ZANZIBAR: Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kukutana kwa dharula Leo

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
5,059
4,224
IMG-20240518-WA0100.jpg


Habari Tanzania,

Kama barua iliyoandikwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Mafunzo & Uenezi Cde Amos Gabriel Makalla inavyojieleza.

Tuendelee kuiombea CCM kwani ni hakika bila CCM imara nchi hii itayumba sana.

Kiduma Chama Cha Mapinduzi.


=======
UPDATES 001.
DK.MWINYI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM, ZANZIBAR

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameongoza kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar tarehe: 19 Mei 2024

IMG-20240519-WA0117.jpg


Dkt Mwinyi makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwa na Mzee Abdulrahim Kinana pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi katika kikao maalum Visiwani Zanzibar.

=====
UPDATES 002.

IMG-20240519-WA0118.jpg


Katibu Mkuu Dkt Emmanuel Nchimbi akifafanua agenda za
kikao.

===
UPDATES 003.
IMG-20240519-WA0148.jpg


Kamati Kuu imemteua Mrs. Suzan Peter kuwa Mrithi wa Jokati Mwegelo katika nafasi ya Katibu Mkuu UWT.


KAZI IENDELEE
 
View attachment 2993659

Habari Tanzania,

Kama barua iliyoandikwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Mafunzo & Uenezi Cde Amos Gabriel Makalla inavyojieleza.

Tuendelee kuiombea CCM kwani ni hakika bila CCM imara nchi hii itayumba sana.

Kiduma Chama Cha Mapinduzi.​
Chama Cha Majizi* bring back our Tanganyika!
.
.
.
.

*Majizi ya Uchaguzi, Fedha & Rasilimali za Umma, na Haki za Raia.
 
Kamati kuu ccm inakutana Zanzibar kujadili mapendekezo ya kamati ya maadili iliyomhoji na kumsikiliza Makonda kufuatia kauli yake kuwa kuna mawaziri wanamtukana rais Samia .


Nipo hapa kwenye kikao, nitaendelea kuwajuza
 
Wanamla kichwa yule mbunge aliyesema kuwa yeye ni Mzanzibari.

#Akili_za_matikiti_maji
Thubutu, wakifanya hivyo wataongeza makelele ya watu na kwa sasa wanataka utulivu... sana sana labda watakuja na kauli za kutuliza gadhabu za waTanganyika na sounds za namna hiyo.
Maneno ni mengi sana kwa sasa na wao ni fofofo tu kwa siku zilizopita, angalau wameamuka sasa.
 
View attachment 2993659

Habari Tanzania,

Kama barua iliyoandikwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Mafunzo & Uenezi Cde Amos Gabriel Makalla inavyojieleza.

Tuendelee kuiombea CCM kwani ni hakika bila CCM imara nchi hii itayumba sana.

Kiduma Chama Cha Mapinduzi.​
kidumu chama Tawala

Kila la Kheri Kamati Kuu, Daima Tunawaombea kheri....

Kwa Shauku na Matumaini Makubwa Sana,

Macho na Maskio ya waTatanzania ni Kisiwa Ndui Zanzubar :BASED:
 
Ajenda:

  1. Kujaribu kuipiku kamati kuu ya CHADEMA inayofuatiliwa sana na wananchi, na ukweli sasa maandamano na madai ya CHADEMA kuhusu katiba mpya, uchaguzi huru wa haki, kilio cha hali ngumu ya maisha ndiyo mambo wananchi wanayo mioyoni mwao huku madai hayo yamebebwa na CHADEMA kuliko chama dola kongwe
  2. Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?
Nchi imewaka na sasa hata ccm hawana cha kuwaambia watawaliwa... wasipo jipanga itakula kwao.
 
Back
Top Bottom