kila Mtu Anataka Maisha Maisha Mazuri Ila Maisha Mazuri Bila Huduma Bora Siyahafiki.

2. La Uzalendo Sijalisemea Chochote Sababu Unaweza Kuwa Hata Urusi Na Bado Ukawa Mzalendo Wa Taifa Lako.

3.Ukaandika Wengine Wanaweza Kurudi Sababu Wameshindwa Kupambana. Ukasema Umepambana Vya Kutosha Na Ukajiridhisha Mapmbano Yale Ukiyaleta Tanzania Utafanikiwa Mara 100 Na Ndiyo Kinachotokea. Hapo Ndipo Nilisema Unadanganya Na Unless Upambanaji Unaouzungumzia Uwe Wa Kukwepa Kodi, Lakini Kama Ulikuwa Umeanzisha Biashara/Ajira Hata Siku Moja Uwezi Fananisha Turnover Ya Biashara Ya Bongo Na Ulaya/USA "Like To Like" Yeyote Ile Hata Ya Kinyozi Halafu Bongo Upate 100 times.
Na Kwahili Sihitaji Kukujua Ili Niamini Sababu Mimi Nilishafanya Kazi Nchi Za Ulaya Na Nikafanya Biashara Huko Na Pia Hapa Bongo Na Biashara Lakini Huwezi Sema 100 times.

4. Ukasema Unaweza Kurudi Kwa Home sickness Jibu Langu Lilikuwa Linasupport Hoja Yako Kuwa Ukiwa Na Fursa Hiyo Inakuwa Hamna.

5.Ukasema Fursa Ndiyo Inayowezesha Mtu Kurudi Na Nikajibu Fursa Iko Popote Tu Na Ni Jinsi Gani Ulivyojipanga, Cha Muhimu Ni Kuangalia Basics Needs Za Mwanadamu Kwenye Fursa Ndiyo Muhimu.
Nilijibu Hivyo Sababu Wewe Ulimaanisha Fursa Zipo Tanzania Tu Ndiyo Maana Hata Wazungu Wanakuja Tanzania. Huku Ulaya Pia Kuna Fursa Nyingi Na Watu Wanapata Mamilioni Kama Ukibadili Kwa Pesa Za Madafu. Na Siajasema Mahali Popote Kuwa Ulaya Kuna Fursa Kuliko Tz Nimesema Fursa Ipo Popote Tu.
 
Watanzania tuna bahati sana, raia wa nchi nyingine wanaogopa kurudi nyumbani kwa sababu ya civil war, uchumi na mambo mengine.

Sky,
Kumbuka daima, War and political instability is very good for business.

Somalia wanasafirisha MBUZI Saudi Arabia wenye thamani ya $350 MILLION kila mwaka japo wapo vitani.

South Sudan wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya biashara. Nchi changa inahitaji kununua kila kitu, Rais wao kawaweka ndugu zake katika kila kona ya uchumi na hataki kugawa keki ya taifa kwa kabila nyingine.

Na raia wanarudi sana nchi za vita kutafuta madaraka na biashara. Karibu viongozi wote Somalia wana uraia wa nchi za magharibi. Hata Sudan ya Kusini, wale LOST BOYS wanarudi kila siku, kutafuta kazi serikalini kwa kutumia elimu yao waliopewa bure na serikali ya Marekani. Kabila ya Kiir wote wamepewa kazi nyeti.

Wewe ukiona uchumi mbaya na vita, mwenzako anaona uchumi mkubwa wa kuuza silaha na kununua madini kwa bei ya kutupa. Mbali ya kuwauzia chakula, madawa, magodoro na tent kwa bei maradufu akina UNICEF na UNHCR.
 
Sky,
Kumbuka daima, War and political stability is very good for business.

Somalia wanasafirisha MBUZI Saudi Arabia wenye thamani ya $350 MILLION kila mwaka japo wapo vitani.

South Sudan wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya biashara. Nchi changa inahitaji kununua kila kitu, Rais wao kawaweka ndugu zake katika kila kona ya uchumi na hataki kugawa keki ya taifa kwa kabila nyingine.

Na raia wanarudi sana nchi za vita kutafuta madaraka na biashara. Karibu viongozi wote Somalia wana uraia wa nchi za magharibi. Hata Sudan ya Kusini, wale LOST BOYS wanarudi kila siku, kutafuta kazi serikalini kwa kutumia elimu yao waliopewa bure na serikali ya Marekani. Kabila ya Kiir wote wamepewa kazi nyeti.

Wewe ukiona uchumi mbaya na vita, mwenzako anaona uchumi mkubwa wa kuuza silaha na kununua madini kwa bei ya kutupa. Mbali ya kuwauzia chakula madawa, magodoro na tent kwa bei maradufu akina UNICEF na UNHCR.
I meant that, since we had never experienced civil war and internal conflicts, we are not aggressive enough to fight for life in foreign countries. I met Nigerians who are fighting tooth and nail to bring the whole family in western countries. The minute a husband or wife get a student visa, that is all they need and rest will be resolved as they go.
 
Kama hutojali.

Unaweza niambia sababu zipi zinakufanya usirudi?

Moja, ni familia yangu hapa. Pili sipati "peace of mind" Bongo . (hali ya siasa ni ya ukandamizi wa wananchi, uoneaji kwa wapinzani wa serikali, kutokuwa na mahakama huru). Napata uchungu sana kuona wananchi wanapasuliwa vichwa na FFU hata wakijisalimisha. Siku Watanzania wakiweza kuandamana bila ya kupigwa mabomu wala kupasuliwa vichwa, pengine nitawaza kurudi.

Tatu, binafsi, quality matters more than quantity. Kuna mchangiaji aliandika nyuma kuhusu tiba. Kuwa na tiba bora ni muhimu kuliko bilioni mia katika benki yangu. Mwisho, napenda kuishi kwenye nchi iliyo na sifa za kidemokrasia.

Pengine, sababu muhimu ni kuridhika na ninachokipata hapa.
 
Kila mtu anauhuru wa kwenda kuishi na haya hua yanakuja kama baado hujawa na familia yaani mke watoto, ila Tz ni nchi pekee duniani enye raha,
Ukisema mpinza anabaguliwa, ulitaka kiwe na serikali ngapi?? ,,,

Mpinzani ndo maana akaitwa mpinzani--mpinzani hata kama kitu kizuri yeye ni kukosoa na kupinga,, yeye kwake zuri hakuna..
 
I meant that, since we had never experienced civil war and internal conflicts, we are not aggressive enough to fight for life in foreign countries. I met Nigerians who are fighting tooth and nail to bring the whole family in western countries. The minute a husband or wife get a student visa, that is all they need and rest will be resolved as they go.

I think it's cultural and lack of proper education. Wanigeria wapo wengi na wana elimu bora. Maisha huko ni magumu bila elimu na kazi hanma za kutosha. Wanasafiri ili watafute maisha. Ditto with the Indians.

Tanzania, watu wanaridhika haraka. Dunia tumeijua juzi juzi. Kumbuka, mpaka 1980, tulikuwa haturuhusiwi kusafiri kirahisi. Dollar was illegal, etc. Wenzetu wameanza kusafiri zamani na leo wana ndugu kila kona ya dunia. They know how the world operates. Watanzania wengi ni Xenophobic. Marekani ni ubongo wa dunia (innovation center) kwa sababu ya akili za wageni kama kina Einstein. Australia na Kanada wanawakaribisha wageni ili walete maarifa zaidi ya kujenga uchumi wao.
 
nimeomba Max na Mike watufungulie subform yetu sisi wana Diaspora

mimi to be honest nishamake up my mind kuwa Tanzania is not for me

niliondoka baada ya kumaliza form 6 na nimekaa nje miaka karibuni 19 na nimejaribu kurudi bongo kwa visingizio vya uzalendo, quality of life, ku invest na mwishowe nimeona sipawezi. Mimi DNA yangu ni ki marekani marekani tuuu and Africa isn't for me kuishi or otherwise.

Hapa nilipo nauza assets zangu za Tanzania zote japo soko lililopo ni buyers market lakini I've had enough cash nitakayopata si chini ya milioni 500 sasa hizo naamini hizo naweza kuinvest huku kwa kuwa na shares walau Netflix,GSK, Google, BP, na Facebook to name a few

To be honest mambo yanaoyonifanya niondokane na wazimu wa bongo ni kuwa I have nothing in common na Tanzania let alone familia yangu mwenyewe mbaya zaidi the way nchi inavyoendeshwa haingii akilini. Tazama yaliyomkuta Matarajio wa TPDC na wengineo

Kuta holiday ni mtihani tuu hapa nilipo wife anataka nije naye huko mwezi ujao for 1 month naona naadhibiwa tuuu maana mwishowe ndugu au jamaa au mediocrity kwenye kila kitu kitanichefua roho yangu na mimi all I want is peace of mind.

I don't mind kuja hapo for 1 week lakini mwezi mwima I think I will go mental....

Pia kitu kingpin mimi siwezi mambo ya kupiga maggot na kuabudu miungu watu wa hapo (kwenye mambo ya kazi, basher na kijamii).

Huku mimi kazi yangu ni kwenye financial sector na Investment Banking to be precise.

ZAIDI NITARUDI BAADAE.
 
I think it's cultural and lack of proper education. Wanigeria wapo wengi na wanna elimu bora. Maisha huko ni magumu bila elimu na kazi hanma za kutosha. Wanasafiri ili watafute maisha. Ditto with the Indians.

Tanzania, watu wanaridhika haraka. Dunia tumeijua juzi juzi. Kumbuka, mpaka 1980, tulikuwa haturuhusiwi kusafiri kirahisi. Dollar was illegal, etc. Wenzetu wameanza kusafiri zamani na leo wana ndugu kila kona ya dunia. They know how the world operates. Watanzania wengi ni Xenophobic. Marekani ni ubongo wa dunia (innovation center) kwa sababu ya akili za wageni kama kina Einstein. Australia na Kanada wanawakaribisha wageni ili walete maarifa zaidi ya kujenga uchumi wao.
Like wise, lack of exposure is making us not to make a use of our potentials. If they say agriculture is still our economy back bone, still the majority of supermarkets are owned by foreigners and sell foreign products.

Wanigeria waliana kutoka siku nyingi sana, unakuta wako lawyers ambao wanasaidia wengine, doctors and career nyingine ughaibuni. Sisi bado hata tukitoka tunabeba mabox.
 
I think it's cultural and lack of proper education. Wanigeria wapo wengi na wanna elimu bora. Maisha huko ni magumu bila elimu na kazi hanma za kutosha. Wanasafiri ili watafute maisha. Ditto with the Indians.

Tanzania, watu wanaridhika haraka. Dunia tumeijua juzi juzi. Kumbuka, mpaka 1980, tulikuwa haturuhusiwi kusafiri kirahisi. Dollar was illegal, etc. Wenzetu wameanza kusafiri zamani na leo wana ndugu kila kona ya dunia. They know how the world operates. Watanzania wengi ni Xenophobic. Marekani ni ubongo wa dunia (innovation center) kwa sababu ya akili za wageni kama kina Einstein. Australia na Kanada wanawakaribisha wageni ili walete maarifa zaidi ya kujenga uchumi wao.
Aisee yaani sisi Watanzania sijui tukoje kwenye maisha ukijishusha unategemea mgeni aje afanyaje??,,
Yaani wewe unaanza kulinganisha Tanzania Na USA-UK, Mataifa enye kalne na kalne, sisi tuna rais wa 5, Marekan wana Rais wa 45, Hapi na Wapi??

Kipindi cha utawala wa Mh. Jk sisi hawahawa Wa Tz kutwaa Ooh Rais Gani wa kucheka cheka tu,,

Ameingia Jembe oooh Rais Gaidi Mala likali sasa wewe ufanyiwe nini!!!

Serikali ilisha legeza mashaariti ya kutoa pass ya kusafilia International, sasa inakuwaje mtu anaanza kuomba ushauri wa kwenda kuishi njee au kuomba ushauri kwa watanzania wanao ipenda nchi yao wamerudi na ku invest kwenye nchi yao!!

MH. Rais aendelee kuweka sawa tunamuombea,,
 
Kila mtu anauhuru wa kwenda kuishi na haya hua yanakuja kama baado hujawa na familia yaani mke watoto, ila Tz ni nchi pekee duniani enye raha,
Ukisema mpinza anabaguliwa, ulitaka kiwe na serikali ngapi?? ,,,

Mpinzani ndo maana akaitwa mpinzani--mpinzani hata kama kitu kizuri yeye ni kukosoa na kupinga,, yeye kwake zuri hakuna..

issue hapa ni quality of life.

Subiri pesa ziishe kisha uumwe au take kufanya dialysis na utaniambia hizo lake 5 per session zitatoka wapi
 
Kwa kawaida mtanzania anapokwenda kusoma nje ya nchi au hata kufanya kazi anapaswa kufuata masharti ya scholarship aliyotunukiwa kama ni mwanafunzi au mkataba wa kazi kwa mwanataaluma ambao ameingia na huyo mwajiri wa nje ya nchi. Moja kati ya masharti muhimu ya mkataba au scholarship ni kipengere cha kurejea nyumbani baada ya kumaliza masomo au kwisha kwa mkataba wa kazi. Usimamizi wa scholarship/mkataba unafanywa na watu wa ubalozi kwa ushirikiano na wizara iliyopitisha kibali cha kwenda kufanya kazi nje ya nchi. Kwa watanzania wanaotaka kuhama kabisa nchi pia wana utaratibu wao ambao huratibiwa na ubalozi wa nchi unayotaka kuhamia,lakini pia kuna wazamiaji ambao wanaamua kwenda mpaka kwa mpaka hadi huko walikokusudia kwenda, lakini mwisho wa yote kama umekwenda nje kwa masomo au kazi,mkataba ukiisha ni lazima urudi tu au ukaombe kuongeza muda au uamue kuishi kiujanja ujanja mpaka hapo utakapopata uhalali wa kuishi nje nchi ya yako.
 
Aisee yaani sisi Watanzania sijui tukoje kwenye maisha ukijishusha unategemea mgeni aje afanyaje??,,
Yaani wewe unaanza kulinganisha Tanzania Na USA-UK, Mataifa enye kalne na kalne, sisi tuna rais wa 5, Marekan wana Rais wa 45, Hapi na Wapi??

Kipindi cha utawala wa Mh. Jk sisi hawahawa Wa Tz kutwaa Ooh Rais Gani wa kucheka cheka tu,,

Ameingia Jembe oooh Rais Gaidi Mala likali sasa wewe ufanyiwe nini!!!

Serikali ilisha legeza mashaariti ya kutoa pass ya kusafilia International, sasa inakuwaje mtu anaanza kuomba ushauri wa kwenda kuishi njee au kuomba ushauri kwa watanzania wanao ipenda nchi yao wamerudi na ku invest kwenye nchi yao!!

MH. Rais aendelee kuweka sawa tunamuombea,,

Soma ulichokiandika tena. You make no sense. Tulia ili upange mawazo yako vizuri.
 
Life is not supposed to be lived in one place,
Travel as much and as far as you can
Go places and see things different,

Huwezi kuishi sehemu moja tu kama mti,kutoka nje na kwenda nchi zingine kunafungua akili zaidi kwani unakutana na new "challenges"

Ukiishi sehemu moja tu na akili nayo itawaza kua hakuna maisha mengine zaidi ya hayo unayoishi tu!

Anyway naona zile thread za kuponda wabeba box zimegeuka na kuwataka wabeba box wasirudi bongo!! Vipi mleta mada mambo magumu Mkuu?
 
Back
Top Bottom