Waliokuwa 10 bora Tanzania (PCB) nane kati yao wamenyimwa mkopo

taifa limegawanyika maana kwenye kulipa kodi tunalipa wote lakini likija swala la kusoma ni huyu anaweza kupewa mkopo ambao ni kodi za wote lakini huyu hawezi maana wazazi wake wana uwezo Eti tunataka kwenda kwenye uchumi wa kati na ubaguzi huu maana kesho utasikia huyu alisomeshwa na wazazi wake kwa hiyo ana uwezo so hatuwezi kumpatia ajira
 
Tumia akili kufikiria mkuu..huo ni mkopo kwa wale wasioweza kujisomesha chuo na sio fadhila kwa waliofaulu

Hapo wanatumia vigezo gani kama baba alimsomesha mtoto wakati anafanya kazi sasa amestaafu kinua mgongo 25% mtoto amefaulu anaambiwa hupati mkopo!! Akimaliza mtamuuliza kwani ni sio mzalendo ? Akipata Kazi Botswana?
 
Sio rahisi mzazi kumsomesha mtoto sekondari ada 4M+ then familia hiyohiyo ishindwe kutoa 1.8M kumsomesha chuo..vitu vingine tuwe tu wakweli

Afterall tujue kuwa huo ni mkopo na utarudishwa na mkopaji pindi atakapomaliza masomo yake..
Hapo wanatumia vigezo gani kama baba alimsomesha mtoto wakati anafanya kazi sasa amestaafu kinua mgongo 25% mtoto amefaulu anaambiwa hupati mkopo!! Akimaliza mtamuuliza kwani ni sio mzalendo ? Akipata Kazi Botswana?
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni
Kwny mkopo umeaongea pumba
Ila kwny kuwajal kwa kuwaendeleza kwa upekee wao, nakupa big up kwa nice idea
 
Kama waliomba na wenyewe wana haki ya kupata mkopo. Kuna wazazi wanajinyima ili watoto wao wasome shule nzuri akimaliza six anapumua akitegemea mkopo utampunguzia majukumu.
 
Tumia akili kufikiria mkuu..huo ni mkopo kwa wale wasioweza kujisomesha chuo na sio fadhila kwa waliofaulu
Mkopo sio msaada. Kiposha wote, kisha waambie warudishe.
Kwani umesikia wale waliosoma private wamekataa kurudisha?
No roho mbay tu, ndio inayoongoza mawazo mengine.
 
lengo kubwa la huu uzi ni kuonesha mwenye nacho aongezewe na asiyenacho azidi kukosa...kuwa top 10 si ndiyo kigezo cha kupata mkopo na hata kwenye form ya mkopo hakuna hiko kigezo...na serikali si wajinga washaona dhairi hao nane waliokosa mikopo wanaweza jisomesha bila hata mikopo sema ni uzembe tu si kwamba hawana pesa ila wameomba mikopo kwa mazoea...ukitaka kuamini je ni kweli wameshindwa kwenda chuo baada ya kukosa mikopo? jibu hapana
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni
kawaida tu...kufaulu sana sio kigezo cha kupata mkopo. labda familia yao ina uchumi mzuri kitu ambacho kinamwekea kikwazo kwenye kupata mkopo, na mkopo uko pale kwa ajili ya watoto wanaotoka familia duni
 
Tatizo una hasira sana na inaonekana unatumia makalio kufikri....mkopo ninkwa ajili ya kusaidia wasiojiweza na sio reward kwa aliyefaulu.....alaf hii ni Tanzania na sio nchi za wenzetu
Mikopo ni kwa yeyote anayeweza kulipa.
 
Sometime inachekesha mnaweza sema kwa sababu wamesoma shule za gharama
Ooh wazazi wao wana pesa wawalilie na chuo
But turud katika ukweli “ hawa ni watu wenye uwezo mkubwa na vipaji vikubwa sana ingetakiwa serikali iinvest kwao, iwatafutie vyuo bora na kuwasomesha ili kutoa madaktari bora kabisa wa kuja kulisaidia taifa”
Inashangaza kuona nane kati yao wamekosa mkopo na wawili ndo wamepata ufadhiri kutoka taasisi binafsi

Sawa wamesoma shule za gharama but hawa ni watu muhim sana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia Taifa mbeleni

Sababu za KIPUUZI. Wazazi wao waliweza kuwasaidia kupata elimu bora ya chini hawashindwi kuwatafutia vyuo bora kwa elimu ya juu. Hivi kwa akili yako hiyo uliyotumia kuwaza haya umewahi kufikiri kuwa kijana ambaye familia yake inamudu kulipa milioni 10 ada ya sekondari atakuwa tayari kuwa posted kwetu Litumbandyosi ili akaitumikie serikali iliyomsomesha? Kwa mshahara upi wakati familia yake ina more than enough na imewekeza kwenye elimu yake ilo iifae familia. Acheni masikini wasomeshwe wakatumikie ndugu zao mashambani huko nyie.
 
kuna point hapa serikali yetu ijaribu kuwekeza kwa wale wanaoonekana kuwa dinstinctive, mambo makubwa katika nchi yoyote huletwa na watu wachache wenye uwezo tofauti kiakili na wengine.

Angalau top 3 ama 2 katika mitihani ya F6 kuwe na kipaumbele cha kugharamiwa na serikali katika prominent universities.
 
Nilichoambulia kwenye uzi huu ni kuwa Jitihada binafsi ni kizuizi cha mtu kupata/kupewa msaada! Yaani nimeuza shamba langu nililoachiwa urithi na fedha zote nikazipeleka kumsomesha mwanangu kwenye shule bora tayari naonekana tajiri wakati hata shamba tu la kulima mchicha nilishaliuza!Hilo ni moja! Nna jingine ni kuwa Shule za binafsi Ni bora sana kuliko zile za serikali ndiyo maana kwenye Top 10 wanajazana wa private schools,
 
Unatakiwa kuekewa hoja hizi
1. Kupata division one kwa shule za private siyo kigezo cha kuwa na akili nyingi kiasi cha kwamba serikali ilazimike kukupa mkopo hata kama haujakidhi vigezo vingine vya kupatiwa mkopo. Mtu anayesoma private anakutana na mazingira mazuri ya kusoma ikiwamo vitabu, walimu, ratiba , vitu ambavyo mtoto anayesoma government anavikosa sana. Mfano shule nyingi hazina walimu wakutosha wa phys, na advanced math.
NB: usisahau kwamba pamoja na mazingira kuwa magumu kuna watu wamepata dv 1 ya pcb kutoka shule za government.
2. Katika orodha ya vigezo vya mwanafunzi kupatiwa mkopo kigezo cha ufaulu hakipo kabisa
3. Zaman tulikuwa tunaenda chuo watu wachache sana. Hivyo pesa ilikuwa ya kutosha na serikali ilikuwa na uwezo wa kuwapa wanafunzi wengi mkopo hivyo serikali ilikuwa inazingatia sana kigezo cha kusoma coz ambazo ni priority, katika ugawaji wa mikopo, kuliko kigezo cha umaskini. Ila saiv wanaoenda chuo ni wengi sana, na mheshimiwa kaongeza bajeti ya serikali kwenye mikopo lakini bado watu ni wengi. Ndio maana serikali ikaona kwamba iangalie sana kigezo cha uwezo wa mwanafunzi kulipia ada kuliko vigezo vingine. Kwahiyo wataanza maskini kwanza kupata mikopo ndipo watafuata wengine
 
Nakumbuka mwaka 2016 ndio mwaka ambao walikuja wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza vyuoni. Na vigezo vya ugawaji mikopo vilikuwa vile vya zamani. Wanafunzi wengi sana walikosa mikopo matajiri na maskini. Nakumbuka pale udsm madogo wengi watoto wa maskini walirudi nyumbani kwasababu hakukuwa na namna nyingine ya kupata pesa kiasi cha 1m ya ada na pesa nyingine za kujikimu. Ila watoto wa matajiri walibaki wakalipa ile pesa na wamedumu mpaka saiv wako 3rd year. Kwahiyo uamuzi wa kubadirisha hivyo vigezo ulikuwa sahihi sana
 
Hv nini maana ya mkopo unaanzaje kumkopesha mtu aliyesoma shule ya ada milion tano kwa mwaka akapat division one halafu umuache yule aliyesona shule ada laki moja akapt division two. Embu acheni kulaum kila kitu.
Kwasababu aliesoma ada milioni 5 ana uhakika wa kuzirudisha zaidi kuliko aliesoma ada laki moja hapo lazima utumie akili
 
Back
Top Bottom