Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Waliojiandikishwa ni milioni 19
Waliopiga kura (turn out) ni milioni 8.6
Kikwete kapata kura milioni 5.2
Slaa kapata kura milioni 2.2
Katika chaguzi kuu kumi zilizopita hatujawahi kuwa na waliojitokeza kupiga kura chini ya asilimia 70, HAIJAWAHI KUTOKEA. Asilimia 70 ya milioni 19 ni watu milioni 13.3
Mwaka huu waliojitokeza (kuanzia saa kumi alfajiri sehemu nyingine) ni asilimia 42.84.
Ina maana karibu watu milioni 12, hawakupiga kura Jumapili ile kwa sababu mbalimbali. Naomba tutoe sababu ambazo zingeweza kuwafanya watu wasipige kura na makisio ya idadi ya watu waliokumbwa na sababu hizo kitaifa tuone kama tunaweza kufikia watu milioni 12.
Unafikiri wale wote waliopiga kura uchaguzi huu uliopita wakiitwa wajitokeze au kuhesabiwa idadi yao itakuwa karibu na 13.3 au na 8.6?
NB: Kuna idadi ya watu milioni 4 wamepungua kutoka kura za Kikwete 2005 na 2010; na kuna watu milioni 4.7 wanapungua kutoka makisio ya asilimia 70 ya waliojiandikisha kulinganisha na wale tulioripotiwa wamepiga kura. WHAT HAPPENED?

Ingawa shahada ziluzwa, bado watu wengi sana walipiga kura kuliko kawaida. To the least, kulikuwa na turnout isyopungua 65%.

Nina imani kuwa hesabu kamili haikutolea, ndiyo maana leo tunasikia jimbo la vunjo kura zionaongezeka. Kuna majimbo mengi sana ambayo kulikuwa na uharibifu wa makusudi wa kura.

Inabidi ndugu zangu tujitafutie utaratibu wetu wa kupiga kura. baadhi ya mapendeklezoa yangu ni:

(a) Kuharamisha potezaji shahada ya kura kusudi liwe ni kosa la jinai.

(b) Kuaharamisha uzembe wa kutopiga kura bila sababu ya maana ili pia liwe ni kosa la jinai (kama ilivyo Australia na New Zealand)

(c)Kuwa na masanduku mawili ya kura: sanduku la kura halisi linalokaa ndani ya chuma cha kura, na sanduku la vishina litakalokuwa sehemua ya wazi. Daima lazima hesabu ya masanduku hayo mawili ikubaliane wakati wote...........( I may have to think further on this proposal).
Hili la 2010 limeshapita, kilichobaki ni kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015 .
Mimi naona tangia mwanzo wa zoezi zima kumekuwa na Deliberate Exaggeration ya namba ya wapiga KURA. Ikumbukwe mwanzo NEC ilisema waliojiandika kupiga KURA ni 19+mil na wakati wa kutangaza ikaja kuwa ni 20+mil.
Naungana na wenzangu hapo juu kuwa kadi a kupiga KURA this time zilinunuliwa sana na si kwa ajili ya kwenda kupigia kura bali kuziondoa katika mzunguko wa kupigia kura hasa Upinzania na ikilengwa wagombea wa CHADEMA.
Mungi, ndio maana tuna soma la historia, lengo sio tuu kujua Mangi Meli, Sina na Marealle walifanya nini au kulitokea nini, lengo ni kuangalia tulipotoka, kupima tulipo ili kujua tunakokwenda. Hivyo lazima tujue kimetokea nini na kwa sababu zipi watu hawakujitokeza?.Hili la 2010 limeshapita, kilichobaki ni kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015, ni wakati muafaka kwa wanasiasa hasa vyama vyenye nia ya dhati ya kuiletea maendeleo nchi hii kuwahamasisha watu hasa vijana ambao wamefikia umri wa kupiga kura kujiandikisha kupiga kura.
Ninaamini chama changu cha CHADEMA kitakuwa mstari wa mbele kuwahamasisha jamii hasa vijana, mimi binafsi nilishaanza hii kazi ya kuwahamasisha vijana.
Sababu ni kama ifuatavyo
Waliokufa tangu daftari liliporekebishwa 300,000
Waliokua wagonjwa siku ya kupiga kura 400,000
waliokua safarini (ndani na nje ya nchi) 150,000
walikosa majina yao kwenye daftari 2,000,000
waliopoteza/uza shahada zao 700,000
wanachama wa ccm waliokataa kupiga kura 800,000
watanzania wazembe waliokataa kupiga kura 500,0000
Kichuguu.. lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.6 kati ya milioni 19? what happened to more than 10 million people.