Waliomchoma mwalimu mshale shingoni wakioneshana ujasiri wakamatwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
e5ae6099ed45bc1cc79fd742c687e887

Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe

JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya linawashikilia vijana watano kwa tuhuma za kumuua kwa kumuchoma na mshale shingoni mwalimu Justine Sospeter Ogo wa Shule ya sekondari Itiryo.

Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Novemba 14,2019 asubuhi katika Kijiji cha Itiryo.

“Chanzo cha mauaji hayo ni vijana wapatao wanane walikuwa wanatembea barabarani wakiwa na silaha za jadi wakiwa wanajiandaa kwenda kwenye tohara Desemba, walikuwa wanasimamisha watu na kuwaomba fedha kwa nguvu kuonyesha ujasiri.

“Mwalimu aliyeuawa alikuwa anampeleka mwenzake kusimamia mitihani ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bungurere, (vijana hao) wakamsimamisha na kuanza kumdai awape fedha, mwalimu na wenzake wakawa wanaondoka bila kusimama, ndipo kijana mmoja wapo alimchoma na mshale shingoni kutoka upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto, alifariki alipofikishwa hospitali,”alisema Mwaibambe.

Mwaibambe alisema vijana watano wamekamatwa kati ya nane wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wengine waliobaki.

Alitaja majina ya vijana hao kuwa ni Nchore Richard, Marwa Mwita Gichome, Gisiri Simion Mhere, Makenge Hongo Chacha na Muhere Mwita Gichumu.

Alisema kwa sasa vijana hao wanashikiliwa kwa mahojiano na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani.

Kamanda Mwaibambe alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi, walezi na wananchi kuwafunza watoto wao maadili mema vinginevyo sheria haitasita kuwachukulia hatua watoto wote wanaojihusha na vitendo vya kihalifu.

Awali akisimulia tukio hilo, Mwalimu wa taaluma katika Shule ya Sekondari Itiryo, Nicku Bariki, alisema mwalimu huyo aliuawa akiendesha pikipiki wakati akiwa njiani na wenzake wawili aliokuwa amewapakia wakielekea Shule ya Sekondari Bungurere kusimamia mitihani.

Chanzo: Mtanzania
 
Itiryo, huko Nyanungu, Itununu, sijui wapi huko kote vijana wengi hana shule na pia maarifa, wengi wanavuta bangi, wengi wezi wa ng'ombe na majambazi.

Hao madogo wachezee miaka qumamae zao.
 
Ila watu wa musoma Ndio walifanya tikashinda vita vya uganda

Vijana wa pwani walitafuta vibali vya kuumwa ili wasiende vitani


Siungi mkono mauaji ya kinyama huo ni ukatili mbaya sana
 
Hebu ona ulivyo mpumbavu,kwa hiyo hata wakitaka kumbaka mamio utawapa ushirikiano kisa tu walisaidia vita ya uganda? Hujui hata kuwa vita yenyewe ilipiganwa wakati hivyo vitoto havijatarajia kuzaliwa!! Nikuache tu upambane na upumbavu wako,hakuna wa kukusaidia
Ila watu wa musoma Ndio walifanya tikashinda vita vya uganda

Vijana wa pwani walitafuta vibali vya kuumwa ili wasiende vitani
 
Back
Top Bottom