Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,650
Kama habari iliyoandikwa na mwandishi Exavery Mzuzu wa Dira ya Mtanzania itakuwa kweli, basi sakata la zabuni ya mafuta TANESCO litachuma mapesa mengi kuliko linavyodhaniwa kuokoa. Mwandishi huyu anaripoti kuwa makampuni yaliyoshinda zabuni kabla ya kutenguliwa na katibu mkuu Maswi yamekimbilia mahakamani kudai fidia. Sasa sijui hili suala kisheria limekaaje, maana hawa PUMA walichofanya ni kuchungulia wenzao wametoa offer kiasi gani halafu wao wakashuka chini yao. Je hii siyo unfair competition?
Pia hivi hatuoni kuwa kuna madhara makubwa sana kama tutaruhusu individuals kuingilia michakato ya kisheria kwa kigezo cha kuokoa "maslahi ya taifa?" Kitendo hiki hiki tunachokiona ni cha kishujaa leo hii, baadaye kitatuumiza vibaya sana. Ni uzalendo huu huu ndio uliogeuka mwiba mchungu kwa Mh. Lowasa. Kwani ilikuwa ni lazima mshindi wa zabuni apatikane kama makampuni yaliyoomba yalitoa bei kubwa? Sheria za manunuzi ya umma zinasemaje kuhusu hili? Kwa nini zabuni isingetangazwa tena ili kuruhusu makampuni zaidi kushiriki (wakiwemo PUMA)?
Kauli aliyotolewa na waziri kuwa wanaodhani bodi haitaingiliwa wanajidanganya inaiweka wapi bodi. Je, kautamaduni haka kakijichimbia mizizi si ndio itakuwa loophole ya ufisadi? Tunashangilia leo bila kujua nini kinakuja kesho. Si lazima itokee kwa waziri aliyepo sasa, inaweza kutokea hata katika wizara nyingine pia, na tutapaswa kuwaelewa na kuheshimu uzalendo wao.
Suala jingine la msingi kabisa hapa: kama kweli PUMA nao walishiriki zabuni ya kwanza na bei yao ikawa juu hadi walipogundua wameshindwa ndipo wakashusha, walitaka kufanya ufisadi pia? Vipi kama makampuni mengine nayo yangepewa nafasi ku-bid kwa kigezo kuwa mshindani wao PUMA kashusha bei, je kuna uwezekano tungewezapata bei chini zaidi ya hiyo 1460/=?
Disclaimer: Mimi si msomi wa sheria za manunuzi au sheria kwa ujumla. Hii ni tafakuri yangu tu.