Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

mkisi program tulianza nayo sisi mwaka 2003,,ahaaaa ilikuwa balaaaa usipokuwa na counter book na past paper za kutosha
 
afande orando mazafanta...alikua ananyanganya sana simu na ipods kwa wanafunzi wa hosteli,
 
miaka hii mitatu kati ya 2010-2013 shule kama imekufa vile, wale walimu wazoefu wa zaidi ya miaka 10 wote wameondoka, wengine ukikaribia kumaliza kamkataba kako unaambiwa ahsante endelea na maisha mengine.....

Mkuu kabanga ni kweli mkuu shule sio kabisa siku hizi sio ile ya akina Wajadi naMassawe ambao waliiweka juu sana shule
Wakati wa ugomvi wa Jiteute naTambaza wakati huo Tambaza bado ikiwa na olevel uliopelekea nafikiri ni konda mmoja kufa mitaa ya Keko kweli Jiteute ilikuwa shule enzi hizo

Hahahahaa....mkuu we kweli wa kale. Jite ya siku hizi nidhamu hakuna kabisa!!!

Mkuu Kulya tulipita pale wakati ndio kwanza hostel inaanza anza wakati bado Massawe akiwa pale kama Headmaster na akina Bwenge na Wajadi wakiwa pale na akina Mama Lyimo na Mama Mnzava
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu mosha katufundisha bookkeeping bila kumsahau jamaa mmoja alikuwa jkt kipindi kile alikuwa wanajitolea kutufundisha somo LA siasa anaitwa wandwe
 
afande orando mazafanta...alikua ananyanganya sana simu na ipods kwa wanafunzi wa hosteli,

Kama sikosei kuna mmoja white hivi eeehh!!! Ila nadhani ni cha mtoto kuna jamaa mmoja alikuja ila hakukaa sana huyu alukuwa anaitwa Teja huyu jamaa kwanza alikuwa na mwili mdogo mdogo alikuwa anavizia wanafunzi wakitoka prepo naye anakuja akiwa amevaa T-shirt ya ya Hostel na kaunta lake la lokoo basi akiwa zamu alikuwa hakosi angalau simu moja kwa siku Jamaa alikuja kufukuzwa baadae baada ya kutorosha mwanafunzi na kukaa naye gheto kwa siku tatu
 
Kuna huyu afande huwa anajifanya mbabe sana anaitwa Kajimara ukizinguana naye anakutishi kukuwekea bangi sijui bado yupo?

Huyu afande alikuwa na sauti yake ya bangi bangi...

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Nakumbuka mabweni ya wavulana waliokuwa wanakaaa hostel Mwakyambiki,Makame... Nakumbuka pia usafi wa jumamosi mnamwagia maji ardhi afu mnafagia na kutandika saaafi unapanga plate,kijiko na kikombe kwa ajili ya ukaguzi...

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Nawakumbuka kina Bruno,Bichizi, ilikuwa ukitaka kutoka mapema Bichizi anabeba Begi hadi studio pale nje,halafu smart area unapita mbio. Ila maafande wakikudaka nae anakukana. Nilisoma pale 1999 - 2001

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Mwaka 2007 nikiwa ukingoni kumaliza A level, nakumbuka kipindi nikizurura nje wakati wenzangu wakiwa ktk mkisi program, nilikutana na Major Mkisi, kipindi hicho mwenyewe akijiita major msomi, major handsome, alinikamata na kunipa adhabu ya kijeshi. Lakini sasa hivi Mkisi kwisha habari yake. Major Kessy ndio mkuu wa sasa hivi pale Jiteute!
 
teja nakumbuka alikua amepewa bweni la form 1 ndo awasimamie..jamaa alikua kama tea kweli
 
Nakumbuka mabweni ya wavulana waliokuwa wanakaaa hostel Mwakyambiki,Makame... Nakumbuka pia usafi wa jumamosi mnamwagia maji ardhi afu mnafagia na kutandika saaafi unapanga plate,kijiko na kikombe kwa ajili ya ukaguzi...

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums

Mkuu Hapo umesahau Toilet paper na T-shirt za hostel Nakumbuka tulikuwa tunapewa T-shirt tatu kwa hiyo siku usafi unavaa moja nyingine mbili unaziweka kwa ajili ya ukaguzi Ila Kasheshe ilikuwa ni siku anakagua Wajadi yaani huyu jamaa ilikuwa akifika tu uwanja wa damu watu wote presha zinaanza kupanda
 
nakumbuka vizuri maisha ya JITE, siwezi kuwasahau Masemele, Madilu mzee wa tai za vitobo, Babu Mafunguo, Mrimi Mnandi, Afande Ismaili, Afande Bruno, Afande Tall, mpiga picha P.DIDI, bila kusahau Mkisi Program
 
Mrimi ameshatangulia mbele ya haki mkuu. Bruno tumbo mzee wa beetle!! Hahahaa...lafudhi ya huyu jamaa ni vituko aise.
 
kwa wale waliosoma jite miaka 1999-2002,nauliza tena wale mapacha watukutu na maarufu kama akina CHACHA wako wapi siku hizi?kutwa utawakuta na vibegi mgongoni over wazungu wa meli.kipindi hicho nakumbuka huyu mtoto maunda zorro alikuwa bado mbichi halafu full mapepe.
 
ebana jamaa sijui wako wapi tuliishi nao sana kota pale za bandari!kuna day moja mzee nimeona mizinguo na uswahilini nna gem ya soka,nikapiga hesabu nijikatae,nikaenda kuzuga pale zilipokua zinawekwa barua za wanafunzi karibu na geti,kuchek huku na kule kweupe nikatoka nduki ya hatari ile kufika getini uso kwa uso na wajadi na alikua katoka kula vitu vyake!kilichofuatua sikilizia usibanduke ni noma!
 
nakumbuka vizuri maisha ya JITE, siwezi kuwasahau Masemele, Madilu mzee wa tai za vitobo, Babu Mafunguo, Mrimi Mnandi, Afande Ismaili, Afande Bruno, Afande Tall, mpiga picha P.DIDI, bila kusahau Mkisi program

Hukusoma enzi za Bwenge ni Discipline Master, Fabian Massawe Head na Afande Shaban mtaka sifa yupo??
 
Back
Top Bottom