Walioshinda Zabuni TANESCO wakimbilia Mahakamani!

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,765
10,643
Kama habari iliyoandikwa na mwandishi Exavery Mzuzu wa Dira ya Mtanzania itakuwa kweli, basi sakata la zabuni ya mafuta TANESCO litachuma mapesa mengi kuliko linavyodhaniwa kuokoa. Mwandishi huyu anaripoti kuwa makampuni yaliyoshinda zabuni kabla ya kutenguliwa na katibu mkuu Maswi yamekimbilia mahakamani kudai fidia. Sasa sijui hili suala kisheria limekaaje, maana hawa PUMA walichofanya ni kuchungulia wenzao wametoa offer kiasi gani halafu wao wakashuka chini yao. Je hii siyo unfair competition?

Pia hivi hatuoni kuwa kuna madhara makubwa sana kama tutaruhusu individuals kuingilia michakato ya kisheria kwa kigezo cha kuokoa "maslahi ya taifa?" Kitendo hiki hiki tunachokiona ni cha kishujaa leo hii, baadaye kitatuumiza vibaya sana. Ni uzalendo huu huu ndio uliogeuka mwiba mchungu kwa Mh. Lowasa. Kwani ilikuwa ni lazima mshindi wa zabuni apatikane kama makampuni yaliyoomba yalitoa bei kubwa? Sheria za manunuzi ya umma zinasemaje kuhusu hili? Kwa nini zabuni isingetangazwa tena ili kuruhusu makampuni zaidi kushiriki (wakiwemo PUMA)?

Kauli aliyotolewa na waziri kuwa wanaodhani bodi haitaingiliwa wanajidanganya inaiweka wapi bodi. Je, kautamaduni haka kakijichimbia mizizi si ndio itakuwa loophole ya ufisadi? Tunashangilia leo bila kujua nini kinakuja kesho. Si lazima itokee kwa waziri aliyepo sasa, inaweza kutokea hata katika wizara nyingine pia, na tutapaswa kuwaelewa na kuheshimu uzalendo wao.

Suala jingine la msingi kabisa hapa: kama kweli PUMA nao walishiriki zabuni ya kwanza na bei yao ikawa juu hadi walipogundua wameshindwa ndipo wakashusha, walitaka kufanya ufisadi pia? Vipi kama makampuni mengine nayo yangepewa nafasi ku-bid kwa kigezo kuwa mshindani wao PUMA kashusha bei, je kuna uwezekano tungewezapata bei chini zaidi ya hiyo 1460/=?

Disclaimer: Mimi si msomi wa sheria za manunuzi au sheria kwa ujumla. Hii ni tafakuri yangu tu.
 
Wacha waende mahakamani tu, ni haki yao ya kikatiba na kisheria.
Sasa unapo conclude kwamba serikali italipa mamilioni ya shilingi, wewe ndiye jaji utakayekabidhiwa kesi hiyo ili uitolee judgement kwa favour ya makampuni yanayokusudia kwenda mahakamani? au basi tu umeamua kuchukua mikoba ya sheikh yahya!!??
 
Nyenyere

Kwa ujumla kitendo cha PS kuingilia mchakato wa zabuni kwa kuipa zabuni kampuni ambayop haikushida/haikushiriki ni ukiukwaji wa dhana nzima ya zabuni na ushindani wa kibiashara. Kama kweli kulikuwepo na vitu ambavyo havikukaa vizuri kuhusiana na zabuni, njia sahihi ingalikuwa na kufuta mchakato wote na kuanza upya na kuweka vigezo ambavyo vingezuia makampuni ambayo yalifanya malpractice katika mchakato wa awali.

Kwa jinsi alivyofanya PS, amezuia tanesco kuweza kujua/kupata bei ya chini (maana tuna uhakika gani kama hiyo bei ya puma ndio ya chini, kama mchakato wake haukuhusisha washindani wengine)! Hii tug-of-war yote tunayoishuhudia, hakuna upande ambao umetanguliza maslahi ya taifa mbele. Wote wanatizama 'matumbo' yao kwanza!
 
Last edited by a moderator:
Hata hizo siku za mbeleni kama watatokea individuals ambao wanafanya mambo yenye manufaa zaidi kwa wananchi na Taifa ukilinganisha na maamuzi ya bodi, mimi naona ni sawa tu. Bodi zinaundwa kwa kuamini kuwa kwa kuwa wanakuwa wengi, wataunganisha mawazo yao, na kisha kuja na uamuzi wenye manufaa na tija kuliko uamuzi wa mtu mmoja. Kama inatokea bodi yenye wajumbe wengi, inakaa na kutoka na uamuzi hopeless usio na faida kwa umma, hata ulazima wa hizo bodi haupo. Hiyo bodi iliyohusika na kuteua hayo makampuni ivunjwe, na wajumbe wake wachunguzwe kama walifanya hivyo kwa uzembe, kwa sababu ya uwezo mdogo au walifanya makusudi baada ya kupokea rushwa. Vyovyote iwavyo, wanastahili kufukuzwa kwanza kabla ya hatua nyingine.
 
Kama ni kweli Puma hawaku-bid mwanzoni au walishindwa kwenye kumpata The Lowest Evaluated Tenderer, halafu wakaenda kubadilisha bei baada ya kushindwa, kisheria haikubaliki kabisa. Lakini kama wao nao walikuwa Evaluated na kuingia kwenye negotiations na kushusha bei, na kama makampuni yote yaliyopita kwenye awamu hiyo yalipewa fursa ya kuingia kwenye negotiation, lakini wao hawakushusha bei kwa kiwango ambacho Tanesco walichoona kinafaa, basi wako hapo Kihalali. Tuiache sheria ifanye kazi yake na kila mtu aje na Ushahidi wake.
 
Wacha waende mahakamani tu, ni haki yao ya kikatiba na kisheria.
Sasa unapo conclude kwamba serikali italipa mamilioni ya shilingi, wewe ndiye jaji utakayekabidhiwa kesi hiyo ili uitolee judgement kwa favour ya makampuni yanayokusudia kwenda mahakamani? au basi tu umeamua kuchukua mikoba ya sheikh yahya!!??

Mkuu asante kwa observation yako. Niliandika hivyo kutokana na ukweli kwamba haya makampuni matatu yalishinda zabuni na kuagiza mafuta hayo. Wakati yakiwa katika mchakato wa kupeleka mafuta hayo ndio ikaja taarifa ya zabuni kusitishwa. Vipi kuhusu hizo hoja nyingine?

Bado sijaona tatizo la Mh. Zito mpaka sasa unless rushwa ithibitike. Hapa nahisi kuna political motive.
 
Acha liwalo na liwe...inanikumbusha hadithi ya mtu aliyejitosa kwenye mto wenye maji yenye kasi huku akiwa hajui kuogelea wala majaaliwa yake.
 
Nyenyere

Kwa ujumla kitendo cha PS kuingilia mchakato wa zabuni kwa kuipa zabuni kampuni ambayop haikushida/haikushiriki ni ukiukwaji wa dhana nzima ya zabuni na ushindani wa kibiashara. Kama kweli kulikuwepo na vitu ambavyo havikukaa vizuri kuhusiana na zabuni, njia sahihi ingalikuwa na kufuta mchakato wote na kuanza upya na kuweka vigezo ambavyo vingezuia makampuni ambayo yalifanya malpractice katika mchakato wa awali.

Kwa jinsi alivyofanya PS, amezuia tanesco kuweza kujua/kupata bei ya chini (maana tuna uhakika gani kama hiyo bei ya puma ndio ya chini, kama mchakato wake haukuhusisha washindani wengine)! Hii tug-of-war yote tunayoishuhudia, hakuna upande ambao umetanguliza maslahi ya taifa mbele. Wote wanatizama 'matumbo' yao kwanza!

Kwa hiyo mwenzetu uko happy na ufisadi.Mimi ninavyoelewa ni kwamba accounting officer ndiyo mwenye discretion ya kubadili upepo kama kwa kufanya hivyo ni kwa maslahi ya taifa.Hii imeonyesha alichofanya accounting officer/PS ni kwa maslahi ya taifa considering the matriality of the financial implication in terms of saving.Kwamba angeokoa shs.3billion kwa wiki mbili na hivyo 6bln kwa mwezi ni justifiable kuingilia na sheria imeruhusu.Akina zitto na wenzake imekula kwao.Maswi is safe for ever
 
Mkuu asante kwa observation yako. Niliandika hivyo kutokana na ukweli kwamba haya makampuni matatu yalishinda zabuni na kuagiza mafuta hayo. Wakati yakiwa katika mchakato wa kupeleka mafuta hayo ndio ikaja taarifa ya zabuni kusitishwa. Vipi kuhusu hizo hoja nyingine?

Bado sijaona tatizo la Mh. Zito mpaka sasa unless rushwa ithibitike. Hapa nahisi kuna political motive.
Usiangalie kushinda tu angalia na makando kando mengine yatayomfanya mshindi apewe kazi, umeambiwa accounting officer hasa vetto on any issue regarding procurement provided is for public interest period.Kina zitto wana kesi ya kujibu
 
Unaelezeaje kisheria kwamba tayari washindi wa zabuni walishapatikana na kuagiza mzigo kabla ya kuambiwa zabuni imefutwa. Are they not eligible kupewa compensation for damages resulted?
 
Kwa hiyo mwenzetu uko happy na ufisadi.Mimi ninavyoelewa ni kwamba accounting officer ndiyo mwenye discretion ya kubadili upepo kama kwa kufanya hivyo ni kwa maslahi ya taifa.Hii imeonyesha alichofanya accounting officer/PS ni kwa maslahi ya taifa considering the matriality of the financial implication in terms of saving.Kwamba angeokoa shs.3billion kwa wiki mbili na hivyo 6bln kwa mwezi ni justifiable kuingilia na sheria imeruhusu.Akina zitto na wenzake imekula kwao.Maswi is safe for ever
Hapana. Sipendi ufisadi na pia sipendi mafisadi. Lakini napenda sheria na principles. Ninachokisema hapa ni kuwa bila PUMA kushindanishwa na washindani wengine (kwa kutumia vigezo vya Maswi) tunajuaje kuwa bei yao ndio ya chini kuliko ile ambayo ingepatikana kama washindani wote wangeambiwa walete zabuni upya (kwa vigezo vipya)? Actually alichofanya Maswi apparently inaweza kuonekana kuokoa pesa lakini bado ni kiini macho kwa sababu ametufanya tulinganishe bei ya PUMA na zile za makampuni mengine lakini bei hizo hazikutolewa katia level playing field (PUMA alikuwa tayari anajua wengine wame quote bei gani!). Kwa mfano, kama sasa hivi wakisema waitishe zabuni hiyo upya, si kweli kuwa almost makampuni yote yataleta bei ya chini ya hiyo ya PUMA? - na hivyo taifa kuokoa gharama zaidi.
 
Tanesco imeng'ang'aniwa kama kupe afanyavyo. Yaani kila kona wanaiba. ..agrrrr
 
Unaelezeaje kisheria kwamba tayari washindi wa zabuni walishapatikana na kuagiza mzigo kabla ya kuambiwa zabuni imefutwa. Are they not eligible kupewa compensation for damages resulted?

Inategemea kama hizo tender walishinda kihalali.
 
Lakini pia mkumbuke kuwa ki-mkataba anayetakiwa kununua mafuta kwenda IPTL ni serikali wala si TANESCO walikuwa wanafanya hivyo kuhalalisha wizi na kurahisisha migawo.kwa maana nyingine hiyo tender ni batili pia kwani TANESCO alijitwalia jukumu lisilo lake
 
Kama habari iliyoandikwa na mwandishi Exavery Mzuzu wa Dira ya Mtanzania itakuwa kweli, basi sakata la zabuni ya mafuta TANESCO litachuma mapesa mengi kuliko linavyodhaniwa kuokoa. Mwandishi huyu anaripoti kuwa makampuni yaliyoshinda zabuni kabla ya kutenguliwa na katibu mkuu Maswi yamekimbilia mahakamani kudai fidia. Sasa sijui hili suala kisheria limekaaje, maana hawa PUMA walichofanya ni kuchungulia wenzao wametoa offer kiasi gani halafu wao wakashuka chini yao. Je hii siyo unfair competition?

Pia hivi hatuoni kuwa kuna madhara makubwa sana kama tutaruhusu individuals kuingilia michakato ya kisheria kwa kigezo cha kuokoa "maslahi ya taifa?" Kitendo hiki hiki tunachokiona ni cha kishujaa leo hii, baadaye kitatuumiza vibaya sana. Ni uzalendo huu huu ndio uliogeuka mwiba mchungu kwa Mh. Lowasa. Kwani ilikuwa ni lazima mshindi wa zabuni apatikane kama makampuni yaliyoomba yalitoa bei kubwa? Sheria za manunuzi ya umma zinasemaje kuhusu hili? Kwa nini zabuni isingetangazwa tena ili kuruhusu makampuni zaidi kushiriki (wakiwemo PUMA)?

Kauli aliyotolewa na waziri kuwa wanaodhani bodi haitaingiliwa wanajidanganya inaiweka wapi bodi. Je, kautamaduni haka kakijichimbia mizizi si ndio itakuwa loophole ya ufisadi? Tunashangilia leo bila kujua nini kinakuja kesho. Si lazima itokee kwa waziri aliyepo sasa, inaweza kutokea hata katika wizara nyingine pia, na tutapaswa kuwaelewa na kuheshimu uzalendo wao.

Suala jingine la msingi kabisa hapa: kama kweli PUMA nao walishiriki zabuni ya kwanza na bei yao ikawa juu hadi walipogundua wameshindwa ndipo wakashusha, walitaka kufanya ufisadi pia? Vipi kama makampuni mengine nayo yangepewa nafasi ku-bid kwa kigezo kuwa mshindani wao PUMA kashusha bei, je kuna uwezekano tungewezapata bei chini zaidi ya hiyo 1460/=?

Disclaimer: Mimi si msomi wa sheria za manunuzi au sheria kwa ujumla. Hii ni tafakuri yangu tu.

Kama nilivyomuelewa waziri, alisema kuwa Puma walikuwapo kwenye bidding ya kwanza na kwa bei hiyo hiyo ya chini wakatoswa.Haya makampuni mengine wakapewa kwa mkataba wa 1500 Tshs kwa lita arround there, lakini ilipofika kwenye malipo wakawa wanalipwa 1800 tshs kwa lita. Nadhani tatizo liko hapo maana yake walikiuka mkataba tayari. Labda tufuatilie tena kuujua ukweli kwenye hili.
 
Kuna mdau mmoja nam-quote kama alivyopost:

"Tanzania ni taifa la experiments ambazo nyingine hufichwa nyuma ya pazia la Uzalendo. Hapa yatatokea yale ya Dowans, na Tanesco italazimika tena kulipa fidia kwa sababu hakuna atakayezuia hili kisheria.
Kampuni nane ziliomba zabuni ikiwemo Puma Energy, na katika mchakato huo Puma ikawa disqualified kwa sababu ilikuwa imefungiwa wakati huo baada ya kugoma kuuza mafuta kwa bei ya serikali, na pia kuwa na bei ya juu kuliko wengine na sababu kadhaa za kifundi-kulingana na taarifa za maandishi toka Bodi ya Tanesco. Baada ya kutupwa nje, kwa kuwa walikuwa wameshaangalia bei za wenzao wakati wa ufunguzi wa tenda, wakakimbia kwenda wizarani na kusema walikuwa tayari kuuza mafuta kwa bei ya chini kuliko wale walioshinda zabuni hiyo.
Katibu mkuu ama kwa uzalendo wake kwa nchi au kwa sababu zaidi, akawapa puma zabuni ya bilioni 13 bila kutangaza zabuni nyingine(akwapa juu ya meza kwa sababu walitoa bei nzuri).
Wakati akitoa zabuni hii, kule Tanesco kuna kampuni tatu zilishapewa zabuni na kuambiwa ziagize mafuta, na zikawa zimeagiza. Wakati wanajiandaa kupeleka mafuta, wakaambiwa tenda imefutwa na kapewa Puma Energy. Sarakasi ikaanzia hapo.
Na Tanesco wakaamrishwa na katibu mkuu kuilipa Puma na kuiandika LPO ya bilioni 13, na Muhando kwa uoga ama kwa sababu ya utii kwa wakubwa wake akafuata maagizo. Waliokuwa wameshinda zabuni wakakimbilia PPRA na sasa wako mahakamani wanadai fidia.
Maswi siyo mla rushwa, na miongoni mwa vijana waadilifu lakini katika hili nadhani aliteleza, na kama ni kumtetea nitafanya hivyo kwa sababu ya heshima yangu kati yangu na yeye-lakini hakutenda vema.

Source: https://groups.google.com/forum/?fromgroups#!msg/mabadilikotanzania/sy-SJ4Z4M9s/LS3jqIlw3qQJ
 
Mkuu asante kwa observation yako. Niliandika hivyo kutokana na ukweli kwamba haya makampuni matatu yalishinda zabuni na kuagiza mafuta hayo. Wakati yakiwa katika mchakato wa kupeleka mafuta hayo ndio ikaja taarifa ya zabuni kusitishwa. Vipi kuhusu hizo hoja nyingine?

Bado sijaona tatizo la Mh. Zito mpaka sasa unless rushwa ithibitike. Hapa nahisi kuna political motive.

Hadi nitakapopata taarifa kamili juu ya mchakato mzima wa zabuni hiyo ndipo nitaweza kutoa maoni ya uhakika zaidi.
Lakini kwa uzoefu wangu mdogo kwenye mambo ya manunuzi, wazabuni mnaweza kuombwa na mnunuzi kushusha bei kidogo wakati wa negotiations kama mnunuzi anaona wazabuni wote mko juu ya kiwango cha bajeti yake.

Katika hili la tanesco na mafuta sijajua kwamba ni katika hatua gani katibu mkuu aliingilia kati mchakato wa zabuni na kuipa zabuni hiyo kampuni ya PUMA. Nadhani kwa hayo makampuni kwenda mahakamani yatatusaidia kufahamu mengi zaidi yaliyokuwa yameigubika hiyo zabuni.

Suala la shutuma za rushwa dhidi ya zitto kabwe sidhani kama hapa ni mahali pake kwakuwa iko thread ya jambo hilo na tumelijadili sana kule, unaweza kuitembelea utaona mawazo ya wadau, na ya kwangu utayakuta kule, hapa tujikite kuzungumzia mchakato wa zabuni ya mafuta na tishio la wazabuni kwenda mahakamani.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom