Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Malima kwa kauli yake alikubali ya kuwa alikuwa na SMG kwakuwa hakujua atakutana na nani na aliyejiandaaje? Iweje leo mkuu wa police anakanusha kauli ya mshtaki? Je Malima hajui smg? Utata mtupu.... Achen hizo mapolice....wabongo hatudanganywi tena...
 
Ni wazi mwizi alikuwa kiburudisho chake ...
hakuwa mzoefu bali alitamani hivo vitu vya mheshimiwa baada ya kuviona chumbani .
akilinganisha na hali ngumu ya maisha inayomkabili.
 
Waache kutupotosha. Wamepika story za kuwahadaa wananchi.
Amesafishwa na Malaya. na mnavyojua malaya hana shida na silaha.
hata mwizi wa kuku haachi silaha. yaani mabegi yabebwe asiweke silaha kwenye begi!
Polisi wanaboa sana
 
Malima kwa kauli yake alikubali ya kuwa alikuwa na SMG kwakuwa hakujua atakutana na nani na aliyejiandaaje? Iweje leo mkuu wa police anakanusha kauli ya mshtaki? Je Malima hajui smg? Utata mtupu.... Achen hizo mapolice....wabongo hatudanganywi tena...

Tatizo lao wanaamini watanzania wote ni Vilaza
Malima mwenyewe kaongea tena kwa msisitizo kabisa
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’ [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Fidelis Butahe
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Duuuh..kamanda naye keshachemsha katika stori yao..hahahahahah
 
Tangu sakata hili lianze mimi nilisema ingekuwa ni nchi za wenzetu walio makini POLISI angepandishwa cheo kwa ku-UNCOVER huu uongo wa Malima. Lakini nchi hii ya Wadanganyika huyo RPC Adolphina Chialo atapandishwa cheo kwa ku-COVER UP uongo wa Malima.

Lakini pia anapojaribu ku-cook up hii story ya Malima, awaapatie basi hata POLISI wenzake wajaribu kufukia fukia mashimo, kwani ina matundu mengi ambayo hata mtoto wa STD I atayachana chana vibaya
1. Vitu vilikutwa kwa mama Mdogo? Huyo mama Mdogo hatajwi jina wala sehemu anayoishi?!
2. Watuhumiwa tayari wamekamatwa, Majina yao na sehemu wanaoishi hayatajwi?
3. Aliyemuibia sio MWANAMKE! Ina maana mwizi wanamfahamu na atakuwa mawanaume, kwanini hawamsemi?
4. Nyao za mwizi zilikutwa nje ya dirisha la Malima,mwizi hakuwa na viatu, Asubuhi ya tukio nyao hizo hatukuziona!
5. Malima alikiri alikuwa na SMG, Kaimu kamanada amesema SMG haikuibiwa, RPC anasema hakuwa na SMG? Lakini pia hasemi ilikuwa ni bunduki ya aina gani?

Nchi hii kweli imejaa usanii, lakini kinachonisikitishwa kuna W.A.J.I.N.G.A tena wengi wanao buy hii cooked story!
 
nimesoma page ya kwanza tu nikajua habari ya kupikwa......waliposema kuwa hakuibiwa na mwanamke hapo ndo ameharibu........malima mwenyewe alisema kuwa alikuwa na smg na bastola na akasema wazi kabisa kuwa silaha zile ni mtaji mzuri wa maisha
 
Waache kutupotosha. Wamepika story za kuwahadaa wananchi.
Amesafishwa na Malaya. na mnavyojua malaya hana shida na silaha.
hata mwizi wa kuku haachi silaha. yaani mabegi yabebwe asiweke silaha kwenye begi!
Polisi wanaboa sana

Enhee, tupe uzoefu, inaonesha amma umesomea kupambana na uhalifu amma una uzoefu wa muda mrefu wa shughuli hizo, amma ni wa lile kabila maarufu linalojulikana Afrika Mashariki kwa wizi.

Inafurahisha sana, tunaomba utuchambulie kwa kina.
 
Anasema anabeba hiyo SMG kwani hajui adui yake yuko vipi. Ina maana SMG ndo silaha kubwa kabisa ambayo adui anaweza kuwa nayo, wataalamu wa silaha watueleze. Kama maadui ni watano na kila mmoja ana SMG, yupo tayari kutembea na ghala la silaha kwa ajili ya kujilinda!!!
 
asa kyupi alichoiba changu alimvua au aliiba ya kwny begi?? Maana ka aliiba alokua amevaa jamaa basi inawezkana changu kamfanya vitu vingi sana jamaa.., hata vidole maeneo yale..,
 
Mbona jinsia ya mwizi hawajataja?
Wkt tuliambiwa mwanamke mweupe alifika na waziri mjengoni hapo.
 
Tatizo la Malaya wa bei poa, LAZIMA WAPIGE SACHI!
 
Hivi kulikuwa kuna haja ya kumkamata mwizi ili umuulize na aseme kuwa bunduki haikuwa SMG? Wakati tunajuwa bunduki haikuibiwa, kulikuwa kuna haja ya kumkamata ndiyo tujue kuwa ni SMG au RPG?
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Fidelis Butahe
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hesabu ya hapo kwenye nyekundu sijaielewa, simu tatu mbili zimewekwa gharama yake ambayo ni 750,000, hiyo blackberry ni zaidi ya 3,000,000 ili kuipata hiyo hesabu ya Milioni 5.5!! Aisee
 
Back
Top Bottom