Waliomwombea mabaya Makamba walie tu.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliomwombea mabaya Makamba walie tu....................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 4, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  Makamba kuendelea kuula CCM Saturday, 04 December 2010 07:35

  [​IMG]Fredy Azzah
  CCM imesema haina mpango wa kufanya mabadiliko yoyote ya uongozi hadi wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho uliopangwa kufanyika mwaka kesho, uamuzi ambao unamfanya katibu mkuu wa sasa, Yusuf Makamba utakapofika kuwa na uhakika wa kumalizia kipindi chake.
  Baada ya tofauti kubwa zilizojitokeza kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, kupoteza viti vingi vya ubunge na ushindi wa mgombea urais wa chama hicho kupungua kwa takriban asilimia 20, ilibashiriwa kuwa CCM ingefanya mabadiliko makubwa, ikiwa ni pamoja na kumuondoa Makamba ambaye amekuwa akilaumiwa kwa kushindwa kumudu nafasi yake hasa wakati wa migogoro.

  CCM pia ilikuwa imeitisha kikao chake cha kamati kuu Desemba mosi jijini Dar es salaam ambacho kilibashiriwa na wengi kuwa kingefanya mabadiliko hayo, lakini ikasemekana kuwa pande mbili zilianza kupingana kuhusu uamuzi wa kumng'oa Makamba. Kikao hicho sasa kimeahirishwa. “Kwa katiba ya chama chetu, viongozi wanaongoza kwa kipindi cha miaka mitano... kwa sasa hakuna mpango wowote wa kumbadilisha katibu mkuu; narudia tena hakuna mpango wowote wa kumbadilisha katibu mkuu,” alisema makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa. “Kwa viongozi wote wa CCM uchaguzi wetu utafanyika mwaka 2012, wakati huo viongozi wote tuliochaguliwa mwaka 2007 muda wetu utakuwa umekwisha.

  Kuna magazeti, lakini siyo Mwananchi; weka kwenye mabano hiyo, kazi yake ni kuandika habari za uongo, uzushi na uzandiki. "Andika maneno hayo kama nilivyo yataja halafu ishia hapohapo tena uiweke hiyo headline.” Habari ambazo Mwananchi ilizipata zinasema kuwa kikao hicho cha kamati kuu kiliahirishwa kutokana na pande mbili kutofautiana katika suala hilo la kumuondoa Makamba ili kuimarisha chama.

  Habari hizo zilisema kuwa CCM ilikuwa inakusudia kufanya mabadiliko makubwa katika safu zake za uongozi baada ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi mkuu ambao ulianza kwa wanachama kutofautiana kwenye kura za maoni na baadaye halmashauri kuu kupitisha majina ya watu ambao walishindwa na kuendelea kwa makundi yaliyoibuka wakati wa kura za maoni ambayo pia yalichangia kuanguka kwa CCM kwenye ubunge, hasa Tanzania Bara.
  Vyombo vya habari viliripoti mapema wiki hii kuwa waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Makazi, John Chiligati hakurejeshwa kwenye uwaziri ikiwa ni mkakati wa kumuandaa kumbadili Makamba katika nafasi ya ukatibu mkuu. Chiligati amekuwa ni katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, kazi ambayo wachambuzi wanadai aliifanya vizuri.

  Habari zaidi zinadai kwamba kundi ambalo lisingependa Makamba ang’oke ndilo lililosababisha kuahirishwa kwa kikao hicho cha kamati kuu ya CCM, uamuzi uliotafsiriwa kuwa ni ushindi kwa kundi hilo katika harakati zake za maandalizi kwa ajili ya kumuwezesha mtu wao kuingia Ikulu mwaka 2015. Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa pamoja na kuahirishwa kwa kikao hicho, suala la Makamba litaibuka wakati CCM itakapokutana kujadili majina ya wagombea umeya wa maeneo mbalimbali kutokana na upande mmoja kutoridhishwa na uamuzi wa kutomuondoa kada huyo.

  Lakini Msekwa aliiambia Mwananchi kuwa kuahirishwa kwa kikao cha kamati kuu kunatokana na kutokamilika kwa ajenda ya uteuzi wa mameya ambayo alisema ilikuwa ajenda kuu. Kwa mujibu wa Msekwa, mkutano huo ulikuwa na ajenda moja tu ya watu wanaogombea nafasi za umeya kupitia chama hicho. Spika huyo wa zamani wa Bunge alifafanua kuwa kwa sababu majina hayo yalikuwa hayajawa tayari, mkutano huo uliahirishwa mpaka utakapoitishwa tena. “Siwezi kukwambia ni lini tutafanya tena huo mkutano; tarehe tunaijua wenyewe, lakini hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kuuahirisha,” alisema Msekwa.

  Kikwete alikabidhiwa uenyekiti wa CCM Juni 25, 2006, ikiwa ni miezi michache baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchi na baadaye alipendekeza sekretarieti yake, akimteua Makamba kuwa katibu mkuu kushika nafasi ya Phillip Mangula. Katika sekretarieti hiyo, nafasi ya naibu katibu mkuu wa Bara ilikwenda kwa Jaka Mwambi wakati ya Zanzibar ilichukuliwa na Salehe Ramadhan Ferouz. Nafasi ya katibu wa uchumi na fedha ilikwenda kwa Amos Makala ambaye alichukua nafasi ya Rostam Aziz na nafasi ya katibu wa organaizesheni ilichukuliwa na Kidawa Hamid.
  Wengine waliochakuliwa katika mkutano huo walikuwa ni Aggrey Mwanri aliyeteuliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na John Chiligati. Nafasi ya katibu wa siasa na uhusiano wa kimataifa ilichukuliwa na Dk Asha Rose Migiro ambaye kwa sasa ni naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN). Naye Msekwa ambaye atamaliza muda wake kipindi hicho alishika nafasi ya umakamu mwenyekiti wa chama hicho akirithi mikoba ya John Malecela.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Poleni sana CCM
  mnaongozwa na mzimu
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Pua zimeshazoea harufu ya uvundo!
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mnalo hilo, muombea mabaya humfika yeye sasa mfukuzeni zitto mbaki wadini ile peke yenu
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hili unalolisema kweli lina ukweli wake khaaaaa

   
 6. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Loleee!!!! Unamaanisha kwa Nzi kinyesi deal???????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Makamba ni kiboko yao........ keshaenda kuwapika hao, hawaoni wala nini... wakitaka labda hayo maamuzi wakayafanyie nje ya nchi na asijue

  uswahili una faida zake
   
 8. n

  ngoko JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ohh!!! mizimu tena , ile inayomletea maono mnajimu Y.H au .
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  nguruwe lake tope
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  - Siasa za majina na Tanzania zimetufikisha pabaya sana hili taifa na bado hatuamki usingizini, I mean as if Mh. Makamba akitolewa kwenye nafasi basi taifa litasonga mbele na maendeleo!

  - Mungu aendelee tu kutuhurumia hili taifa!, maana with in us wananchi hakuna msaada kabisaa wa kujikomboa!  William.
   
 11. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  Makamba ameachwa amalizie kipindi chake. Chama hakiwezi kumbwaga na hivyo kuwa na ''lundo la makatibu wakuu wastaafu'' - ni gharama kuwahudumia. In fact, Makamba ataendelea kipindi kingine tena ili yeye na mwenyekiti wake wamalize pamoja come 2015

  Safi sana CCM
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Chama chetu cha 'cc ni m' ni chama kinachohitaji walopokaji kwa sababu kinaendeshwa kwa propaganda. Sasa aliyekuwa anamwombea mabaya makamba alikuwa hakijui chama chetu vizuri.
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,859
  Likes Received: 11,978
  Trophy Points: 280
  Ofcourse oppositions still need Makamba hasn't finished work yet.
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  mabaya yamemfika mengi kwani alitegemea Mwanae J Mkamba apate angalau Uwaziri lakini hakupata , kweli JK Kiboko latelekeza familia za waliokuwa na kieleeleee na na kimbelembele
   
 15. S

  Siao Member

  #15
  Dec 4, 2010
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa upinza ni vizuri makamba akibaki - upinzani unapata mahali kwa kuanzia makamba akiwepo... atachemsha wakati wowote, na hapohapo chchm itashikiwa... kwenye siasa tunahitaji watu wanaokosea - kwa usalama wa wananchi...
   
 16. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo kwa Makamba kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM ndiyo nchi inaendelea?

  Logic ni kuwa CCM ndicho Chama Tawala na maana yake ndicho kinaunda Serikali ::: As it stand Makamba ana play a very big role katika UTAWALA wa Tanzania (right?) - Tatizo ni kuwa Makamba hastahili kuwa sehemu ya UTAWALA wa nchi hii ndiyo maana tunapiga kelele aondoke CCM and probably! the right person anaweza kuchukua nafasi hiyo na kuwa MTAWALA wa kutupeleka katika maendeleo tunayotaka!
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  - Tunatakiwa kujali taifa sana kuliko vyama vya siasa, huu sio uwanja wa chama chochote lakini ninaamini sana kwamba ni uwanja wa taifa zaidi kuliko chama chochote cha siasa, ya vyama tuwaachie wenyewe wenye vyama mpaka inapobidi tu, viongozi wa ndani wa CCM wanatuhusu nini taifa?

  - I mean CCM ndio kwanza wameshinda uchaguzi taifa, understandable kwamba wameshuka namba lakini bado Mh. Makamba anaweza kwua na valid argument kwamba CCM imeshinda under his watch and directives, ndio maana niansema haya ya uongozi wa ndani wa vyama tuwaachie wenyewe vyama vya siasa!


  William.
   
Loading...